JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DROO YA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

- Atakayepita katika mchezo kati ya Bayern Munich na Chelsea atakutana na atakayepita kati ya Barcelona na Napoli

- Aidha, atakayepita kati ya Manchester City na Real Madrid atakutana na atakayepita kati ya Juventus na Lyon

- Michezo yote ya robo fainali itachezwa kati ya Agosti 12-15. Michuano hiyo itachezwa kwa siku 12 huko Ureno na fainali itakuwa Agosti 23 Jijini Lisbon

#Michezo #Sports #JFSports #JamiiForums #JFMichezo
DROO YA ROBO FAINALI - MICHUANO YA LIGI YA EUROPA

- Michezo ya hatua ya 16 bora ambayo haikuchezwa kutokana na #CoronaVirus itachezwa Agosti 5-6

- Michezo ya robo fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 10-11 nchini Ujerumani huko Cologne, Dusseldorf, Duisburg au Gelsenkirchen

#Michezo #JamiiForums #JFSports #JFMichezo #Sports
Baadhi ya maneno ya Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimsifia Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake, Dkt. Ali Mohammed Shein

- Rais Magufuli amemsifia Rais Shein katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ilipokuwa inachagua mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho

#Uchaguzi2020 #JFSiasa #Siasa
ARUSHA: KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KG 1,378.4 ZA BANGI

> Seuri Kisamu (34) na Losieku Mollel (35), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakikabiliwa na kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na Bangi

Soma https://jamii.app/UhujumuUchumi
MALAWI: WANANCHI WANAANDAMANA KUPINGA TEUZI ZA RAIS

> Ni baada ya Rais Lazarus Chakwera kuwateua watu ambao ni ndugu kwenye Baraza la Mawaziri

> Rais Chakwera aliwahi kumkosoa Rais Mutharika kwa tabia hiyo alipokuwa madarakani

Soma https://jamii.app/MalawiDemonstrations
UTEUZI WA BALOZI: DAVID CONCAR KUCHUKUA NAFASI YA SARAH COOKE

> David Concar ameteuliwa kuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania akichukua nafasi ya aliyekuwa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ambaye amepangiwa majukumu mengine ya kidiplomasia

Soma https://jamii.app/UbaloziUingerezaTZ
JOSHUA LAWRENCE ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS KUPITIA ACT WAZALENDO

- Amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania Urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT Wazalendo

- Ameahidi kushughulikia Kilimo na Ufugaji akihakikisha kila mwananchi anafuga Kuku wasiopungua 1,000

Soma https://jamii.app/UraisACT2020
#Uchaguzi2020
MALEZI: FAIDA ZA MTOTO KULELEWA NA BABA NA MAMA

> Wadau wa JamiiForums wanadai mtoto akilelewa na mzazi mmoja atakua lakini tafiti zinaonesha wanaolelewa na pande zote mbili huwa na tabia bora zaidi

> Mtoto akilelewa na mzazi mmoja huweza kukosa baadhi ya mahitaji endapo mzazi husika hana uchumi imara

Je, una maoni gani kuhusiana na hoja hiyo?

Kujadili, tembelea https://jamii.app/WatotoMalezi
#JFMalezi
AHUKUMIWA JELA MIAKA MIWILI AU FAINI YA TSH. 500,000 KWA KUMILIKI KOBE BILA KIBALI

> Daniel Chizua wa Masaki, Dar amekiri kukutwa na Kobe wawili wenye thamani ya Tsh. 320,000

> Pia, ametakiwa kulipa Tsh. 650,000 baada ya kuongea na DPP

Soma https://jamii.app/KobeLeseniNyara
UMUHIMU WA KUFANYA β€˜CHECK UP’ YA MIFUMO YA UMEME KWENYE GARI LAKO

> Kutokagua mifumo ya umeme inaweza kukufanya uingie gharama kubwa na hata kugharimu maisha kutokana na hitilafu zinazoweza kutokea

> Gari likiwa na shida ya umeme betri hutumika hata ukizima gari, hivyo betri hufa mapema. Usiporekebisha, hata betri jipya litakufa ndani ya muda mfupi

Soma https://jamii.app/GariUmemeUkaguzi
#JFGarage
DODOMA: DAS WA HANDENI AFARIKI KWENYE AJALI, MBUNGE AJERUHIWA

> Watu 3 wamefariki akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, Mwalimu Boniface Maiga baada ya gari mbili kugongana

> Polisi wamethibitisha Mbunge wa Handeni, Omary Abdallah Kigoda kuwa mmoja wa majeruhi

Soma https://jamii.app/AjaliDodomaDAS
FACEBOOK YAFUTA VIDEO YA GWAJIMA ILIYOHUSISHA #COVID19 NA 5G

> Askofu Gwajima alidai janga la #CoronaVirus lina uhusiano na Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ya 5G

> Facebook walishatangaza kudhibiti taarifa za kupotosha kuhusu #COVID19

Soma https://jamii.app/GwajimaFBCOVID19
IBRAHIM LIPUMBA: FURAHA KWA WATANZANIA INAWEZEKANA

> Profesa Ibrahim Lipumba, amesema katika uchaguzi wa 2020 CUF inakuja na ajenda ya β€œFuraha kwa Watanzania inawezekana”

> Pia, amewaomba CCM kupambana kwa hoja katika kipindi cha kampeni

Soma https://jamii.app/MkutanoCCM2020
#JFSiasa
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MZEE MWINYI: MAGUFULI APEWE KIPINDI KINGINE CHA β€˜ASANTE’

> Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amesema β€œNi muhimu kuifuata Katiba lakini tunaweza kumuongezea Rais Magufuli kipindi kingine cha β€˜Asante’”

Soma https://jamii.app/MkutanoCCM2020
#JFSiasa
RAIS MAGUFULI AWAOMBA WAZANZIBARI WASIMCHAGULIE MTU ATAKAYEMUAMKIA

> Rais Magufuli amesema amemzidi umri mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi

> Amewaomba wasimchagulie mtu ambaye akienda kuongea naye lazima aanze na β€˜shikamoo’ kwani zinachosha

Soma https://jamii.app/MkutanoCCM2020
#JFSiasa
RAIS MAGUFULI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS WA CCM KWA 100% YA KURA ZA WAJUMBE

> Amepita kwa kupata kura za β€˜Ndiyo’ 1,822 zilizopigwa na Wajumbe 1,822

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally alisema, Rais Magufuli ni mgombea pekee kwani hakuna mwingine aliyejitokeza kuchukua fomu

Soma https://jamii.app/MkutanoCCM2020
#JFSiasa