JamiiForums
56.4K subscribers
32.6K photos
1.81K videos
29.8K links
Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained
Download Telegram
RUVUMA: MWANAFUNZI AFARIKI KWA KIPIGO KUTOKANA NA KUFELI MTIHANI WA MOCK

Mwanafunzi aliumia na kupata uvimbe kwenye paja la kulia na katikati ya mgongo na ndipo Wazazi wake walipompeleka Kituo cha Afya

Walimu sita wanashikiliwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/KifoMtihaniMock
#JFLeo
WIZARA YA MAWASILIANO YAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUSAINISHWA MIKATABA ILIYO KATIKA LUGHA YA KIGENI

Naibu Waziri, Mhandisi Kundo Mathew amesema mikataba ya Lugha Ngeni ina nia ovu kwa Wananchi

> Ili ieleweke inapaswa kuwa kwa Kingereza na Kiswahili

Soma https://jamii.app/LughaNgeni
RAIS MACRON ANAONGOZA ORODHA YA WANAOLENGWA NA UDUKUZI

Kwa mujibu wa Gazeti la #Washington Post, miongoni mwa Namba 50,000 za Simu zilizo kwenye orodha ya udukuzi, zipo namba za Rais wa Afrika Kusini (aliyelengwa na Rwanda) na Barham Salih wa #Iraq

Soma https://jamii.app/MacronNSOAttack
NJOMBE: WANAFUNZI WATORO WALIPISHWA FAINI YA TSH. 5000 KWA KUTOFIKA SHULENI

Wakazi wa Mavanga, wilaya ya Ludewa wamelalamikia faini hiyo kwa kila siku mwanafunzi anayoshindwa kufika shuleni

> Aidha wamelalamika kulipishwa Tsh. 10,000 ya walimu wanaojitolea

Soma https://jamii.app/NjombeWatoro
NJOMBE: JIKO LA MKAA CHUMBANI LASABABISHA VIFO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amesema waliofariki ni Benitho Mbatha (23) na Jazila Said (27)

> Wawili hao waliingiza jiko la mkaa chumbani ili kupunguza baridi ndani

Soma https://jamii.app/MkaaNjombe
MYNAMAR: MADAKTARI WAJIFICHA HUKU WAGONJWA WAKIZIDI ONGEZEKA

Wagonjwa wa #COVID19 waongezeka huku wengi wakitibiwa nyumbani kutokana na Hospitali kukosa Madaktari na Vifaa Tiba

> Oksijeni imeendelea kuwa haba kwa ongezeko la Wagonjwa

Soma https://jamii.app/MynmarCOVID19
#UVIKO3
MADHARA YA KULALA NA JIKO LA MKAA NDANI

Endapo utalala na Jiko la Mkaa ndani ya chumba halafu umefunga Milango pamoja na Madirisha yote, itasababisha Jiko litumie #Oxygen nyingi kuendelea kuwaka na litazalisha kiwango kikubwa cha #Carbonmonoxide ambayo ni mbaya kwa Binadamu

Hali ambayo husababisha Mtu kukosa kabisa hewa na matokeo yake ni kushindwa kupumua na kupoteza Maisha.

#JamiiForums #Afya
IJUE PEGASUS INAYOTUMIWA NA MAMLAKA MBALIMBALI KUFUATILIA WANAHARAKATI NA WANAHABARI

Imetengenezwa 2018 na NSO (Kampuni Israel), inaweza kudukua hadi iOS 14.6

> NSO imedai iliitengeneza ili kudhibiti wahalifu ila Mamlaka zinaitumia vibaya

Soma https://jamii.app/Pegasus
#DigitalSecurity
POLISI: MBOWE ALISAFIRISHWA KWENDA DAR KUHOJIWA KWA MAKOSA MENGINE

Polisi Mkoa wa Mwanza imesema Freeman Mbowe alikamatwa Julai 21, 2021 na alipelekwa Dar kwa mahojiano

> Atarudishwa Mwanza kuungana na wenzake wanaoshikiliwa kuhusiana na Kongamano

Soma https://jamii.app/MboweDar
#JFLeo
NAWA MIKONO VYEMA KUEPUKA MAAMBUKIZI YA #COVID19

> Endelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Korona #UVIKO3 kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji safi tiririka

ILANI: Elimu hii ni katika kukumbushana mambo muhimu ya kuzingatia kukabiliana na mlipuko huu

#UVIKO3
AZAN ZUNGU: UJERUMANI YENYEWE IMEWEKA 'SOLIDARITY FUND'

Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu amesema kodi imewekwa kwaajili ya Watu wenye uwezo ambapo kati ya Watu Milioni 50 wanaomiliki line za Simu, Watu Milioni 20 hawalipi hii kodi

Asema "Ujerumani yenyewe imeweka 'Solidarity Fund' ili kuwasaidia wenye uwezo mdogo. Ukikatwa usijiwaze wewe, waza wale ambao wana hali ya chini kuliko wewe"

Soma - https://jamii.app/ZunguTozoSimu
#TozoYaMiamala
MADAGASCAR: RAIS ANUSURIKA KUUAWA

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina amenusurika katika jaribio la mauaji

> Raia kadhaa wa kigeni wamekamatwa kufuatia tukio hilo wakiwemo Raia wawili wa Ufaransa

Soma https://jamii.app/AssasinationAttempt
#JFLeo
TANZIA: ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa #Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha

Aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo mwaka 2015

#JFLeo #RIPMghwira
MTEJA ANA HAKI YA KUPATA TAARIFA KUHUSU HUDUMA AU BIDHAA

Kutangaza bidhaa Mtandaoni bila taarifa sahihi huleta usumbufu kwa kuwa Wateja hupata bidhaa ambazo hawakuzitarajia

> Ukitangaza biashara weka taarifa zote ikiwemo bei

Soma https://jamii.app/TaarifaBidhaa
#BiasharaNaDigitali
USAFI WA MWILI: Inashauriwa kuoga kila siku kwa kutumia sabuni na Maji ili kuondoa Seli zilizokufa kwenye Ngozi, Mafuta pamoja na Bakteria

Unapooga hakikisha unasugua vizuri maeneo ambayo huzalisha Jasho kwa wingi ikiwemo Kwapani, Katikati ya vidole vya Miguu, na sehemu za siri

Pia, unashauriwa kuosha Nywele zako kwa 'Shampoo' angalau mara moja kwa wiki, au zaidi ikiwezekana. Tumia 'Deodorant' wakati umeshaukausha Mwili vizuri ili kuzuia harufu.

#JamiiForums #PersonalHygiene #Usafi
PROF. LIPUMBA APATA CHANJO YA CORONA, ASHAURI WANANCHI WAJITOKEZE KUPATA CHANJO

M/Kiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya COVID-19 ktk kliniki ya UN, Masaki

> Amewashauri Wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo

Soma https://jamii.app/LipumbaChanjo
#UVIKO3
LINDI: WATU WATATU WAUAWA KUTOKANA NA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Chande Magoma alimkuta Mfugaji akilisha ktk shamba lake wakapigana na kupata majeraha yaliyopelekea vifo vyao

> Pia, Wanakijiji walimuua kijana 1 wakiamini ni Jamii ya Wafugaji

Soma https://jamii.app/MauajiLindi
JamiiForums inatoa Salamu za Rambirambi/Pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa #Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira
-
Marehemu amekuwa Mwanachama Hai wa JamiiForums kwa zaidi ya miaka 9, akishiriki na kuanzisha mijadala yenye tija hususani kuhusu Sekta ya Elimu Tanzania
-
Tunawaombea faraja wote walioguswa na Msiba huu na Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi

#RIPMghwira
IRINGA: MIKUTANO ISIYO YA LAZIMA YAZUIWA ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA COVID-19

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema maambukizi ya #COVID19 yanaongezeka mkoani humo

> Ametoa wito kwa Wananchi kuchukua tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa

Soma https://jamii.app/CoronaIringa
#UVIKO3