JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AL-SHABAAB YATISHIA KUSHAMBULIA KENYA

Wapiganaji hao wametuma ujumbe wa kuishambulia #Kenya kama kisasi cha uwepo wa Majeshi yake Nchini Somalia

Watu 13 wameuawa tangu kuanza mwaka 2022. Vifo vimehusishwa na wapiganaji wa Al-Shabaab

Soma - https://jamii.app/KenyaAlShabaab
UGANDA KUHARIBU DOZI ZAIDI 400,000 ZILIZOISHA MUDA

Kasi ndogo ya utoaji Chanjo dhidi ya #COVID19 imesababisha Chanjo za Moderna na #AstraZeneca kuisha muda wa matumizi

Dozi 12,220,106 zimetolewa hadi sasa. Uganda imerekodi Vifo 3,378

Soma - https://jamii.app/DoziLakiNne

#UVIKO3 #JFAfya
AUSTRALIA YAFUTA VISA YA NOVAK DJOKOVIC KWA KUTOCHOMA CHANJO YA #COVID19

Waziri wa masuala ya Uhamiaji amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuzingatia Sheria ya Afya

Djokovic bado anaweza kufungua kesi nyingine kupinga kufukuzwa Nchini humo

Soma https://jamii.app/DjokovicVisaBan
#UVIKO3
MALEZI: NAMNA YA KUMSAIDIA MTOTO KUWA MTU BORA KWENYE JAMII

1. Mfundishe kufanya kazi kwa Ushirikiano (Teamwork). Mfano unaweza kutenga muda kusaidiana naye kwenye 'Homework' au majukumu ya Nyumbani

2. Shiriki au Mfundishe kupanga malengo pamoja na maono mliyonayo. Washirikishe Watoto kwenye uwekaji wa Sheria/Miongozo itakayowasaidia kitabia

Soma - https://jamii.app/MtotoBora
#Malezi
UGANDA: WANAFUNZI MILIONI 4.5 HAWATARUDI SHULE

Ripoti ya Mamlaka ya Mipango ya Taifa imeonesha Wanafunzi hao hawataweza kurudi Shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo Ujauzito

Uganda imefungua Shule hivi karibuni baada ya kuzifunga kwa takriban miaka 2

Soma https://jamii.app/MilioniWanafunzi

#JFElimu
WHO YAPENDEKEZA DAWA MBILI KUTUMIKA KUTIBU #COVID19

Baricitinib imependekezwa kutumika kutibu wagonjwa mahututi wa #COVID19 na Sotrovimab kutumika kwa Corona isiyo kali

Dawa zimependekezwa baada ya majaribio saba yaliyohusisha watu 4,000

Soma - https://jamii.app/DawaCorona

#UVIKO3 #JFAfya
WATOA HUDUMA ZA 'MASSAGE' WATAKIWA KUJISAJILI KABLA YA MACHI 31, 2022

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema huduma ya 'Massage' ni tiba asili hivyo watoa huduma wanatakiwa kupata Mafunzo Maalum na Leseni ya kutoa huduma hiyo

Soma https://jamii.app/MassageService
#JFAfya
12.7% YA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2021 WAPATA SIFURI

NECTA imetangaza matokeo ya Kidato cha Nne. Wanafunzi 652,611 walifanya mitihani na 422,388 wamefaulu kwa kupata Daraja la Kwanza hadi Daraja la Nne sawa na 87.3%

> 19.24% wamefaulu Hisabati

Soma https://jamii.app/CSEE2021

#JFElimu
MATOKEO KIDATO CHA 4: WANAFUNZI WAONESHA UMWAMBA KWENYE KISWAHILI NA KEMIA

Katika wanafunzi waliofaulu mtihani wa kidato cha nne 2021, waliofaulu Kiswahili ni 95.58% na Kemia 92.02%

> Hisabati imeendelea kuwaburuza, waliofaulu Hisabati ni 19.24%

Soma https://jamii.app/CSEE2021

#JFElimu
WASICHANA WANG’ARA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2021

Nafasi ya Kwanza hadi ya Saba zimeshilikiliwa na Wasichana, ya Nane na Tisa zimeshikiliwa na Wavulana

Nafasi ya Kumi pia imefungwa na Msichana

Soma - https://jamii.app/CSEE2021

#JFElimu
UN: WATU TAKRIBAN 108 WAMEUAWA TANGU JANUARI MOSI 2022 NCHINI #ETHIOPIA

Raia hao wameuawa ktk mashambulizi ya anga kwenye Jimbo la #Tigray

Mashambulizi yalifanyika dhidi ya Basi dogo, Uwanja wa Ndege na kambi ya Watu wasio na makazi

Soma - https://jamii.app/DeathTigrayJAN

#HumanRights
SHULE MOJA YA SERIKALI YAINGIA KUMI BORA

Mzumbe Sekondari iliyopo Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro imekuwa Shule pekee ya Serikali iliyoingia kumi bora

Imeshika nafasi ya kumi huku nafasi tisa za awali zikishikwa na Shule binafsi

Soma - https://jamii.app/CSEE2021

#JFElimu
UTAFITI: 2021 UMESHIKA NAFASI YA 6 KWA MIAKA YENYE JOTO ZAIDI

Ni kwa Takwimu za Shirika la Utafiti wa Anga za Mbali (NASA) na Idara ya Bahari na Anga(NOAA)

Wastani wa Joto ulikuwa nyuzi joto 1.51 za kipimo cha Celsius juu ya viwango vya karne ya 20

Soma https://jamii.app/2021JotoNo6
DAR: SOKO LA KARUME LATEKETEA KWA MOTO

Soko la Karume lililopo Wilayani Ilala Dar es Salaam limeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika

> Taarifa zaidi kukujia

Soma - https://jamii.app/KarumeMoto

#JFMatukio
Polisi Nchini #Haiti imesema Seneta wa zamani, John Joel Joseph ambaye ni mshukiwa mkuu ktk mauaji ya aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo ametiwa mbaroni Nchini #Jamaica

Rais Moise alivamiwa Nyumbani kwake Julai 7, 2020 na kuuawa kwa kupigwa risasi

Soma - https://jamii.app/JosephHaitiArr

#Accountability
TANGA: TRENI YA ABIRIA YAPATA AJALI, MTOTO AFARIKI

Treni iliyokuwa inatoka Arusha kuelekea Dar ikiwa na abiria 700 imepata ajali alfajiri ya leo, Januari 16 Wilayani Pangani

Mabehewa 5 yamepinduka, 4 yameacha njia na kusababisha majeruhi 5

Soma - https://jamii.app/AjaliTRC

#JFMatukio
AUSTRALIA: Mahakama ya Shirikisho la #Australia imeikataa rufaa iliyoletwa na Bingwa wa Tennis Duniani, Novak Djokovic akipinga kufutwa kwa 'visa' yake na kufukuzwa kwa kutochoma Chanjo

Michuano ya #Tennis ya Australian Open inaanza leo, Januri 17 ambapo alikuwa amenuia kutafuta taji la 21 la Grand Slam

Soma - https://jamii.app/DjokovicNoRufaa

#JFSports
RIPOTI: MATAJIRI WATAJIRIKA ZAIDI WAKATI WA COVID-19

Shirika la Oxfam lasema utajiri wa Mabilionea 10 wakubwa zaidi umeongezeka maradufu wakati wa #CoronaVirus

Mapato ya chini ya Mataifa masikini zaidi yalichangia vifo vya watu 21,000 kila siku

Soma - https://jamii.app/OxfamReport

#JFMatukio