JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ISAYA MWITA ACHUKUA FOMU KUOMBA KUTEULIWA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA

- Mwita aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar anakuwa mgombea wa 6 kuchukua fomu hiyo

- Kaulimbiu yake ni "Mageuzi ya mfumo wa elimu, upanuaji na uongezaji wa ajira kwa vijana na mchakato wa Katiba Mpya"

Soma https://jamii.app/IsayaMwitaTZ-CDM
#Uchaguzi2020
TETESI: KAI HAVERTZ ANATAMANI KUUNGANA NA TIMO WERNER NDANI YA CHELSEA

- Inaelezwa Chelsea inataka kutumia shahuku ya Kiungo huyo kuondoka Bayer Leverkusen ili imsajili

- Inadaiwa Kai ataiambia Leverkusen anataka kuondoka katika dirisha la usajili litakalofunguliwa karibuni

#JFMichezo #Sports
LIVINGSTONE LUSINDE AHOJIWA NA TAKUKURU AKITUHUMIWA KUGAWA RUSHWA

> Aliyekuwa Mbunge wa Mtera alihojiwa kuhusu tuhuma za kuwakusanya watu na kuwapa rushwa ili nao wakawashawishi wengine waweze kumpigia kura katika kura za maoni

Soma https://jamii.app/LivingstoneLusinde
#JFSiasa #KemeaRushwa
SERUKAMBA ASHIKILIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA

> Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba anashikiliwa kwa tuhuma za kutaka kutoa rushwa kwa wajumbe wa CCM na wapiga kura wake

> Uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea

Soma https://jamii.app/PCCBSerukamba
#KemeaRushwa
SAKATA LA BANGI ARUSHA: WATENDAJI WA KIJIJI NA KATA YA MWANDETI WASIMAMISHWA KAZI

> Mkuu wa Mkoa, Idd Kimanta amefanya ziara Wilayani Arumeru baada ya maelekezo ya Rais Magufuli

> Amewataka viongozi kuwafichua wote wanaofanya kilimo cha Bangi

Soma https://jamii.app/WatendajiKaziMeru
ARUSHA: Waziri Selemani Jafo amemuondoa kwenye nafasi yake, Meneja wa TARURA Jijini humo, Podia Mwankenja kwa kushindwa kukusanya Wananchi kwenye ufunguzi wa barabara

- Amesema Meneja huyo amefanya 'sabotage' ili Rais Magufuli aonekane hajafanya kitu

Soma https://jamii.app/JafoMenejaTARURA-AR
IRINGA: WASICHANA WAANZA KUPIMWA MIMBA BAADA YA SHULE KUFUNGULIWA

> Manispaa ya Iringa imeanza kuwafuatilia wanafunzi ili kuwabaini wanafunzi watoro na wajawazito

> Awali, Shinyanga iliripoti wanafunzi 101 kupewa mimba kipindi cha likizo ya Corona

Soma https://jamii.app/IringaMimbaWanafunzi
MAMBO YALIYOAINISHWA KTK TAMKO LA MISINGI YA UHURU WA KUJIELEZA BARANI AFRIKA

> Kuwapo kwa tasnia ya utangazaji habari yenye washiriki wa aina mbalimbali, vyombo huru vinavyomilikiwa na watu au taasisi binafsi, kuliko kuwapo kwa ukiritimba wa Dola

> Uwajibikaji wa vyombo vya utangazaji vya umma kwa Wananchi kupitia muhimili wa kutunga sheria (Bunge), kuliko muhimili wa utawala pekee

> Kuwepo kwa mfumo wa usajili wa magazeti na machapisho usioweka vikwazo dhidi ya #UhuruWaKujieleza

> Sheria dhidi ya kashfa zisizozuia usambazaji wa habari au taarifa zenye maslahi

> Kulinda vyanzo vya habari au taarifa za siri isipokuwa ktk mazingira maalumu yaliyoainishwa

Soma > https://jamii.app/MkatabaHakiZaBinadamu
#CORONAVIRUS: KENYA YATANGAZA ONGEZEKO LA WAGONJWA WAPYA 447

- Sampuli 3,803 zimepimwa ndani ya saa 24 zilizopita. Maambukizi yamefikia 8,975

- Watu 4 wamefariki na jumla ya vifo imefikia 173. Watu 64 zaidi wamepona na waliopona wamefikia 2,657

Soma https://jamii.app/COVID19KE-8975
#JFCOVID19_Updates
ALIYEKUWA MBUNGE WA SAME MAGHARIBI, DKT. MATHAYO DAVID AHOJIWA NA TAKUKURU

- TAKUKURU imemuhoji na kuyashikilia magari 10 ya Wagonjwa aliyokuwa ayagawe katika Kata 10 za Jimbo la Same Magharibi kama utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka 2015

Soma https://jamii.app/MathayoDavidPCCB
#KemeaRushwa
MALAWI: RAIS CHAKWERA AKOSOLEWA KWA KUTEUA NDUGU KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

- Sidik Mia ni Waziri wa Uchukuzi na mkewe, Abida Mia ni Naibu Waziri wa Ardhi

- Kenny Kandodo ni Waziri wa Kazi na dada yake, Khumbize Kandodo ni Waziri wa Afya

- Mfanyabiashara Gospel Kazako amekuwa Waziri wa Habari huku Shemeji yake, Agnes Nkusa Nkhoma akiwa Naibu Waziri wa Kilimo

Soma https://jamii.app/MawaziriMalawi
#JFLeo
KIGOMA: ALBERT OBAMA MATATANI, AKUTWA NA TAKUKURU AKIGAWIA HELA WAJUMBE

> TAKUKURU inachunguza tukio la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Buhigwe kuitisha kikao na kuwapa pesa wajumbe 21

> Tsh. 210,000 zimekamatwa huku mtuhumiwa akisalimisha Tsh. 2,000,000

Soma https://jamii.app/PCCBKigoma
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKUU WA WILAYA NA MKURUGENZI

- Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega

- Solomon Isack Shati ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang

Soma https://jamii.app/Uteuzi-DC-DAS
WAZIRI MKUCHIKA AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA 2

- Amemteua Omary Mwanga kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea

- Amemteua aliyekuwa Afisa Tarafa Wilayani Mbulu, Saitoti Zelothe Stephen kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya

Soma https://jamii.app/Uteuzi-DC-DAS
PWANI: KIJANA AUAWA NA RAIA BAADA YA KUWAUA WATOTO WAWILI KIKATILI

> Yasin Abdala ameuawa na raia alipojaribu kutoroka kwenye ofisi ya Kijiji alimofungiwa baada ya kukamatwa na kwa kosa la kuwaua watoto 2 kwa mapanga na kumjeruhi mama wa watoto hao

Soma zaidi https://jamii.app/PwaniKijanaWatoto
RAIS MAGUFULI ATEUA WAKILI MKUU WA SERIKALI NA NAIBU WAKE

- Gabriel Pascal Malata ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba

- Dkt. Boniface Luhende ameteuliwa kuwa Naibu Wakili Mkuu akichukua nafasi ya Gabriel Pascal Malata

Soma https://jamii.app/UteuziWakiliSerikali
MAJINA MATATU YALIYOPENDEKEZWA KWA NEC-CCM KUWANIA URAIS ZANZIBAR YATANGAZWA

- Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru ametangaza majina matatu yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa

- Waliopendekezwa ni Dkt. Khalid Salim Mohammed, Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha

Fuatilia https://jamii.app/MgombeaCCM-ZNZ
#Uchaguzi2020
SIMBA RICHMOND AKARO NEO ACHUKUA FOMU KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA

> Wakili Simba Richmond Akaro Neo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Tanzania

> Ni mtu wa 7 kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CHADEMA

Soma https://jamii.app/Uchaguzi2020Chadema
#JFSiasa
CCM IMEMCHAGUA HUSSEIN MWINYI KUWA MGOMBEA WA URAIS ZANZIBAR

- Hussein Mwinyi amechaguliwa kwa kupata kura 129 katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM uliofanyika leo

- Amewashinda Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16 na Khalid Mohamed aliyepata kura 19

Zaidi, soma https://jamii.app/MgombeaCCM-ZNZ
#Uchaguzi2020
HALMASHAURI KUU YA CCM IMEMPENDEKEZA DKT. JOHN MAGUFULI KUWANIA URAIS WA TANZANIA

- Ni baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri hiyo kupendekeza jina lake akiwa ni Mgombea pekee aliyechukua fomu kuwania Urais

- Jina litapelekwa katika Mkutano Mkuu utakaofanyika kesho ili lipitishwe

#Uchaguzi2020