JamiiForums
55.9K subscribers
33.1K photos
1.93K videos
30.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MICHEZO: Nyota wa Soka kutoka Ureno, #CristianoRonaldo, ameweka rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza Duniani kufikisha Magoli 900 katika maisha yake ya Soka, rekodi ambayo ni kwa mujibu wa Tovuti ya Transfermarkt

Akiichezea Ureno katika mchezo dhidi ya Croatia, Ronaldo amefunga Goli hilo katika dakika ya 34 baada ya Diogo Dalot kufunga goli la utangulizi, ingawa baadaye (Dalot) alijifunga na kusababisha mchezo kumalizika kwa Magoli 2-1

Kufuatia ushindi huo dhidi ya Croatia, Ureno ilifungana pointi na Poland inayoongoza Kundi A1 ambayo iliichapa Scotland mabao 3-2 katika Mchezo wa UEFA Nations League

Soma https://jamii.app/Ronaldo900

#JamiiForums #JFSports #UEFANationsLeague
MBEYA: Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 kujeruhiwa baada ya Basi la Abiria la A-N Coach (T282 CXT) lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora, kupinduka wakati likikwepa Lori na kuingia mtaroni

Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Septemba 6, 2024

Aidha, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Darson Andrew amethibitisha idadi ya vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44, wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Soma https://jamii.app/11WafarikiMbeya

#JFMatukio #JamiiForums
Usiposambaza taarifa, picha au video za 'utupu', za faragha au zenye maudhui ya dhihaka au unyanyasaji unasaidia kukomesha Ukatili Mtandaoni

Kila Mtu anastahili usalama, faragha na Utu Mtandaoni. Tunapowaonea huruma na kuwastahi Watu wetu wa karibu, tunapaswa kuwastahi na ambao hatuwajui

Kumbuka, chaguo la kutosambaza linaweza kuwa msaada mkubwa kwa Waathirika na Watumiaji wengine wa Majukwaa ya Mtandaoni, hivyo kuwa na Majukwaa salama ambapo kila Mtu atashiriki kwa Uhuru.

Soma https://jamii.app/UkatiliKwaWanawakeMtandaoni

#JamiiForums #EndGBV #LindaFaragha #PingaUkatiliMtandaoni #UkatiliMtandaoni #OnlineSafety #DigitalRights #JFWomen
SHERIA: Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kupitia Mawakili wake ametoa Siku 5 kwa Mchungaji Peter Msigwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, kumuomba radhi hadharani na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu

Msigwa anadaiwa kutoa kauli za kumdhalilisha Mbowe hadharani, baada ya kuhamia CCM, akidai Mbowe anatumia Chama (CHADEMA) kwa manufaa binafsi na kwamba ameanzisha taasisi inayoitwa "Mbowe Foundation" kwa maslahi yake

Aidha, Msigwa alidai CHADEMA Digital, huduma ya usajili wa Wanachama zinamilikiwa na Kampuni binafsi ambayo inaendeleza maslahi binafsi ya Mbowe

Mawakili wamedai kauli za Msigwa zimeathiri 'Brand' yake, sifa yake Kitaifa na Kimataifa, hasa kutokana na nafasi zake za uongozi, hivyo Msigwa asipoomba radhi na kulipa Tsh. Bilioni 5 atafunguliwa kesi Mahakamani.

Soma https://jamii.app/MboweVsMsigwa

#JamiiForums #Governance #Democracy
JE, ULISHIRIKI SHINDANO LA 'STORIES OF CHANGE' 2024? USIKAE MBALI NA PM YAKO

Siku ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Shindano la #StoriesOfChange2024 ni Septemba 21, 2024, ambapo washiriki walioandika Andiko Bora kuhusu #TanzaniaTuitakayo kwa Miaka 5-25 ijayo watatangazwa

Sasa, kama ulishiriki Shindano hili tafadhalli hakikisha unapitia na kusoma Jumbe kupitia 'Private Message' (PM) ya akaunti yako ya JamiiForums.com

JamiiForums itawasiliana na Wanaoelekea kuwa Washindi kupitia PM kama ilivyoelekezwa kwenye Vigezo na Masharti ya Shindano hili

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
UGANDA: Rais Yoweri Museveni amesisitiza kuwa Serikali haiwezi kuruhusu utaratibu wa Dhamana kwa Watu wanaotuhumiwa kuhusika na #Ufisadi, #Rushwa na Kesi za Mauaji

Akizungumza katika Mkutano wa kila Mwaka kati ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP) na Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai, Museveni amesema njia pekee inayoweza kutumika ni upande wa mashtaka kuharakisha Kesi ili kila upande upate Haki yake

Aidha, Rais Museveni, ameongeza kuwa si Haki kuona mtu anayetuhumiwa kwa mauaji akizurura kwa uhuru katika jamii baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya Polisi, kauli ambayo imepingwa na baadhi ya Wadau wa Sheria

Soma https://jamii.app/UgandaBail

#JamiiForums #Governance #HumanRights #Accountability
DODOMA: Akijibu hoja iliyotolewa na Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuwa wanazungushwa na baadhi ya Maafisa wa Serikali au mamlaka zinazosimamia Mashirikia hayo, Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko amesema Maafisa wanaohusika wanatakiwa kutoa majibu haraka kwa wale wanaohitaji ufafanuzi au huduma na sio kuwazungusha

Akizungumza katika mkutano wa Mwaka wa NGOs 2024, Biteko amesema “Kama jibu ni Hapana mwambie Hapana, ukimwambia utampunguzia muda wa kuzunguka, kuliko kumwambia njoo kesho, ukifanya hivyo unatengeneza njia ya Rushwa.”

Ameongeza “Nasema hivyo kwa kuwa kila mwaka wanapoita mgeni rasmi, NGOs zinakuwa na maelezo yakeyale, maana yake wamekuja Dodoma kupiga picha? Lazima wapate majibu ya maswali na hoja zao, hilo siyo jambo la hisani, ni haki yao.”

Soma https://jamii.app/ANGOF2024Day3

#JFMatukio #Governance #ANGOsForum2024 #ANGOF2024 #JamiiForums
DODOMA: Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko, mesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yana umuhimu mkubwa na yamekuwa yakisaidia majukumu ya Serikali ikiwemo kutoa zaidi ya ajira 21,000 ambazo bila hivyo ingekuwa ni jukumu la Serikali kuwahudumia

Ameeleza kuwa Jumla ya Tsh. Trilioni 2.6 zimetumika na kuzunguka Nchi nzima katika michakato ya Mashirika hayo, hali ambayo inamaanisha kuna Watu wengi wamenufaika kutokana na uwepo wa NGO's

Ameongeza “Serikali haiwezi na haina mpango wa kusigana na NGO's bali ina mpango wake kusaidia mtimize majukumu yenu.”

Soma https://jamii.app/ANGOF2024Day3

#JFMatukio #Governance #ANGOsForum2024 #ANGOF2024 #JamiiForums
DODOMA: Wakazi wa mtaa wa Muungano jijini Dodoma, Mwamvita Mwakibasi (33) na binti yake Salma Ramadhan (13) wameuawa usiku wa kuamkia Septemba 6, 2024 baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili na watu ambao hawajafahamika

Dada wa marehemu, Pendo Mwakibasi amesema alipigiwa simu na mama yao mzazi kutoka Mbeya saa 8:00 usiku akiambiwa mdogo wake amevamiwa nyumbani kwake, alipofika aliwakuta katika hali mbaya wakitokwa Damu na hawawezi kuzungumza

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Dodoma, Daniel Dendarugaho, akizungumzia tukio hilo, ameomba wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Soma https://jamii.app/MamaMwanaWauwawa

#JamiiForums #JFMatukio
MBEYA: Jeshi la Polisi limesema ajali iliyotokea leo Septemba 6, 2024 na kuua Watu 12, ilisababishwa na uzembe wa Dereva, Hamduni Nassoro Salum aliyeshindwa kulimudu Gari kwenye mteremko na kona kali

Taarifa ya Polisi, imesema katika ajali hiyo watu 12 walipoteza maisha kati yao wanaume ni watano akiwemo dereva wa Basi na wanawake 7 wakiwemo watoto wadogo wawili

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa watu 33 ni majeruhi ambapo 22 ni wanaume na 11 ni wanawake wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Hospitali ya Wilaya ya Chunya na Kituo cha Afya Chalangwa kilichopo Wilaya ya Chunya.

Soma https://jamii.app/UzembeDerevaAjaliMbeya

#JamiiForums #JFMatukio
DODOMA: Francisca Mboya kutoka Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) anasema kuna Wafanyakazi wengi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wanatumia Akili Mnemba (AI) lakini hawataki kuonekana wanatumia wakati si kitu cha kujificha wala kuona aibu kwakuwa Dunia ndio ilipo kwa sasa

Amesema “Ukiuliza Mtu mmojammoja kwenye Shirika kuhusu utumiaji wa AI watakwambia hawatumii, ukifanya uchunguzi kiuhalisia wanatumia lakini hawataki kuonekana wanatumia. Matumizi ya Teknolojia ni muhimu yanapunguza gharama, pia inarahisisha uchakataji wa taarifa"

Pia amesema, “Tusione aibu, tutumie AI inasaidia na inarahisisha utendaji kazi, mfano matumizi ya Lugha ya Kingereza kwakuwa hiyo kwetu ni Lugha ya pili, unaweza kutumia kurahisisha na kunyoosha maandiko.”

Soma https://jamii.app/ANGOF2024Day3

#JFMatukio #Governance #ANGOsForum2024 #ANGOF2024 #JamiiForums
Kuwa sehemu ya Mabadiliko. Chagua kutosambaza taarifa, video au picha zinazolenga Kudhalilisha, Kunyanyasa au Kutweza utu.

#JamiiForums #EndGBV #LindaFaragha #PingaUkatiliMtandaoni #UkatiliMtandaoni #OnlineSafety #DigitalRights #JFWomen
JE, ULISHIRIKI SHINDANO LA 'STORIES OF CHANGE' 2024? USIKAE MBALI NA PM YAKO

Siku ya kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Shindano la #StoriesOfChange2024 ni Septemba 21, 2024, ambapo washiriki walioandika Andiko Bora kuhusu #TanzaniaTuitakayo kwa Miaka 5-25 ijayo watatangazwa

Sasa, kama ulishiriki Shindano hili tafadhalli hakikisha unapitia na kusoma Jumbe kupitia 'Private Message' (PM) ya akaunti yako ya JamiiForums.com

JamiiForums itawasiliana na Wanaoelekea kuwa Washindi kupitia PM kama ilivyoelekezwa kwenye Vigezo na Masharti ya Shindano hili

#JamiiForums #SoC2024 #StoriesOfChange #Accountability #Governance #TanzaniaTuitakayo #SoCS4
Mdau wa JamiiForums.com anashauri watu kuwa na utulivu wa akili inapotokea wamepata changamoto ili kupata namna nzuri ya kuzitatua bila 'papara' na watafikiri kabla ya kuamua

Amesema mtu anaweza kuwa anahitaji msaada lakini anapokosa utulivu wa fikra ni rahisi kujikuta mikononi mwa 'Wapigaji'

Je, unakubaliana na hoja ya Mdau?

Mjadala https://jamii.app/MatatizoNaFursa

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle #JFChitchats
MOROGORO: Mdau amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwasaidia Wastaafu wa Kiwanda cha Maturubai Morogoro (Morogoro Canvas Mill) ambao anadai wamekuwa wakizungushwa na Ofisi ya Msajili, kulipwa stahiki zao ikiwemo mishahara kabla ya kuondolewa kazini pamoja na fidia ya kuondolewa katika ajira

Anadai wameandika barua kwenda kwa Waziri Mkuu kuomba msaada wa kupata madai yao yaliyohakikiwa na Kamati ya Uhakiki wa Madeni ya Mashirika ya Umma Yaliyobinafishwa iliyowajulisha Julai 2020 kuwa madai yao yamepitishwa na Bunge

Pia anaeleza kuwa, baadaye Mtendaji mmoja wa Hazina aliwajulisha malipo yao ni Tsh. Milioni 36 badala ya Tsh. Bilioni 123.4 wanayodai jambo ambalo hawakubaliani nalo

Soma https://jamii.app/MadauCANVAS

#CivilRights #Accountability #JamiiForums