JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FACEBOOK KUACHA KUTUMIA MFUMO WA "FACIAL RECOGNITION"

Itafuta alama za Sura (Faceprint) zaidi ya Bilioni 1 baada ya kutangaza itaachana na mfumo wake wa utambuzi wa Sura

Kumekuwa na shinikizo kutokana na wasiwasi unaozunguka Teknolojia hiyo

Soma https://jamii.app/FBFaceRecognition

#JFTech
UTAJIRI WA KAMPUNI YA APPLE WAZIDI GDP YA AFRIKA

Kampuni ya Apple imefikisha thamani ya Dola trilioni 3 (takriban Tsh. Trilioni 6,920.88) katika Soko la Hisa

Pato la Ndani la Afrika (GDP) ni Dola Trilioni 2.6 sawa na Tsh. Trilioni 5,998.1

Soma - https://jamii.app/AppleUtajiri

#JFTech
MASHIRIKA YA NDEGE YAHOFIA ATHARI ZA 5G KWENYE MAWASILIANO YA NDEGE

Jana, Januari 19, 2022 huduma ya Mtandao wa 5G ilianza kutumika Nchini Marekani kwa kuwashwa Minara 4500 ambayo inadaiwa inaweza kuathiri mawasiliano ya Ndege za #Boeing777

Mashirika makubwa ikiwemo Emirates, Air India, All Nippon Airways, Japan Airlines, Lufthansa na British Airways yamesitisha safari zake

Soma - https://jamii.app/5GVsAirlines

#5GTechnology #JFTech
Wataalamu wanasema Roketi ya Tajiri Elon Musk, #SpaceX iliyorushwa 2015 na kushindwa kurudi Duniani iko kwenye mwendo wa kugonga sehemu ya Mwezi (dark side of the Moon) Machi 4, 2022

Hata hivyo, hakutakuwa na madhara katika tukio hilo la kugongana

Soma - https://jamii.app/MbalamweziRoketi

#JFTech
Mitandao ya Kijamii imetajwa kama moja ya njia kuu ambazo Intaneti huathiri Afya ya Akili

Hii hutokea unapojilinganisha na watu wengine au kuhisi wasiwasi kuhusu kutopata 'Likes' za kutosha ikielezwa vitendo hivi vinaporudiwa mara kwa mara inakuwa uraibu

Unapotumia Mitandao ya Kijamii usiweke nguvu kubwa kufurahisha watumiaji wengine

Soma - https://jamii.app/InternetMentalHealth

#MentalHealth #JFTech
KOREA KASKAZINI YADAIWA KUIBA FEDHA KUPITIA UDUKUZI

Wataalamu wa UN wanasema Fedha hizo zimekuwa zikitumika kufadhili miradi ya Nyuklia na Makombora

Inaelezwa Wadukuzi waliiba zaidi ya Dola milioni 50 Mwaka 2020 mpaka katikati ya 2021

Soma https://jamii.app/UdukuziKZUN

#CyberCrimes #JFTech
Elon Musk ametangaza kuwa atasitisha ununuzi wa #Twitter kwa kuwa kampuni hiyo haikumpa ushirikiano alipohitaji taarifa za Akaunti Feki katika jukwaa hilo

> Aidha, atatakiwa kulipa takriban Tsh. Trilioni 2.3 kwa kuvunja Mkataba

Soma - https://jamii.app/MuskTwitter

#JFTech
😁16👍12
MITANDAO NI DARASA TOSHA, INATUMIKA IPASAVYO?

Wadau ndani ya JamiiForums.com wanasema #Teknolojia ni Mwalimu mzuri, na Ujuzi/Mafunzo mengi yapo Mitandaoni. Hata hivyo, watu wengi hawaitumii ipasavyo kujifunza

Ni kitu gani umefanikiwa kujifunza kupitia Mtandao na unakitumia mara kwa mara?

Soma https://jamii.app/AdvMitandao

#JFDigitali #Technology #JFTech
👍61
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kwa mara ya kwanza, China imeandaa mechi ya Soka inayochezwa na Roboti wa umbo la binadamu (humanoid robots) wanaojiendesha kwa kutumia Akili Unde (#AI), bila msaada wa Binadamu

Mechi hiyo ilifanyika mwishoni mwa mwezi Juni, 2025 katika Chuo Kikuu cha Tsinghua, Beijing, kama maandalizi ya Mshindano ya Dunia ya Roboti (World Humanoid Robot Games) yatakayofanyika Agosti 2025. Roboti hao walitumia AI kutambua mpira, kuchambua mazingira, kufanya maamuzi na kucheza

Licha ya Roboti hao kuangukaanguka na kuwaacha watazamaji 'wakifa mbavu' kwa vicheko, tukio hili linaonesha mafanikio makubwa Kiteknolojia nchini humo na huenda kwa miaka ijayo yakashuhudiwa Mapinduzi makubwa kwenye ulimwengu wa Soka

Fuatilia zaidi https://jamii.app/ChinaRobotiSoka

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFTeknoloji #JFTech #AkiliUnde #AI #Soka #Michezo #JFSports #HumanoidRobots