JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS WA URUSI AWAFUKUZA KAZI MAJENERALI 5

> Rais Vladmir Putin amewafuta kazi majenerali 5 ktk Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Dharula, Baraza la Uchunguzi na Huduma za Magereza

> Aidha, Novemba 2019 alifukuza Majenerali wengine 11

Soma - https://jamii.app/PutinFiresGenerals
#JFLeo
MICHEZO: Mchezo wa Yanga dhidi ya Tanzania Prisons wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliokuwa uchezwe kesho, Desemba 27 umeahirishwa kutokana na Uwanja wa Sokione kuwa katika hali mbaya hivyo mchezo utapangiwa tarehe nyingine
-
Timu zote zimefikia makubaliano hayo baada ya kupokea taarifa ya hali isiyoridhisha kiusalama kwenye Uwanja huo na kutakiwa kutafuta viwanja mbadala
SERENGETI: MVUA YAUA WATU 3 NA KUHARIBU MIUNDOMBINU

> Mvua kubwa iliyonyesha usiku imesababisha vifo vya watu 3 wakiwamo watoto 2 wa familia moja na dereva wa bodaboda aliyesombwa na maji barabarani

> Imesababisha daraja la Nyiberekera kukatika na barabara za kutoka Mugumu kwenda Arusha kupitia Fort Ikoma na Makunduzi kujaa maji

Soma - https://jamii.app/MadharaVifoMvuaSerengeti
EPL: CHELSEA YABAMIZWA GOLI 2-0 NYUMBANI KWAKE

Chelsea FC ilikuwa ikicheza na Southampton Fc. Magoli ya @SouthamptonFC yamefungwa na Obafemi dakika ya 31 na Redmond kunako dakika ya 73

> Klabu ya @ChelseaFC imekuwa na matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni

#JFSports
KENYA: WATU 3 WAFARIKI BAADA YA DALADALA KUGONGANA NA GARI LILILOBEBA KONDOO

> Ajali hiyo imetokea katika eneo la Nangili katika Barabara Kuu ya Kitale kwenda Eldoret

> Imeelezwa kuwa Madereva wa magari yote wamefariki pao hapo

Soma > https://jamii.app/AjaliEldoretKenya

#JamiiForums
SHANGHAI, CHINA: BINTI WA BRUCE LEE AWASHTAKI WALIOTUMIA TASWIRA YA BABA YAKE

> Shannon Lee ameishtaki Kampuni ya Vyakula iliyotumia sura ya Baba yake kwenye matangazo yao ya biashara bila ya kukubaliana na familia ya Bruce Lee

> Anaitaka Kampuni hiyo kulipa fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 68.7 za Kitanzania

Zaidi, soma => https://jamii.app/ShannonLee
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KAZAKHSTAN: NDEGE ILIYOBEBA ABIRIA 100 YAANGUKA, 14 WATHIBITIKA KUFARIKI, 35 MAJERUHI

> Ndege ya #AirBek imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Almaty

> Ilikuwa ikielekea Mji Mkuu wa Kazakhstan wa Nursultan

Soma > https://jamii.app/AirBekCrashes

#PlaneCrash
KENYA: AKAMATWA KWA KUMLAZIMISHA MTOTO WA MIAKA 2 KUNYWA BIA

> Polisi wanamshikilia Mwanaume wa miaka 30 kwa kumlazimisha Mtoto wa miaka 2 kunywa bia siku ya Krismasi

> Wanafamilia walimkimbiza Mtoto Hospitali wakihofia anaweza kupoteza maisha

Soma > https://jamii.app/BiaMtotoKE
KENYA, GARISSA: WAFANYABIASHARA 2 WATEKWA NA AL-SHABAAB

> Polisi mjini Garissa wameanzisha juhudi za kuwaokoa Abdulahi Isaack Harun na Abdi Hassan wanaoaminika kutekwa nyara jana Asubuhi na Kundi la Al-Shabaab

> Inadaiwa walichukuliwa katika eneo la Wardeglo Dam na kupelekwa Somalia

Soma - https://jamii.app/KenyansAbductedAlShabaab
RAIS AONGEZA SIKU 20 KWA AJILI YA USAJILI WA LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE

> Rais John Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia Januari 1, 2020 kwa watu wote watakaoshindwa kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole ifikapo Desemba 31

> Desemba 31 ulikuwa ndiyo ukomo wa muda wa awali wa kuwataka wananchi kusajili laini zao na baada ya hapo zisizosajiliwa zingefungwa

Soma - https://jamii.app/OngezoMudaUsajiliLaini
FAHAMU KUHUSU KODI INAYOTOKANA NA AJIRA (PAYE) INAYOLALAMIKIWA NA WENGI

> Kodi inayotokana na Ajira inajulikana kama Lipa Kadiri Unavyopata (PAYE). Sehemu ya 81 ya Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mwajiri kushikilia kodi kutoka kwa malipo ya mfanyakazi na kuilipa TRA

> Viwango vya kodi ambavyo mtu anatakiwa kukatwa vinatofautiana kulingana na kiwango cha kipato anachopata mtu kwa mwezi ambapo kipato cha chini kukatwa ni malipo ya Tsh. 170,000 kwa mwezi

Soma - https://jamii.app/FahamuKodiMshahara
SERIKALI YAKUSUDIA KUKATA RUFAA DHIDI YA ABDUL NONDO

> Hii ni baada ya Mahakama Kuu(Iringa) kumpa ushindi, Abdul Nondo ktk rufaa iliyokatwa na Serikali

> Serikali inapinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa iliyoeleza kuwa Nondo hana hatia

Soma > https://jamii.app/GvtVsAbdulNondo
POLISI DODOMA: MMILIKI WA SHULE YA ZAMZAM ALIFARIKI KWA MATATIZO YA MOYO

> Kamanda Gilles Muroto, amesema kwamba hawakukuta viashiria vyovyote vya mauaji, badala yake uchunguzi umebainika kuwa Sheikh Rashid Bura alifariki baada ya kukosa msaada kwa kuwa hali hiyo ilimkuta ofisini akiwa peke yake

Soma - https://jamii.app/RipotiKifoBuraZamZam
UGANDA YAPATA HASARA KIBIASHARA KUTOKANA NA MIZOZO NA NCHI JIRANI

> Sekta ya Biashara nchini Uganda imepata pigo kubwa mwaka huu kwa kupata hasara ya takriban trilioni 3.4 kutokana na mizozo ya kibiashara na mataifa jirani

> Ripoti ya ufanisi wa kibiashara ya mwaka 2018/2019 imesema shughuli za kibiashara kati ya Uganda na mataifa jirani, zilipungua kutoka dola milioni 932 mwaka 2017/2018, hadi dola milioni 11, 2019

Soma - https://jamii.app/UGLossBusinessConflict
EPL: WOLVES YAIADHIBU MAN CITY KWA GOLI 3-2

> Man City imekubali kipigo hicho usiku huu ikiwa ugenini katika mechi iliyoshuhudia miamba hiyo ya soka ikicheza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya kipa wake kupata kadi nyekundu

#WOLMCI #EPL
DAR: DAKTARI ASHTAKIWA KWA UTOAJI WA MIMBA NA KUTAKATISHA FEDHA

> Ni Dkt. Awadhi Juma wa Dental Clinic(Sinza) pamoja na Muuguzi Kidawa Ramadhani(26) wa Kituo cha Afya Manzese

> Wanakabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo kutakatisha Tsh. 260,000

Soma > https://jamii.app/DaktariKutakafishaFedha
MOGADISHU, SOMALIA: BOMU LILILOTEGWA KWENYE GARI LALIPUKA NA KUUA WATU ZAIDI YA 20

> Bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye gari, kwenye Kituo cha Ukaguzi cha Polisi

> Imeelezwa kuwa, shambulio hilo lilikilenga Kituo cha Ukusanyaji wa Mapato

Soma > https://jamii.app/BomuLaua5Somalia