JamiiForums
56.2K subscribers
32.8K photos
1.85K videos
30K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
ASKARI ALIYEKATAA RUSHWA YA TSH. MILIONI 10 ASHUSHWA CHEO

Askari Meshack Samson aliyepandishwa kutoka Sajenti kuwa Stesheni Sajenti mwaka 2019 ameshushwa cheo kwa utovu wa nidhamu

Polisi yasema alikataa kusoma kozi ya kuendana na cheo kipya

Soma - https://jamii.app/UtovuNidhamu
NDEGE KUTOKA TANZANIA KUTORUHUSIWA UAE KUANZIA DESEMBA 25

Mamlaka ya Udhibiti wa Majanga ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imechukua hatua hiyo kufuatia ongezeko la Visa vya #Omicron

Nchi nyingine zilizozuiwa ni Kenya, Ethiopia na Nigeria

Soma - https://jamii.app/NdegeTzUAE

#UVIKO3
KOREA KUSINI: RAIS ALIYEFUNGWA KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA ASAMEHEWA

Rais Moon Jae-in amemsamehe Rais wa zamani Park Geun-hye aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 22

> Park alifungwa mwaka 2018 kwa matumizi mabaya ya madaraka na rushwa

Soma https://jamii.app/RaisMsamaha
RWANDA: UHURU WA KUJIELEZA NA KUTOA MAONI NI TATIZO

Ripoti ya Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu inasema Sheria ya Vyombo vya Habari inakataza vifaa vya Mwandishi kukamatwa, huku Sheria ya Idara ya Taifa ya Upelelezi ikimpa mpelelezi haki ya kukamata kila kitu

Soma - https://jamii.app/FreeSpeechRWD
#FreeSpeech
AFYA: MUDA WA MAMA ALIYEJIFUNGUA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Baada ya kujifungua, Wanawake wengi hupoteza hamu ya Tendo la Ndoa kutokana na Mabadiliko ya Hisia. Kitaalamu Mama hushauriwa kusubiri mpaka wiki sita ndio aweze kushiriki Tendo

Mama aliyejifungua kwa njia ya upasuaji anapaswa kusubiri kwa muda mrefu na pia azingatie kufanya kwa utaratibu na kuepuka staili zinazoumiza mshono

Soma - https://jamii.app/TendoNdoaMzazi
#Afya
ZANZIBAR: ELIMU YA MSINGI KUISHIA DARASA LA 7 KUANZIA MWAKA 2022

Ilibainika kuishia Darasa la 6 hufanya Wanafunzi waingie Sekondari wakiwa wadogo na kufeli

Waziri wa Elimu, Simai Mohammed Said asema mabadiliko hayo yamefanywa ili kuimarisha Elimu

Soma - https://jamii.app/STD7Znz
KENYA: WASIOPATA CHANJO YA COVID-19 KUTORUHUSIWA KUINGIA BAA

Jumuiya ya Wamiliki wa Baa, Hoteli na Maduka ya Vileo (BAHLITA) imekubali kutotoa huduma kwa wasiochanjwa

Pia, uthibitisho wa Chanjo utahitajika ktk usafiri na huduma za kijamii

Soma https://jamii.app/ChanjoKE

#UVIKO3
Tunakutakia Sikukuu Njema ya Krismasi

> Iwe siku ya furaha na baraka tele kwako na familia yako

#christmas2021
URUSI: GOOGLE YAPIGWA FAINI YA TSH. BILIONI 225.7

Kampuni ya #Google inatuhumiwa kushindwa kuondoa maudhui ambayo Urusi inasema yanaenda kinyume na Sheria

> Kampuni za Meta na #Twitter pia zimewahi kupigwa faini kwa kosa kama hilo

Soma https://jamii.app/FainiGoogleUrusi

#DigitalRights
ZANZIBAR: WATU 89 WAKUTWA NA MAAMBUKIZI YA COVID-19

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Dkt. Marijani Msafiri amesema 38 kati yao ni Watumishi wa Afya na hawajalazwa kwani hawana dalili hatarishi

> Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari

Soma https://jamii.app/COVID19Znz
#UVIKO3
LIBYA: WAGOMBEA UBUNGE WAITISHA MAANDAMANO KUPINGA KUFUTWA KWA UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi imependekeza Uchaguzi wa Rais sasa ufanyike Januari 24, 2022 lakini hakuna tarehe rasmi iliyopangwa au kukubaliwa na pande hasimu Nchini humo

Soma - https://jamii.app/ProtestLibyaMP
#LibyaElection
Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya amesema Wasafiri wote wanaoishia Nchi za Marekani, UAE, baadhi ya Nchi za Ulaya na India watatakiwa kufanyiwa kipimo cha haraka cha #COVID19 kabla ya kuondoka

Aidha, Wasafiri wote wanaunganisha Ndege kupitia #Tanzania wanapaswa kufanya kipimo cha haraka Uwanjani ndani ya Saa 6 kabla ya kusafiri

Soma - https://jamii.app/CovidTestTrav
#UVIKO3
TANZANIA YAPOKEA DOZI 376,320 ZA CHANJO YA MODERNA

Hii ni Awamu ya Kwanza kwa aina hii ya Chanjo kuingia Nchini. Dozi hizo zitatumika kuchanja Watu 188,160

Hadi sasa Tanzania imepokea Dozi 6,408,950 zikijumuisha #Sinopharm, J&J na #Pfizer

Soma - https://jamii.app/ModernaTZ
#UVIKO3
ALIYEKUWA ASKOFU MKUU WA TAG AFARIKI DUNIA

Askofu Prof. Ranwell Mwenisongole alikuwa Mchungaji Kiongozi wa City Christian Center (CCC) Upanga na Askofu Mkuu Awamu ya Pili

Alikuwa akisumbuliwa na Maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu

Soma - https://jamii.app/RIPMwenisongole
TANZIA: ASKOFU DESMOND TUTU AFARIKI DUNIA

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Askofu Desmond Tutu ambaye alishiriki kupambana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90

> Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa

Soma https://jamii.app/DesmondTutu
JAJI WEREMA: NCHI IMEPITIA WAKATI MGUMU MIAKA 5 ILIYOPITA

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Awamu ya Nne, Jaji Frederick Werema amesema Rais kuwa na madaraka makubwa bila kuhojiwa ni hoja ya wanaodai #Katiba Mpya tangu mwaka 1992

Soma - https://jamii.app/JajiWerema

#JFSiasa
WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AKUTWA NA #COVID19

Waziri Nassor Ahmed Mazrui amethibitishwa kuwa na Virusi vya Corona. Ana dalili za wazi ikiwemo homa kali na maumivu ya viungo

Wananchi wahimizwa kuchukua tahadhari na kupata Chanjo ili kujikinga

Soma https://jamii.app/WaziriWaAfya

#UVIKO3
RAIS WA ZAMANI WA UGIRIKI, KAROLOS PAPOULIAS AFARIKI DUNIA

Rais Karolos Papoulias aliyeongoza Ugiriki 2005 hadi 2015 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92

Pia alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 1985 hadi 1989, na 1993 hadi 1996

Soma - https://jamii.app/RaisUgiriki

#JFLeo
AFGHANISTAN: WANAWAKE WATAKIWA KUSINDIKIZWA KATIKA SAFARI NDEFU

Taliban imesema Wanawake wanaotaka kusafiri zaidi ya KM 72 wasipewe usafiri isipokuwa wakiwa na ndugu wa kiume wa karibu

Wamiliki magari wahimizwa kutopandisha Wanawake wasiovaa Hijabu

Soma https://jamii.app/SafariWanawake
UFARANSA: WATU 104,611 WAKUTWA NA COVID-19 NDANI YA SAA 24

Idadi hiyo haijawahi kufikiwa Nchini humo tangu kuingia kwa janga la Corona

Idadi ya waliolazwa vitengo vya uangalizi maalum imepanda kutoka Wagonjwa 28 na kufikia Watu 3,282

Soma - https://jamii.app/CoronaSpikeFrance

#UVIKO3