JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#COVID19: Korea Kusini imerekodi maambukizi 13,102 huku Mamlaka zikionya Kirusi cha Corona aina ya #Omicron kinaweza kuchangia hadi 90% ya maambukizi mapya wiki zijazo

Ni mara ya kwanza Visa zaidi ya 13,000 kurekodiwa katika Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/OmicronSK

#UVIKO3 #JFAfya
UAE KUONDOA MARUFUKU KWA WASAFIRI KUTOKA NCHI 12 ZA AFRIKA

Mataifa hayo ni Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia, Congo, Botswana, Eswatini, Lesotho, Msumbuji, Namibia na Zimbabwe

Marufuku iliwekwa kutokana na Kirusi cha Omicron

Soma https://jamii.app/UAEBanLifted

#UVIKO3
RWANDA: WASIOPATA CHANJO KUTORUHUSIWA MAENEO YA UMMA

Serikali imewataka Wananchi kupata Chanjo kamili ya #COVID19 ili kuruhusiwa kuingia maeneo ya umma

Watu milioni 7 wameshapata Chanjo kamili na zaidi ya milioni 8 wamepata Chanjo ya kwanza

Soma https://jamii.app/RwandaUmma

#UVIKO3
UFARANSA: Watu 13 wamekamatwa kwa kutengeneza na kuuza vyeti bandia 62,000 vya #COVID19 jijini Paris na Lyon

Uchunguzi umebaini kundi hilo la wahalifu lilidukua akaunti ya nesi wa kituo cha Afya na kuanza kufoji vyeti hivyo

Soma - https://jamii.app/FakeCOVID19Pass

#UVIKO3
INDIA: MAAMBUKIZI YA COVID-19 YAPUNGUA DELHI, MIGAHAWA YAFUNGULIWA

Migahawa, baa na kumbi za sinema zitaruhusiwa kufanya kazi kwa sharti la kuchukua watu 50% ya uwezo

#Delhi ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na Wimbi la Tatu

Soma https://jamii.app/COVIDDelhi

#UVIKO3
👍1
#COVID19: Denmark imeondoa masharti ya Uvaaji Barakoa kwenye Usafiri wa Umma, Madukani, kwenye Migahawa pamoja na amri ya kuonesha cheti cha Chanjo maeneo ya Burudani na Mapumziko

Maafisa wa Afya wasema idadi ya wagonjwa mahututi imepungua

Soma - https://jamii.app/VizuiziOffDen

#UVIKO3 #Governance
👍1
#COVID19: Kampuni ya #BioNTech pamoja na mshirika wake #Pfizer, wameomba kibali cha dharura Marekani, cha matumizi ya Chanjo ya Corona kwa Watoto chini ya miaka 5

Wakipata Kibali itakuwa Chanjo ya 1 kutumika kwa Watoto kuanzia Miezi sita

Soma - https://jamii.app/BioNtechInfants

#UVIKO3 #JFAfya
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimesema Mawakili 65 wamefariki dunia kwa #COVID19 tangu kutangazwa kisa cha kwanza cha Ugonjwa huo Machi 16, 2020

Serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa chanjo bila malipo

Soma - https://jamii.app/Mawakili65Corona

#UVIKO3
AUSTRALIA KUFUNGUA MIPAKA BAADA YA TAKRIBAN MIAKA MIWILI

Itafungua Mipaka kwa Wasafiri waliopata chanjo dhidi ya #COVID19 ifikapo Februari 21

#Australia ni miongoni mwa Nchi zilizoweka kanuni kali zaidi Mipakani kufuatia Mlipuko huo

Soma - https://jamii.app/MipakaAus

#UVIKO3
ATHARI ZA COVID-19: Huduma za Msingi za Afya zikiwemo programu za Chanjo na matibabu ya magonjwa kama UKIMWI ziliripotiwa kuathiriwa kwa 92% katika Nchi 129

WHO imesema huduma ziliathiriwa kwa kiasi kikubwa, huku kukiwa na maboresho kidogo

Soma https://jamii.app/AthariHudumaAfya

#UVIKO3 #JFAfya