JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: Chama cha #ACTWazalendo kimeitaka Wizara ya Afya kueleza ukweli kuhusu mlipuko wa Ugonjwa wa #Marbug na itangaze hatua za tahadhari kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo Mkoani Kagera, baada ya Wizara hiyo kukanusha taarifa za uwepo wa ugonjwa huo nchini

Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri Kivuli wa Afya wa Chama hicho, Dkt. Elizabeth Benedict Sanga imesema Wizara ya Afya kukanusha uwepo wa Ugonjwa huu bila tahadhari, kunaiweka Tanzania mahali pabaya kimataifa na kunaishushia hadhi yake kubwa iliyojijengea hivi karibuni baada ya kushinda Kiti cha Ukurugenzi Mkuu wa WHO - Kanda ya Afrika, pia kunadhihirisha kuwa Wizara ya Afya haijali usalama wa Wananchi

Aidha, ACT Wazalendo imeitaka Wizara ya Afya itangaze haraka hatua za tahadhari kwa Umma juu ya namna ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kufanya uchunguzi zaidi kwa kila anayeingia na kutoka Mkoani Kagera

Soma https://jamii.app/ACTMarburgTamko

#JamiiForums #Afya #Governance #PublicHealth
😁1