JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WHO: HALI YA CORONA INAWEZA KUWA MBAYA ZAIDI SERIKALI ZISIPOTEKELEZA SERA SAHIHI

- Mkuu wa Shirika la Afya, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema janga la #COVID19 bado lipo

- Amesema nchi nyingi zimepiga hatua, lakini ugonjwa unaendelea kushika kasi

Soma https://jamii.app/WHOCoronaDuniani
ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA, MRISHO GAMBO AHOJIWA NA TAKUKURU

> Kwa mujibu wa Gazeti la Jamhuri, Mrisho Gambo amehojiwa na TAKUKURU akituhumiwa kugawa rushwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Arusha wanaohusika kupitisha jina la mgombea Ubunge

> Gazeti hilo limeeleza kuwa inadaiwa Gambo amekuwa na matamanio ya kuwania Ubunge jijini Arusha

Soma - https://jamii.app/GamboTakukuru
MALAWI: RAIS LAZARUS CHAKWERA AMUONDOLEA KINGA YA KUTOSHTAKIWA MUTHARIKA

> Saa 24 tangu ashike madaraka, Chakwera amemuondolea kinga ya kutoshtakiwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Peter Mutharika

> Pia, amemfuta kazi Mkuu wa Polisi na kuwataka Mawaziri kurudisha mali za Serikali

Soma https://jamii.app/MutharikaImmunity
#JFLeo #Siasa
UGANDA: VISA VYA #COVID19 VYAFIKIA 889. WATANZANIA 7 WARUDISHWA

- Serikali imethibitisha visa vipya 19 baada ya kupima sampuli 2,170

- Madereva wa Kenya-15, Tanzania-7, Misri-2 na Burundi-1 wamerudishwa nchini mwao kwa kukutwa na maambukizi

Soma https://jamii.app/Corona889-UG
#JFCOVID19_Updates
INDIA: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU 'APP' ZA CHINA, YASEMA NI TISHIO KWA NCHI

- Serikali ya India imepiga marufuku 'app' 59 za China zikiwemo TikTok, WeChat na UC Browser

- Ni kufuatia malalamiko kuwa zinaiba na kuhamisha taarifa za watumiaji

Soma - https://jamii.app/IndiaBansChinaApps
MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU DR CONGO: MFALME WA UBELGIJI AELEZA MAJUTO YA UTAWALA WAO

- Mfalme Philippe amesema hayo katika barua aliyomuandikia Rais Tshisekedi

- Ubelgiji ilitawala DR Congo kwa miaka kadhaa hadi 1960 ilipopata uhuru

Soma https://jamii.app/UbelgijiUkoloniCongo
SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO(2015): UJUE WAJIBU WA WATOA HUDUMA

> Kifungu 39: Kinazuia watoa huduma kufuatilia taarifa anayoisambaza au kuihifadhi, au kutafuta taarifa za viashiria vya shughuli zinazohusisha uvunjaji wa sheria

> Waziri anaweza kuwataka watoa huduma kuziarifu mamlaka kuhusu shughuli zozote zinazodaiwa kuhusisha uvunjanji wa sheria

https://jamii.app/MakosaSheriaMtandao

#UhuruWaKujieleza
#CORONAVIRUS KENYA: VISA VYAFIKIA 6,366, WAGONJWA 2,039 WAPONA

- Wagonjwa wapya 176 wamethibitishwa baada ya sampuli 2,419 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita

- Pia, wagonjwa 4 wamefariki dunia na idadi ya vifo imefikia 148

Soma - https://jamii.app/Corona6336-KE

#JFCOVID19_Updates
ARUSHA: TAKUKURU YAKANUSHA KUMHOJI MRISHO GAMBO

> TAKUKURU imekanusha taarifa kuwa imemhoji aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa Wajumbe wa CCM wanaohusika na kupitisha jina la mgombea Ubunge

Soma - https://jamii.app/KanushoGamboRushwa
DAR: BEI YA PETROLI, DIZELI KUONGEZEKA KUANZIA JULAI 1

- EWURA imesema mabadiliko hayo yamechangiwa na mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia

- Bei ya mafuta ya taa haijapanda kwasababu hayajaingizwa nchini kupitia Bandari ya Dar

Soma https://jamii.app/EWURAMafutaBei
KAMPUNI YA MOIL YALIPA FAINI YA TSH. MILIONI 10 KWA KUHUJUMU MAFUTA

> EWURA imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha na kulipa faini ya Tsh. Milioni 10

> Aidha, kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Olympic Petroleum lipo pale pale baada ya Kampuni hiyo kukaidi maelekezo

Soma - https://jamii.app/FidiaUhujumuMafuta
POLISI WAAGIZWA KUKAMATA WANAOFUNGA VING'ORA KWENYE MAGARI

- Polisi na Wakuu wa Usalama wameagizwa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wanaofunga ving’ora, vimulimuli, taa za mwanga mkali na zinazobadilika rangi bila kibali

Soma - https://jamii.app/PolisiMagariSheria
HOJA: KWANINI SIKU HIZI VIJANA WADOGO WANA KIWANGO KIKUBWA CHA MSONGO WA MAWAZO?

> Mdau wa JamiiForums anadai miaka ya hivi karibuni imekuwa ni hali ya kawaida kukuta kijana wa Sekondari au Chuo Kikuu akilalamika kuwa na msongo wa mawazo hali inayopelekea baadhi yao kujidhuru au kujiua

> Anauliza hali hiyo husababishwa na nini? Je, ni kukosa malezi mazuri au ni hali ngumu za kiuchumi kwenye familia zao? Je, ni changamoto za kimapenzi?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/DepressionVijana
#JFLeo #Depression
KATAVI: AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KOSA LA KUMUUA MKE WAKE MAKUSUDI

> Mahakama ya Hakimu Mkazi imemhukumu kunyongwa hadi kufa Susumo Shija (53) kwa kosa la kumuua Ng'washi Nkuba kwa makusudi baada ya kumtuhumu kumuua mwanaye mdogo kwa imani za kishirikina

Soma - https://jamii.app/KunyongwaMauaji
SERIKALI KUACHA KUTUMIA NGUZO ZA MITI KWENYE NISHATI YA UMEME

> Serikali itaachana na matumizi ya nguzo za umeme zitokanazo na miti na kutumia nguzo za zege ili kuepukana na adha ya nguzo kuoza na kusababisha ukatikaji wa umeme

> Mradi umeanza kwa baadhi ya maeneo ya Kibaha na kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere ikiwa lengo ni kuweka nchi nzima

Soma https://jamii.app/NguzoZege
MHARIRI WA MAGAZETI YA SERIKALI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Osca Joseph Mbuza amefikishwa Mahakama ya Wilaya Temeke na ameshtakiwa kwa kushawishi, kuomba na kupokea rushwa

- Aliomba Dola 6,000 na baadae alibadili na kutaka apewe Milioni 5

Soma https://jamii.app/RushwaMhaririSerikali
SHERIA YA KUMILIKI LAINI 1 KWA KILA MTANDAO YAANZA KUTEKELEZWA LEO

> Ikibainika unamiliki laini zaidi ya moja kutoka kwenye kampuni moja ya simu adhabu yake ni faini ya Tsh. Milioni 5 au kifungo jela mwaka 1 au vyote kwa pamoja

> TCRA imesema sheria haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada

Soma - https://jamii.app/SheriaLaini1
MAREKANI: JOE BIDEN ASEMA HATOFANYA KAMPENI WAKATI WA CORONA

- Mpinzani huyo wa Rais Trump amesema atafuata maelekezo ya wataalamu kwa manufaa ya nchi nzima

- Marekani imerekodi visa 2,868,012, vifo 132,834 na wagonjwa 1,084,341 wamepona

Soma - https://jamii.app/JoeBidenKampeniUrais
MAMLAKA YA TCRA JUU YA WAZALISHA MAUDHUI WA MTANDAONI

> Kifungu 4(1)(a): kinaitaka TCRA kuwa na rekodi ya blogu, majukwaa, redio na televisheni za mtandaoni

> Usajili huu ni kinyume na matakwa ya intaneti na uhuru wa kujieleza

> Kifungu 4 (1) (b): Kinazipa nguvu mamlaka kuchukua hatua dhidi ya wasiofuata taratibu za usajili

> Moja ya hatua ni pamoja na kuamuru uondolewaji wa maudhui

> Utaratibu huu unawajengea woga Wananchi

Soma > https://jamii.app/MakosaSheriaMtandao
#UhuruWaKujieleza
JECHA: SIJAVUNJA KATIBA KUTAKA KUGOMBEA URAIS

> Aliyekuwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha amesema ni haki yake kugombea kama Mtanzania yeyote

> Amesema alifuta matokeo ya Urais baada ya mmoja wa wagombea kuchapisha karatasi za kura

Soma https://jamii.app/JechaUraisZbar
#JFSiasa