JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akitoa amri kuhusu kesi dhidi ya Tundu Lissu kurushwa moja kwa moja (#LiveStreaming), Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga amesema Mahakama imesitisha matangazo ya moja kwa moja (LIVE), utangazaji, usambazaji wa moja kwa moja au aina nyingine ya uenezaji wa moja kwa moja kwa umma ikijumuisha na mitandao ya kijamii hadi pale itakapotolewa amri nyingineyo.

Soma zaidi https://jamii.app/KuripotiLissuKibaliMahakamani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akitoa amri kuhusu kesi dhidi ya Tundu Lissu kurushwa moja kwa moja (#LiveStreaming), Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga amesema kuchapisha na kusambaza nakala zenye ushahidi au ushahidi wowote utakaoweza kufichua mashaidi wa kiraia kesi ya Lissu inakatazwa na ni marufuku bila idhini ya Mahakama.

Pia ameongeza kwa kusema “Mtu au Vyombo vya Habari vinavyotaka kuchapisha habari kuhusu mwenendo wa kesi ya Lissu “committal proceedings” au mashahidi ni lazima vipeleke maombi mahakamani ili kuonesha kuhariri na kuondolewa kwa utambulisho na Mahakama kuu umekamilika na uchapishaji hautafichua utambulisho wa mashahidi wanaolindwa na Mahakama”

Soma https://jamii.app/VibaliMahakamaKesiLissu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) ya kutaka kutenguliwa kwa uamuzi wa Juni 10, 2025, uliowazuia kuendelea na shughuli za Kisiasa kwa kutumia mali za Chama.

Uamuzi huo mdogo umetolewa leo Agosti 18, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA kuhusu mgawanyo wa rasilimali kati ya Chama hicho Bara na Upande wa Zanazibar.

Wakili wa CHADEMA, Hekima Mwasipu amesema Jaji Mwanga baada ya kukataa maombi yao, pande zote zimekubaliana kuendelea na shauri ambapo Mahakama imeahirisha kesi hadi Agosti 28, 2025 kwa mapitio ya hoja zinazobishaniwa na kupanga utaratibu wa kuendelea na kesi kuu.

Zaidi soma https://jamii.app/OmbiLaChadema

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Tume ya Uchaguzi (ZEC), leo Agosti 18, 2025, imesema kuwa kampeni za Uchaguzi Mkuu zitaanza rasmi Septemba 11, 2025, Saa 10:01 Jioni mara baada ya uteuzi wa Wagombea na zitaendelea hadi siku ya mwisho kabla ya upigaji kura Oktoba 29, 2025.

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Goerge Joseph Kazi amesema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za Wagombea wa Urais, Baraza la Wawakilishi na Udiwani utafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 10, 2025 Saa 10:00 Jioni, na uteuzi rasmi kufanyika Septemba 11, 2025 Saa 10:00 Jioni kabla ya kuanza kwa kampeni.

Zaidi soma https://jamii.app/UchaguziZbar

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Democracy #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, jana 18 Agosti 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi ameeleza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, unafanyika katika mazingira bora zaidi Kisheria tangu uhuru.

Ameongeza kuwa Mwaka 2024 Bunge lilitunga Sheria mbili muhimu ambazo ni Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ambazo zimekuja na mabadiliko makubwa.

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Alliance for Africa Farmers Party (#AAFP), Said Soud Said amesema alijaribu kuandaa utaratibu wa Vyama vya Upinzani kuungana ili kuiondoa #CCM madarakani, lakini juhudi hizo zimegonga mwamba baada ya Vyama hivyo kutambua maendeleo yaliyofanywa na Chama hicho. Amesema hayo Agosti 15, 2025.

Zaidi soma https://jamii.app/SaidVyamaKuungana

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
DODOMA: Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (#CCM) dhidi ya Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa, ambaye anapinga uhalali wa mchakato uliompitisha Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwania urais kupitia Chama hicho.

Mawakili wa CCM, Fabian Donates na Alex Mgongolwa, leo Agosti 19,2025 wamewasilisha mapingamizi wakidai hatua za kufungua shauri hilo hazikufuatwa, huku wakisisitiza mlalamikaji alipaswa kuandika barua kwa Katibu Mkuu badala ya mwenyekiti wa Chama.

Aidha, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo, amesema taratibu zilizingatiwa kwani Februari, 2025, Dkt. Malisa alimwandikia barua Rais Samia akilalamikia uteuzi wake, ambapo baada ya hoja za pande zote kusikilizwa, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 22, 2025.

Soma https://jamii.app/MalisaNaCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Akizungumza Agosti 18, 2025, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema "Uchaguzi wetu kila baada ya Miaka mitano ni jambo muhimu sana kwa Taifa letu, ndiyo kielelezo cha #Demokrasia ya #Tanzania. Nchi hii haijawahi kuahirisha uchaguzi hata mara moja na katika mazingira magumu kuliko sasa. Wanaotaka Uchaguzi uahirishwe hawaelewi historia ya nchi hii."

Zaidi soma https://jamii.app/KabudiUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Demokrasia #UchaguziMkuu2025 #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo Agosti 20, 2025 kwa njia ya Mtandao, Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema miongoni mwa mabadiliko yanayohitajika ni kuwepo na utaratibu wa kupinga matokeo ya Urais Mahakamani iwapo kutatokea mashaka kwenye ushindi huo.

Zaidi soma https://jamii.app/SuguMatokeoUrais

#JamiiForums #JamiiAfrica #Demokrasia #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Governance