JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZAIDI YA SAFARI 6,000 ZA NDEGE ZAFUTWA

Kulingana na tovuti ya Flightware.com zaidi ya safari 6,000 za Ndege zimefutwa Duniani kote tangu Desemba 25

Mashirika mengi yametaja Kirusi cha #Omicron kuwa sababu ya kufuta safari hizo

Soma - https://jamii.app/OmicronFlights
#UVIKO3
MAREKANI: WASIO NA DALILI ZA COVID-19 KUJITENGA KWA SIKU TANO

Waliokutwa na Virusi baada ya kujitenga kwa Siku 10 wanapaswa kuvaa Barakoa kwa Siku 5 wanapokuwa karibu na wengine

#Omicron inachukua 73% ya maambukizi ya Corona Nchini Marekani

Soma https://jamii.app/5DaysNteenUS
#UVIKO3
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema athari inayotokana na Kirusi cha Corona aina ya Omicron bado ipo juu. Maambukizi ulimwenguni yameongezeka kwa 11% wiki iliyopita

Ushahidi waonesha #Omicron ina ukuaji wa haraka zaidi

Soma - https://jamii.app/WHOOmicron

#UVIKO3
ISRAEL YAWA NCHI YA KWANZA KUTOA CHANJO YA NNE YA #COVID19

Ongezeko la maambukizi ya #Omicron limefanya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wapewe 'booster' ya pili

Wengine wanaopewa kipaumbele ni wenye Magonjwa Sugu na Wahudumu wa Afya

Soma https://jamii.app/SecondBoosterDose

#UVIKO3 #JFAfya
UFARANSA YARIPOTI AINA MPYA YA #COVID19, WAKIITA 'IHU'

Watu 12 wamekutwa na kirusi hicho kiitwacho B.1.640.2 au IHU

> Shirika la Afya Duniani (WHO) likithibitisha uwepo wa kirusi hicho kitaweza kuitwa 'Pi' ndio herufi inayoifuata #Omicron

Soma https://jamii.app/UfaransaIHU

#UVIKO3 #JFAfya
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Visa Milioni 9.5 vimeripotiwa ulimwenguni Wiki iliyopita

Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Kirusi cha #Omicron hakipaswi kuainishwa kama 'Hakina makali' kwani kinaua watu

Soma - https://jamii.app/OmicronWHO

#UVIKO3 #JFAfya
WHO: 50% YA WATU BARANI ULAYA WATAAMBUKIZWA OMICRON

Shirika la Afya (WHO) lasema nusu ya watu wataambukizwa #Omicron kipindi cha wiki 6 - 8 zijazo

Makadirio yanatokana na Visa vipya Milioni 7 vilivyoripotiwa Ulaya wiki ya kwanza ya 2022

Soma - https://jamii.app/OmicronUlaya

#UVIKO3 #JFAfya
MICHEZO: Tiketi za Michezo ya Olimpiki ya Msimu wa Baridi 'Winter Olympics' iliyopangwa kuanza Februari 4, 2022 huko Beijing zitatolewa kwa makundi kadhaa ya watu na hazitauzwa kwa Umma

China inapambana kudhibiti maambukizi ya #Omicron

Soma - https://jamii.app/BeijingWO

#JFSports
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwa wiki iliyopita pekee, Kirusi cha #Omicron kimepelekea maambukizi mapya Milioni 18 ulimwenguni

WHO imeeleza wasiwasi wake kuhusu Nchi nyingi kuwa na kasi ndogo ya utoaji Chanjo

Soma - https://jamii.app/KirusiOmicronWHO

#UVIKO3 #JFAfya
UINGEREZA YALEGEZA KANUNI ZA #COVID19

Barakoa hazitokuwa lazima maeneo ya Umma na Shule. Raia hawataendelea kusisitizwa kufanya kazi Nyumbani

Wanasayansi wanaamini Wimbi la maambukizi yaliyotokana na Kirusi cha #Omicron limefikia kilele

Soma - https://jamii.app/KanuniCoronaUK

#UVIKO3 #Governance #JFAfya
ISRAEL YADHIBITI #OMICRON BAADA YA KUTOA DOZI YA NNE

Wizara ya #Afya ya Israel imesema Watu wenye umri wa miaka 60 na kuendelea waliopata Chanjo ya nne wameonesha kuwa na kinga ya Ugonjwa mara tatu zaidi kuliko wale waliopata Dozi tatu

Soma - https://jamii.app/DoziYaNne

#UVIKO3 #JFAfya
PFIZER NA BioNTech WAANZA MAJARIBIO YA CHANJO YA #OMICRON

Majaribio yatajumuisha Watu zaidi ya 1,400 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55

Wamegawanywa ktk makundi; waliopata Chanjo 2, waliopata Chanjo 2 na Booster, na wale wasiopata Chanjo

Soma - https://jamii.app/OmicronChanjo

#UVIKO3 #JFAfya
#COVID19: Korea Kusini imerekodi maambukizi 13,102 huku Mamlaka zikionya Kirusi cha Corona aina ya #Omicron kinaweza kuchangia hadi 90% ya maambukizi mapya wiki zijazo

Ni mara ya kwanza Visa zaidi ya 13,000 kurekodiwa katika Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/OmicronSK

#UVIKO3 #JFAfya
UJERUMANI NA AUSTRIA KULEGEZA KANUNI ZA #COVID19

Ujerumani italegeza Kanuni kufuatia Wimbi la Maambukizi kutokana na Kirusi cha #Omicron kuonekana limepita kilele chake

Serikali ya Austria italegeza asilimia kubwa ya Kanuni kuanzia Machi 5

Soma https://jamii.app/KanuniUVIKO

#UVIKO3 #Governance