JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Wadau ndani ya JamiiForums.com wanasema anachohitaji Mtoto zaidi ni Mzazi/Mlezi kuwa karibu naye, ajue kuwa unampenda, unamjali na yuko salama

Mfanye Mtoto akusikilize, si kwa sababu ya hofu bali kwasababu ya Heshima, Uaminifu pamoja na Ukaribu uliopo kati yenu.

Tembelea https://jamii.app/WatotoNyumbani

#JamiiForums #Malezi #Parenting #ChildSafety24 #ChildSafety
1
Watoto wengi wanaofanya vizuri kwenye Elimu ni wale ambao Wazazi/Walezi wamewekeza muda katika kufuatilia Maendeleo ya Watoto wao Shuleni

Ufuatiliaji huo unawezesha kubaini changamoto wanazokumbana nazo na kushirikiana na Walimu pamoja na Watoto wenyewe kuzitatua kwa wakati

Baadhi ya Watoto wamekuwa wakipitia Ukatili na Unyanyasaji kutoka kwa Walimu, Majirani, Wasaidizi wa Kazi za Nyumbani ama Watoto wenzao, kitu kinachochangia kuwa na Maendeleo mabovu Shuleni kwa kukosa sehemu sahihi ya kuwasilisha matatizo yao au Mtu wa kutambua Mabadiliko yao kwa haraka.

Soma https://jamii.app/MudaMalezi

#Accountability #JamiiForums #ChildSafety24 #Parenting #ChildSafety #Malezi
👍31
Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Utumikishaji wa Watoto huadhimishwa kila Mwaka Juni 12

Siku hii ilianzishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuongeza uelewa kuhusu tatizo la utumikishaji wa Watoto na kuhamasisha hatua za kimataifa za kutokomeza aina hiyo ya Ukatili dhidi ya Watoto

Watoto wote wanatakiwa kupata nafasi ya kukua na kujifunza katika Mazingira salama na yenye Afya, bila kulazimika kufanya kazi.

#JamiiForums #ChildSafety #ChildSafety24 #WorldDayAgainstChildLabour #EndChildLabour #StopChildLabour #ChildRights #EducationForAll #ProtectChildren
Ingawa idadi inatofautiana, inakadiriwa katika Barala la Amerika Kaskazini na Ulaya, Mtu 1 kati ya 17,000 hadi 20,000 ana aina fulani ya Ualbino

Katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, inakadiriwa Mtu 1 kati ya 1,400 ameathiriwa Nchini #Tanzania na kiwango kinafikia Mtu 1 kati ya 1,000 Nchini #Zimbabwe

Upungufu wa #Melanin unamaanisha, Watu wenye Ualbino wako katika hatari kubwa ya kupata Saratani ya Ngozi. Katika baadhi ya Nchi, Watu wenye Ualbino hufariki kutokana na Saratani ya Ngozi wakiwa katika umri wa miaka 30 na 40

Soma https://jamii.app/AlbinismAwareness

#JamiiForums #EndDiscrimination #AlbinismAwarenessDay #EmpowerAlbinism #ProtectChildren #ChildSafety24 #ChildSafety
👍3
Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na UNICEF, inaeleza Takriban watoto Milioni 400 wenye chini ya Miaka 5 au 6 Duniani kote, mara kwa mara huvumilia Unyanyasaji wa Kisaikolojia au adhabu za Kimwili Nyumbani (Kupigwa/Kuchapwa)

Wakati Nchi nyingi zikipiga marufuku adhabu ya Kimwili dhidi ya Watoto Nyumbani na Shuleni, Tanzania ni kati ya Nchi zenye Sheria inayoruhusu Viboko Shuleni. Katika zaidi ya Nchi 66 zilizopiga marufuku mila hiyo, takriban 23 zimetunga Sheria ndani ya Miaka 15 iliyopita

Aidha, Ripoti inaonesha Mzazi 1 kati ya 4 Duniani bado anaamini katika Misingi ya Ulezi ya kumchapa Mtoto kama jambo muhimu katika Kulea na kumfunza Mtoto Adabu ipasavyo.

Soma https://jamii.app/AdhabuKikatili

#JamiiForums #ChildSafety24 #ProtectChildren #ChildSafety #ChildRights #Malezi
Kwasababu ya Tabia ya kupenda kujaribu kujifunza kila kitu, Watoto wanaweza kuharibu Mali au Vitu vya thamani Nyumbani pasipo kuelewa Hasara ya uharibifu huo

Je, unatumia njia gani kumfunza Mtoto ili atambue kosa na asirudie tena pale inapotokea ameharibu Kitu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WatotoKuharibuVitu

#JamiiForums #ChildSafety #Malezi #ChildSafety24 #Parenting
👍1
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka ifikapo Juni 16 kuwakumbuka Watoto waliouawa na Serikali ya Kibaguzi huko #Soweto Mwaka 1976 wakiwa katika Maandamano ya kudai Haki zao ikiwemo Haki ya kupata Elimu na kufundishwa kwa kutumia Lugha zao Asilia

Siku hii pia inaangazia Changamoto ambazo Mtoto wa Kiafrika anazipitia ikiwemo Ukosefu wa Elimu, Ukatili wa aina mbalimbali pamoja na uhitaji wa kuboresha Mazingira yake ya Kuishi

Soma https://jamii.app/DAC2024Day

#JamiiForums #ChildProtection #ChildRights #AfricanChild #DAC2024 #ChildSafety24 #ChildSafety #DayOfTheAfricanChild #YearOfEducation
#Education4All
👍21👎1
Mdau wa JamiiForums.com anasema #Malezi ya Watoto yana mambo mengi sana ambayo ili Mzazi/Mlezi aweze kuyamudu kwa kiasi fulani ni lazima ajifunze kwa njia mbalimbali

Anasema #Elimu ya Malezi itapunguza matumizi ya nguvu na kuongeza matumizi ya fikra kwa Wazazi katika Malezi

Ameeleza Wazazi/Walezi wengi hutumia nguvu sana katika kulitekeleza jukumu lao la kulea, ambapo wengi hujikuta katika mkumbo wa 'kuwaburuta' Watoto kwa yale wanayoyataka pasipo kujua

Soma zaidi https://jamii.app/MaleziTaaluma

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ChildSafety #ChildSafety24
👍1
Kuwafuatilia Watoto wako wanachofanya Mtandaoni inahitaji jitihada. Chukua hatua za kuwachunguza wanawasiliana na nani, wanaangalia nini, na wanapakua (download) nini

Pia, ni vizuri kujadili nao mara kwa mara kuhusu Matumizi ya #Intaneti ili kuwalinda na kuwajengea tabia salama Mtandaoni

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #ChildOnlineSafety #ChildSafety24 #ChildSafety
👍2
Moshi wenye Hewa chafu ndani ya Nyumba, utokanao na kupika kwa kutumia Nishati inayochafua Hewa umeripotiwa kusababisha vifo vya Watoto 500,000 kati ya 700,000 hasa Barani Afrika na Asia

Aidha, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Kitty Van Der Heijden anasema licha ya Maendeleo katika #Afya ya Mama na Mtoto, kila siku takribani Watoto 2,000 wenye Umri chini ya Miaka mitano wanafariki kutokana na madhara ya Afya yasababishwayo na uchafuzi wa Hewa

Soma https://jamii.app/DeathAirPollution21

#JamiiForums #PublicHealth #ClimateChange #AirPollution #ClimateCrisis #ChildSafety24 #ChildSafety
👍1💔1