JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com amelalamikia hali ya Vitambulisho vya #NIDA kufutika Maandishi kwa kipindi cha muda mfupi, huku akidai ukienda kwa Mamlaka husika kutoa taarifa unaambiwa ujaze fomu upya na kuleta 'loss report' halafu ulipie Tsh. 20,000 ili upewe Kitambulisho kingine

Vipi Mdau, umeshakutana na hali hii ya Kitambulisho cha NIDA kufutika Maandishi muda mfupi baada ya kukipata?

Soma https://jamii.app/NIDAKufutika

#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji
UTEUZI: Rais Samia amemteua Gilead John Teri kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority - TISEZA) leo Julai 1, 2025

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusilika, Teri ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji na Maeneo maalum ya mwaka 2025

Aidha, Sheria hiyo imeunganisha majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na iliyokuwa Mamlaka ya Maneno maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA)

Zaidi Bofya https://jamii.app/UteuziGileadTeri

#JamiiAfrica #Utawala #JamiiForums #Uteuzi
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, imeahirishwa hadi Julai 15, 2025 ikiwa bado inasubiri hatua atayoichukua DPP akimaliza kupitia faili, ambalo imeelezwa na Mawakili wa Jamhuri kuwa bado lipo mezani kwake

Akizungumza kabla ya maamuzi hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu aliiomba Mahakama iwaamuru Mawakili wa Jamhuri kueleza hatua ya uchunguzi ilipofikia, kwa kuwa hadi kufikia Wiki inayofuata atakuwa amekaa gerezani kwa Siku 90

Soma https://jamii.app/LissuJulai1

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights
Mdau, wewe ni Mzazi/Mlezi anayeamini katika Mfumo upi wa Malezi?

1. Kumchapa Mtoto humfanya awe na Nidhamu
2. Kumchapa Mtoto huweza kumfanya awe mkaidi zaidi
3. Mtoto anapaswa kulelewa pasipo kuchapwa

Mjadala zaidi https://jamii.app/MaleziKumchapaMtoto

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFStories #JFChitChats #Malezi
Mdau wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com ameomba ushauri wa hatua za kuchukua kutokana na kuchukiwa na Watu bila sababu kiasi kwamba hali hiyo imeanza kuathiri Maisha yake ya kawaida

Unamshauri nini Mdau?

Mjadala zaidi https://jamii.app/NachukiwaBilaSababu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Lifestyle #Maisha
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutajwa kwa shauri la kesi ya uhaini, Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, amesema akifanikiwa kutoka atarejea Barabarani na kuendelea na mchakamchaka ambao hakuufafanua zaidi

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 15, 2025.

Soma https://jamii.app/LissuMahakamaniJulai1

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights
2
KAGERA: Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Karagwe, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Julai 1, 2025

Bashungwa ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa Vipindi Viwili kuanzia Mwaka 2015, aliwasili katika Ofisi hiyo akiwa katika gari ndogo aina ya Toyota Carina na kuchukua fomu kisha kurejesha kwa Katibu wa CCM Karagwe, Anatory Nshange ambapo pia aliondoka akiwa katika usafiri huo

Soma https://jamii.app/BashungwaFomu

#Siasa #Democracy #Kuelekea2025 @UchaguziMkuu2025
1
DAR: Baadhi ya Wakazi wanaoishi karibu na eneo linalodaiwa kujengwa Kanisa la Arise and Shine (Kawe), linaloongozwa na Boniface Mwamposa wamedai ujenzi huo umekuwa kikwazo kwa baadhi ya huduma ikiwemo Barabara kufungwa na maji kukatika

Wakizungumza leo Julai 1, 2025 Asubuhi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule hali hiyo inatokana na uharibifu wa miundombinu unaodaiwa kufanywa na Wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi.

Baada ya kusikia malalamiko hayo, DC Mtambule aliamuru kusitishwa kwa ujenzi huo kwa muda, ili kutoa nafasi ya kufanya tathmini ya kina

Soma https://jamii.app/UjenziKanisa

#JamiiForums #Accountability #JFMatukio #Governance