JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NYALANDU ACHUKUA FOMU YA KUTEULIWA KUWANIA URAIS WA TANZANIA

- Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya CHADEMA

Soma https://jamii.app/NyalanduFomuUrais
#Uchaguzi2020
ARUSHA: JOSHUA NASSARI KUJIUNGA RASMI NA CCM

- Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ametangaza kujiunga na CCM akitokea CHADEMA

- Nassari aliyevuliwa Ubunge kutokana na Utoro amepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James

Soma https://jamii.app/NassariCCM
#JFSiasa
TETESI: REAL MADRID KUANZA UPYA MPANGO WA KUMSAJILI PAUL POGBA

- Real Madrid imeupa kipaumbele usajili wa Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba katika dirisha la usajili lijalo

- Inaelezwa Zinedine Zidane na klabu yake ya Real Madrid imemuwinda Pogba kwa muda mrefu

#Sports #JFMichezo
SERBIA: MAELFU WAANDAMANA KUPINGA KUTAKA KUREJESHWA KWA ZUIO LA KUBAKI NDANI

> Waandamanaji wameilaumu Serikali yao kufungua nchi hiyo kwa sababu za kisiasa hapo awali na sasa kutaka kurejesha zuio

> Serikali imesema inataka kurejesha zuio la kutotoka ndani kwa muda ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi

Soma https://jamii.app/SerbiaProtests
GASPER MWANALYELA ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA

> Wakili Gaspar Mwanalyela ameahidi kufuata nyayo za Baba wa Taifa, Julius Nyerere

> Amesema ataanzisha Vijiji vya Ujamaa na Vijiji vya Wataalamu kama wa Kilimo

Soma https://jamii.app/UraisChadema2020
#CORONAVIRUS-KENYA: IDADI YA MAAMBUKIZI YAFIKIA 8,528 BAADA YA VISA 278 KUONGEZEKA

- Ni baada ya sampuli 3,053 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita

- Wagonjwa waliopona wamefikia 2,593 huku waliofariki wakifikia 169

Soma https://jamii.app/COVID19KE-8528
#JFCOVID19_Updates
UDSM YATENGENEZA MAFUTA YATOKANAYO NA MITI KWA AJILI YA KUJIFUKIZA

> β€˜Fukiza Udanol’ ni mafuta tete yaliyotokana na miti ili kurahisisha kujifukiza

> Meneja Mradi wa dawa hiyo amesema mafuta hayo yatumikapo kujifukizia hutibu maradhi mbalimbali

Soma https://jamii.app/UdanolUDSM
KENYA YAANZA KUTUMIA β€˜INTERNET BALLOONS’ ZA KUWEZASHA WATU KUTUMIA 4G

> Ni baada ya kampuni ya Telkom ya Kenya kuingia ubia na kampuni ya Alphabet

> Teknolojia hii inatumia nishati ya Jua ambapo puto huelea futi 60,000 juu ya usawa wa Bahari

Soma https://jamii.app/InternetBalloonsKE
#JFLeo
LIGI KUU TANZANIA BARA: BINGWA WA LIGI, SIMBA SC YAKABIDHIWA KOMBE

- Klabu ya Simba imekabidhiwa Kombe lao la 21 la Ligi Kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Majaliwa Mkoani Lindi

- Uongozi wa Simba SC umetoa shukrani za dhati kwa Mungu na kisha kwa mashabiki zao

#JFSports
MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JUNI UMEBAKI KUWA 3.2% KAMA MEI

- Baadhi ya bidhaa za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Juni 2020 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019

- Baadhi ya bidhaa hizo ni Unga wa Mahindi kwa 1.6%, Matunda kwa 2.1%, viazi mviringo 0.5% na mihogo 13.3%

Soma https://jamii.app/MfumukoBei-6-2020
TUNDU LISSU: NATARAJIA KURUDI NCHINI MWANGU JULAI 28, 2020

- Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), Tundu Lissu akiwa kwenye Mkutano ulioandaliwa kwa njia ya Mtandao na Taasisi ya 'The Resistance Bureau', amesema ameshakata tiketi ya ndege

Soma https://jamii.app/TunduLissuKurejea
#JFSiasa
CHINA YAKUBALI WHO KUTUMA WATAALAMU BEIJING KUFANYA UCHUNGUZI WA #COVID19

- Kwa mujibu wa CRI-Swahili, Wizara ya Mambo ya Nje imesema #China imekubali Shirika la Afya Duniani (WHO) kutuma Wataalamu nchini humo kutafuta chanzo cha #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/ChinaWHO-COVID19
#JFCOVID19_Updates
INDIA: DAWA ZINAZOSADIKIWA KUPUNGUZA MAKALI YA #COVID19 ZAUZWA KIMAGENDO

> Remdesivir na Tocilizumab zinadaiwa kuwa na uwezo wa kuondoa dalili za #COVID19 ndani ya siku 15

> Wataalamu hawajathibitisha lakini Madaktari wanazidi kuwaandikia watu dawa hizo

Soma https://jamii.app/DawaCOVID19India
IVORY COAST: WAZIRI MKUU AFARIKI BAADA YA KUUGUA AKIWA KWENYE KIKAO

- Amadou Gon Coulibaly (61) aliyewahi kufanyiwa upasuajj wa moyo mwaka 2012, alijisikia vibaya akiwa kwenye kikao cha Mawaziri na kukimbizwa hospitalini alikofariki

- Alirejea nchini humo Julai 02 baada ya kukaa Ufarasa kwa muda mrefu akifanyiwa vipimo vya moyo

Soma https://jamii.app/PMCoulibalyDies
#Tanzia
DKT. KALEMANI: UMEME USIUZWE ZAIDI YA TSH. 100 KWA UNIT 1 KWA WENYE MATUMIZI YA KAWAIDA

> Waziri wa Nishati amewaonya wazalishaji wa umeme wanaowatoza raia bei kubwa zaidi ya bei elekezi

> Alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi hasa wanaoishi visiwani

Soma https://jamii.app/BeiUmeme100
UN: JANGA LA #COVID19 LIMESABABISHA ONGEZEKO LA VIFAA TIBA BANDIA DUNIANI

> Limesababisha uhalifu wa kurubuni watu na biashara bandia huku wahalifu wakitumia wavuti za Kampuni zinazofahamika na kushawishi wanunuzi kuwa ni Kampuni halali

Soma https://jamii.app/COVID19BidhaaFeki
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MJANE WA ALIYEKUWA KAIMU JAJI MKUU WA ZANZIBAR ANATAFUTWA KWA KUHARIBU NYUMBA YA ZHC

> Salma Mkusa alitakiwa kuhama kwenye nyumba ya Shirika la Nyumba Zanzibar alimokuwa akiishi na mumewe

> Kabla ya kuhama, aliamua kuharibu maboresho aliyoyafanya kwenye nyumba hiyo

Soma https://jamii.app/MjaneWaJaji
WANASAYANSI WAONYA JUU YA UWEZEKANO WA #COVID19 KUDHURU UBONGO

- Utafiti wa 'University College London (UCL)' umeonesha Wagonjwa 43 wenye #COVID_19 waliopata shida ya muda kwenye Ubongo, Kiharusi, uharibifu wa neva na shida nyingine katika ubongo

Soma https://jamii.app/COVID19-Ubongo
#JFCOVID19_Updates
BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA YAZINDUA KAMPENI YA KUWAEPUSHA WATOTO NA KAMARI

> Imezindua kampeni ijulikanayo kama β€˜Mlinde mtoto’

> Kampeni hii itawalinda watoto na kuihimiza jamii kutoa taarifa za watoto wanaoshiriki Kamari

Soma https://jamii.app/GBTMlindeMtoto
LEONARD TOJA MANYAMA ACHUKUA FOMU KUOMBA KUTEULIWA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA

- Manyama ambaye ni Mwalimu na Mtaalam wa Mipango Miji amesema kaulimbiu yake ni "Niamini Nikuvushe"

- Amesema akiwa Rais ndani ya siku 100 atarekebisha fao la kujitoa

Soma https://jamii.app/ManyamaTZ-CDM
#Uchaguzi2020