JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAGERA: WALIMU WATATU WA SHULE YA SEKONDARI KALENGE MBARONI

> TAKUKURU inawashikilia Mkuu wa Shule, Makamu na Mwalimu wa taaluma kwa kumfukuza mwanafunzi na jina lake kupewa mwanafunzi mwingine kufanyia mtihani wa Kidato cha nne 2019

> Wazazi wa mwanafunzi aliyefukuzwa walitoa taarifa TAKUKURU baada ya kuona jina la mtoto wao lina ufaulu wa daraja la pili wakati hakufanya mtihani

Soma https://jamii.app/WalimuKagera
WIZARA YA HABARI KUANZA KUTOA TUZO KWA WASANII

> Tuzo zitajumuisha sekta zote ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

> Zinatarajiwa kuongeza ushindani na kuhamasisha wasanii kufanya kazi zenye weledi na ubora zaidi

Soma https://jamii.app/TuzoWasanii
RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI 5

> Amemteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Njombe

> Ameteua Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Chalinze, Bumbuli, Urambo na Babati

Soma https://jamii.app/DCTeuziDED
#JFLeo
BAADHI YA MAMBO YANAYOWEZA KUKUFANYA UISHI VIZURI NA WATU

> Epuka hasira za hovyo na kila mtu. Usijipandikizie chuki na ubaya ktk jamii yako wala usikorofishane na watu wa karibu na wewe

> Usigombane kwa njia inayodumu kama kutuma ujumbe wa maandishi au kuwatungia wimbo watu

Soma https://jamii.app/KuishiNaWatu
#JFLeo
MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA SABASABA

> Maonesho ya biashara ya Sabasaba yalianza kama maonesho ya Kilimo ili kukuza kilimo na ushirika

> Sherehe za sabasaba zilianza kuwa Maonesho ya biashara Mwaka 1978 baada ya kuundwa Bodi ya Biashara

Soma https://jamii.app/Maonyesho77
DR CONGO: WAPIGANAJI WA ADF WAUA RAIA 800 TANGU JANUARI 2019

> ADF ni moja kati ya makundi ya wapiganaji lililoanzia Uganda na kuhamia DR Congo mwaka 1995

> Mwaka 2019 nchi hiyo ilianzisha operesheni ya kuwatokomeza Waasi hao

Soma https://jamii.app/ADF800Raia
WHO: MAGONJWA YANAYOTOKA KWA WANYAMAPORI HUUA WATU MILIONI 2 KILA MWAKA

> Utumiaji wa Wanyamapori kama kitoweo umeongeza magonjwa kwa asilimia 260 katika kipindi cha miaka 50

> WHO imesema tutarajie milipuko zaidi iwapo hatutatunza Wanyamapori na kuhifadhi mazingira

Soma https://jamii.app/WanyamaPoriVirus
MAREKANI KUZUIA MITANDAO YA KIJAMII YA CHINA IKIWEMO β€˜TIK TOK’

> Wataalamu wa kidiplomasia wa Marekani wamewaonya watumiaji wa mitandao ya Kichina wakidai wanapopakua 'Apps' hizo, taarifa zao binafsi zitaenda kwa Serikali ya China

Soma https://jamii.app/BanChineseApps
JOB LUSINDE AFARIKI. ATAKUMBUKWA KWA KUIMARISHA UHUSIANO WA TANZANIA NA CHINA

> Ni mmoja wa Mawaziri 11 wa kwanza wa Tanganyika na alikuwa Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano

> Alitunukiwa na Rais Kikwete tuzo ya "The Order of Union First Class" Aprili 4, 2011

Soma https://jamii.app/LusindeTanzia
RAIS WA BRAZIL ATANGAZA KUPATA #COVID19

- Kupitia chaneli ya Taifa, Rais Jair Bolsonaro (65) ametangaza kupata maambukizi ya #CoronaVirus baada ya kufanyiwa vipimo kwa mara ya nne

- Bolsonaro amekuwa mara kwa mara akipuuza ugonjwa huo huku akiuita ni mafua madogo ya kawaida

Soma https://jamii.app/BolsonaroCOVID19
#JFCOVID19_Updates
WAKILI BASHIR: WATIA NIA WENGI WA CCM WAMEPOTEZA SIFA YA KUTEULIWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM

> Wakili Bashir Yakub ameandika katika mtandao wa Jamiiforums.com kuwa Kanuni ya 35 ya Kanuni za Uchaguzi wa CCM za 2017 hakuna kitu kinaitwa kutangaza/kutia nia

> Amesema kama Chama kinasimamia nidhamu na kanuni kama kinavyojinasibu, hakuna shaka watu hawa wataondolewa katika orodha

Soma zaidi https://jamii.app/HojaSiasa
#JFHoja
KENYA: SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUFUNGULIWA JANUARI 2021

> Wanafunzi wa darasa la 8 na Kidato cha 4 watafanya mitihani yao ya Kitaifa mwaka 2021

> Wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la 7, na kidato cha kwanza hadi cha 3 watabaki kwenye madarasa hayo shule zikifunguliwa

Soma https://jamii.app/KenyaShule2021
MAREKANI YAJITENGA RASMI NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

> Mei 29, Rais Trump aliweka wazi nia ya kujitenga, lakini WHO ilikuwa inatumaini kuwa hatua hiyo ingeweza kuepukwa

> Rais Trump ameilaumu WHO kwa kushindwa kudhibiti #COVID19 mapema

Soma https://jamii.app/WHOvsUS
KENYA: WAANDAMANAJI ZAIDI YA 50 WANAOPINGA UKATILI WA POLISI WAKAMATWA

> Waandamanaji walikuwa wakipinga matumizi ya nguvu yanayotumiwa na Polisi wanapokamata raia

> Polisi wamesema wanaharakati hawakuwataarifu Polisi kuhusu maandamano hayo yaliyofanyika jana

Soma https://jamii.app/50Protesters
UN: WAKENYA WASIO NA UHAKIKA WA CHAKULA WATAONGEZEKA ZAIDI YA MARA MBILI MWAKA HUU

> Mwaka 2019 kulikuwa na Wakenya milioni 1.3 walioathirika na ukosefu wa chakula

> Shirika la WFP limesema Julai 2020, idadi itafikia milioni 3 hadi milioni 3.5

Soma https://jamii.app/KenyaChakula
MISRI YAWAKAMATA WANAOKOSOA HALI YA #COVID19

> Madaktari zaidi ya 10 na Waandishi wa Habari 6 wamekamatwa tangu #COVID19 kuikumba Misri

> Wanaokamatwa ni wanaozungumzia uhaba wa vifaa vya kujikinga au kudadisi idadi ya maambukizi ya #COVID19

Soma https://jamii.app/MisriWakosoaji
UGANDA: BODABODA WAISHTAKI SERIKALI KWA KUTOWARUHUSU KUENDELEA NA BIASHARA

> Chama cha waendesha bodaboda kimefungua kesi Mahakama Kuu ya Kampala kutokana na zuio kwao huku usafiri mwingine ukiruhusiwa

> Wamesema zuio linaweza kupelekea kazi haramu

Soma https://jamii.app/UgandaCyclists
MKURUGENZI WA FBI AKIRI CHINA KUWA TISHIO KWA MAREKANI

- Amesema vitendo vya upelelezi na wizi wa data vinavyofanywa na China ni tishio la muda mrefu kwa Marekani

- Amesema China imeanza juhudi kuhakikisha ndiyo Taifa pekee lenye uwezo mkubwa Duniani

Soma https://jamii.app/USA-ChinaThreats
UMUHIMU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUSTAWISHA DEMOKRASIA

> Demokrasia hutegemea uhuru wa vyombo vya habari kuweza kusimamia haki

> Haki hizo ni pamoja na uhuru wa kutoa maoni, kujieleza, kutafuta, kupokea, na kusambaza taarifa

Soma > https://jamii.app/HabariSheria
#UhuruWaKujieleza