JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AJALI KIPINDI CHA KRISMASI: ZAMBIA YAPOTEZA RAIA 21

> Watu 21 wamefariki na wengine 22 kujeruhiwa ktk ajali za barabarani kipindi cha Krismasi 2019

> Idadi ya ajali za barabarani wakati huu wa Krismasi imeongezeka kutoka 125 za mwaka 2018 hadi 139 kwa mwaka huu

Soma - https://jamii.app/RoadAccidentsChristmas
JAPAN YAIPA MSAADA WA TSH. BILIONI 4.2 TANZANIA KUFUFUA SHIRIKA LA UVUVI

> Serikali imesaini mkataba na Serikali ya Japan wa kupokea msaada wa Tsh. bilioni 4.2 kwa ajili ya kulifufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), lililositisha shughuli zake tangu mwaka 1998

> Fedha hizo zitatumika kununua meli mpya ya uvuvi, mashine ya kutengeneza barafu, ghala la baridi la kuhifadhia samaki na vifaa vya kuvulia samaki na vya karakana

Soma - https://jamii.app/MsaadaKufufuaTAFICO
UTAFITI: KUFUNGA KULA KILA WIKI HUREFUSHA MAISHA NA KUZUIA MAGONJWA

> Watafiti nchini Marekani wamebaini kwamba kutokula kwa masaa 16 - 18 au kufunga kula kila baada ya muda fulani katika wiki huukinga mwili na magonjwa ikiwa ni pamoja na Shinikizo la Damu, Kiribatumbo, Kisukari na Magonjwa ya Moyo

Soma - https://jamii.app/EffectsIntermittentFasting
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: MAGUGU MAJI YASABABISHA ADHA KWA WASAFIRI

> Meli na vivuko vimepata wakati mgumu kusafirisha wananchi baada ya magugu maji kutanda katika Ziwa Victoria

> Mwezi uliopita pia hali hii ilikuwepo na wasafiri walipata adha ya usafiri
FARU FAUSTA AMEKUFA

> Ni faru anayeaminika kuwa mzee zaidi duniani na amekufa akiwa na miaka 57

> Fausta ameishi maisha yake yote katika Hifadhi ya Ngorongoro mpaka umauti ulipomkuta jana Ijumaa, Disemba 27, 2019

> Faru Fausta licha ya umri wake mkubwa hakuwahi kuzaa na hiyo inaelezwa kuwa huenda ikawa ni moja ya sababu ya kuishi kwake kwa muda mrefu

#FaruFausta #JFLeo #animal
RUKWA: MTOTO AFARIKI NA WATU WENGINE 30 KULAZWA BAADA YA KULA MZOGA WA NGURUWE

> Mareni Namsukuma (7) amefariki na wengine 30 wakazi wa Wilayani Kalambo wanaendelea kupatiwa matibabu baada ya kula nyama ya Mzoga wa Nguruwe

> Mwanakijiji mwenzao aliwauzia nyama ya Nguruwe ambaye alikuwa amekufa bila kujua kilichomuua

Soma - https://jamii.app/KifoNyamaMzogaNguruwe
MVUA KUBWA KUIKUMBA MIKOA 6 TANZANIA, TMA YATOA TAHADHARI

> Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar, Morogoro, Pwani, Mikoa ya Kusini pamoja na Unguja na Pemba ni za siku tano mfululizo na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari

Soma - https://jamii.app/TahadhariMvuaRadiUpepo
TEMESA YAKANUSHA KUHUSU MAGUGU KUZUIA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI MWANZA

> Wakala wa Ufundi na Umeme imekanusha uvumi unaoenea mitandaoni kupitia video pamoja na picha vikielezea kusimama kwa huduma za vivuko Mkoani Mwanza kutokana na kuwepo kwa Magugu Maji

> Imesema, tukio la Magugu Maji lilitokea siku ya Desemba 24 na tayari Magugu hayo yaliondolewa

Soma - https://jamii.app/KanushoMaguguKuzuiaVivuko
JE, WAIJUA ADHABU ANAYOWEZA KUPEWA KIJANA ANAYETUHUMIWA KUBAKA WATOTO 12, IRINGA?

> Arnold Mlay anatuhumwa kuwalawiti Watoto 12 katika kituo chake cha 'Video Games' huko Semtema Iringa

> Kuifahamu adhabu ya kubaka kwa mujibu wa kanuni ya adhabu, soma => https://jamii.app/AMlayMbaroni
TABORA: WANASIASA WADAIWA KUCHOCHEA MAUAJI YA ASKARI WA WANAYAMAPORI

> Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgogoro wa Misitu ya Hifadhi wa Isawima umekuwa ukichochewa na Kiongozi wa Wafugaji ambaye ni Mwanasiasa katika eneo hilo, jambo lililopelekea Askari 2 kuvamiwa na kuuawa

Soma - https://jamii.app/SiasaMauajiAskariPori
SHEIKH BURA ALIYEKUTWA AMEFARIKI OFISINI KWAKE ALIKUWA NANI HASA?

> Aliwahi kuwa mlinzi wa getini wa Ikulu Jijini Dar (Kipindi cha Mwalimu Nyerere) kwa miaka 3 mfululizo

> Alifanya kazi ndani ya Jeshi la Polisi katika Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID)

> Aliwahi kufanya kazi Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Zaidi, soma > https://jamii.app/RIPRashidiBura
TCRA YAZIPIGA FAINI YA TSH. BILIONI 5.9 KAMPUNI ZA SIMU

> Ni baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya leseni na kukidhi viwango vya ubora wa huduma kwa mujibu wa Kanuni za Ubora wa Huduma 2018

> Airtel: 1.6 bilioni, TTCL: 1.6 bilioni, Halotel: 900 milioni, Zantel: 850 milioni, Tigo: 500 milioni na Vodacom: 450 milioni

Soma - https://jamii.app/TCRAFainiKampuniSimu
MICHEZO: CHELSEA FC YAINYUKA ARSENAL FC KWA MAGOLI 2 KWA 1

- Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) umechezwa katika Uwanja wa Nyumbani wa Arsenal FC(Emirates) huku Arsenal wakiwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Aubameyang kunako dakika ya 13

- Chelsea walijitutumua na kusawazisha kupitia kwa Jorginho dakika ya 83 kabla ya Tammy Abraham kufunga goli la mwisho dakika ya 87

#JFSports
MICHEZO: LIVERPOOL FC YAIBUKA NA USHINDI WA BAO 1 KWA 0 DHIDI YA WOLVES

> Goli la Sadio Mane lilitosha kuipa ushindi Liverpool dhidi ya Wolverhampton Wanderers

> Hadi sasa Liverpool Fc imeshinda michezo 18 kati ya 19 ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu

#JFSports
UKRAINE: SERIKALI NA WAASI WABADILISHANA WAFUNGWA

- Ni Serikali na Waasi wanaotaka kujitenga Mashariki mwa Ukraine na wanaoungwa mkono na Urusi

- Mwakilishi wa Waasi, Daria Morozova amedai wamerejeshewa Wafungwa 87 na kukabidhi watu 55

Zaidi, soma https://jamii.app/WaasiUkraineWafungwa
DODOMA: WATU SITA WAFARIKI KATIKA AJALI

- Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kisasa imehusisha gari aina ya Toyota Coaster na lori

- Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto amesema Watu wengine 12 wamejeruhiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliDes2019-DOM
DKT. BASHIRU ALLY AWASHANGAA WANAOPENDA ‘KAZI NA BATA’

- Amewataka Wananchi kupuuza kauli hiyo akidai itachangia kuzorotesha uchumi wa Taifa

- Amedai inadhalilisha Wanawake ambao wakati wote wamekuwa wakifanya kazi kusomesha watoto wao

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruAshangaaKaziBata