JamiiForums
56.4K subscribers
32.7K photos
1.81K videos
29.9K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
MANYARA: MAMA AMJERUHI MTOTO KWA KUOMBA PESA KWA MPITA NJIA

Jeshi la Polisi linamshikilia Janeth Doto Vicent kwa kumjeruhi Mtoto wake (3) kwa kutumia kitu chenye ncha kali

Mama alichukizwa na kitendo cha Mtoto kuomba fedha kwa mpita njia

Soma https://jamii.app/UkatiliMtotoHela

#UkatiliWatoto
FAHAMU MAZINGIRA BORA KWA MKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA KUFANYA KAZI

Mkalimani na Kiziwi wanatakiwa kuwa kwenye eneo lenye uwazi na mwanga ili Alama za Mawasiliano ziweze kuonekana na kutafsiriwa kwa usahihi

Mkalimani lazima awe mbobezi kwa kundi au Jamii anayoitafsiria kwa kufahamu Lugha na utamaduni wao

Mkalimani anatakiwa kuwa na ujuzi wa mambo mengi katika nyanja mbalimbali ili aweze kuendana na muktadha

Soma - https://jamii.app/UkalimaniAlama
UN: HALI YA SYRIA SIO SALAMA KWA WAKIMBIZI KURUDI

Wachunguzi wameorodhesha matukio ya vurugu mbaya na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya Wanajeshi wa Serikali ya #Syria, ikiwemo Watu kufungwa bila hatia

Soma - https://jamii.app/UsalamaSyria
#HumanRightsViolations
WATOTO WAPEWE TAARIFA SAHIHI KUHUSU CHANJO YA #COVID19

UNICEF inasema watu wazima wawe na taarifa sahihi kabla ya kuzungumzia chanjo ya Virusi vya Corona kwa Watoto

Pia inashauriwa kuwasikiliza Watoto na kuzingatia hofu zao

Soma - https://jamii.app/WatotoTaarifa

#JamiiForums #UVIKO3
HAITI: WAZIRI MKUU AZUIWA KUTOKA NJE YA NCHI

Ariel Henry amepigwa marufuku kuondoka Nchini humo kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusu kuhusika kwake katika mauaji ya Rais Jovenel Moïse

Ametakiwa kuelezea uhusiano wake na mtuhumiwa muhimu

Soma - https://jamii.app/PMBanHaiti
#HAITI: WAZIRI MKUU AMTIMUA MWENDESHA MASHTAKA KWA KUMSHUKU KUHUSIKA NA KIFO CHA RAIS

Ariel Henry amemfuta kazi Bed-Ford Claude aliyesema, rekodi za simu zinaonesha aliyepanga mauaji ya Rais Moise aliwasiliana na Waziri Mkuu usiku wa tukio

Soma - https://jamii.app/ClaudeOutHaiti
Siku ya Demokrasia Duniani huadhimishwa kila Septemba 15, ikitoa fursa ya kuangalia hali ya Demokrasia.

Miongoni mwa misingi muhimu ya Demokrasia ni kuheshimu #HakiZaBinadamu

Mataifa yanasisitizwa kulinda #UhuruWaKujieleza, Uhuru wa Habari na Haki nyingine

#DemocracyDay
DAR: Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo kesi yao itasikilizwa

Miongoni mwa watakaotoa ushahidi ni pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai

Soma - https://jamii.app/MboweKesiDar
ZINGATIA DOZI KULINGANA NA AINA YA CHANJO YA #COVID19

Wataalamu wanabainisha kuwa kila chanjo huwa na masharti ya idadi ya dozi na muda sahihi wa kuchanjwa

Unashauriwa kuzingatia masharti ya chanjo kujiimarisha dhidi ya Corona

Soma - https://jamii.app/MashartiChanjo

#UVIKO3
NJIA ZA KUFUNGA KIOO CHA SIMU NA USALAMA WAKE (SCREEN LOCK) - 1

SLIDE TO UNLOCK: Hii ni njia rahisi na isiyoshauriwa kutumika kwasababu ni rahisi Mtu mwingine anaweza kufungua Simu yako

PIN CODE LOCK: Hizi ni namba zinazotumika kufunga screen ya simu yako. Ni njia kongwe zaidi ya ulinzi wa Simu

PATTERN LOCK: Njia hii imekuwa ikikosolewa sana na Wataalamu wa #UlinziWaKidigitali. Inaelezwa ni rahisi kwa mdukuzi kukariri mchoro ama 'pattern' zako.

Soma - https://jamii.app/ScreenLocks
#UlinziWaData
SIKU YA DEMOKRASIA: Rais Samia amesema #Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazoongoza kwa kuwa na Vyombo vingi vya Habari

Amesema kwa takwimu za Mei 2021 Magazeti ni 257, Redio 197, Runinga 50, Online TV 451 na Blogu 122

Soma - https://jamii.app/MaadhimishoDemokrasia

#DemocracyDay
RAIS SAMIA: TUTAMUWEKA RAIS MWANAMKE 2025

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyofanyika Dar amesema "Rais Mwanamke tutamuweka 2025. Wameanza kutuchokoza, kuandika kwenye 'vigazeti' Samia hatasimama. Nani kawaambia?"

Soma - https://jamii.app/Urais2025
RAIS SAMIA: CHANGAMOTO ZA DEMOKRASIA BADO ZIPO NCHINI

Akizungumza leo amesema hakuna Taifa ambalo lina ukamilifu ktk suala hilo

Ameeleza, "Pamoja na ukweli kwamba Demokrasia ni lengo, pia ni mchakato. Ni suala ambao ni endelevu"

Soma - https://jamii.app/MaadhimishoDemokrasia

#DemocracyDay
ETHIOPIA: #TIGRAY YAKOSA HUDUMA YA INTANETI KWA SIKU ZAIDI YA 300

Huduma hiyo imekosekana tangu kuanza kwa mzozo Novemba 2020

Kukosekana kwa Intaneti kumesababisha Matukio ya Ukiukwaji wa #HakiZaBinadamu kushindwa kurekodiwa

Soma - https://jamii.app/TigrayInternetOff

#InternetAccess
MDAU: NJIA ZA KUKUSAIDIA KATIKA MATUMIZI MAZURI YA MUDA

1. Anza kwa kupanga siku yako vyema: Jifunze kujiwekea malengo ili kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku hiyo

2. Gawanya kazi katika sehemu ndogondogo: Unapogawanya kazi katika vipande vidogo vidogo ni rahisi kuzitawala na kuzifanya kwa wakati

3. Weka vipaumbele: Jifunze kupanga kazi kulingana na vipaumbele vyake, usifanye kila kitu kwa sababu ni kazi bali fanya kwa kuongozwa na vipaumbele

Soma - https://jamii.app/MatumiziMuda
#Maisha
ZIMBABWE: WATUMISHI WA UMMA WASIOPATA CHANJO WAZUIWA KWENDA KAZINI

Serikali imesema walipewa muda wa kutosha kupata chanjo dhidi ya #COVID19

Mamlaka zinasema takriban 90% ya watu wanaolazwa Hospitali kwasababu ya Corona hawajapata chanjo

Soma - https://jamii.app/ChanjoZimbabwe

#UVIKO3
WB: WATU MILIONI 216 KUKIMBIA MAKAZI YAO KUTOKANA NA UCHAFUZI WA HEWA

Athari zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama upungufu wa Maji, uzalishaji chakula, ongezeko la Maji Baharini zinaweza kusababisha uhamaji wa Watu kufikia 2050

Soma - https://jamii.app/RefugeesClimate
MWIGULU: MKOPO WA IMF KUTUMIKA KWENYE SEKTA ZILIZOATHIRIWA NA #COVID19

Asema tayari Tsh. Trilioni 1.3 zimepokelewa na zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kupunguza msongamano wa Wanafunzi darasani na Wagonjwa Hospitalini

Soma https://jamii.app/IMFMkopoTZ

#UVIKO3
DRC: WAANDAMANAJI WAKAMATWA NA WENGINE KUJERUHIWA NA POLISI

Wafuasi hao ni wa Chama cha Upinzani cha Ecidé kinachoongozwa na Martin Fayulu

Maandamano yalilenga kushinikiza mabadiliko ktk Tume ya Uchaguzi, na kwenye Mahakama ya #Katiba

Soma - https://jamii.app/ProtestsDRC
#Democracy
LEBANON: Ndugu wa Wahanga wa mlipuko uliotokea #Beirut Agosti 2020, walionusurika na Mashirika ya Haki za Binadamu wametaka kufanyika uchunguzi huru chini ya Umoja wa Mataifa (UN)

Wamesema Uchunguzi wa ndani umekuwa unakwamishwa mara kwa mara

Soma - https://jamii.app/UNBeirut