JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAIDA ZA KUTOA PONGEZI KWA MTOTO WAKO

> Pongezi hutoa hamasa kwa watoto kufanya mambo mazuri zaidi: Tabia inayopongezwa hukua zaidi na inayoadhibiwa hudumaa zaidi katika maisha ya mtoto

> Kwa kumpongeza mtoto wako utamfanya ajue kuwa unafuatilia juhudi zake hali itakayomfanya azidishe kufanya mambo mazuri anayoyafanya au kuyakamilisha

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/FaidaKupongezaMtoto
BENKI YA AfDB YATOA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA TANZANIA NA KENYA

> Benki ya Maendeleo Afrika yatoa Euro milioni 345 kusaidia ujenzi wa barabara za Mombasa-Lunga, Lunga/Horohoro na Tanga-Pangani-Bagamoyo katika awamu ya kwanza

> Umoja wa Ulaya umechangia Euro milioni 30 ikiwa ni asilimia 7.7 ya gharama za mradi kwa Serikali ya Kenya

Soma - https://jamii.app/AfDBFedhaUjenziTzKe
KENYA YATOA TAHADHARI YA DALILI ZA UWEPO WA SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari kuhusu vitisho vya uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya

> Inspekta Jenerali wa Polisi amewataka wananchi kuwa waangalifu katika maeneo ya kuabudu na katika vituo vya usafiri wa umma

Soma - https://jamii.app/TahadhariUgaidiSikukuu
INDONESIA: TAKRIBAN WATU 26 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA BASI KUANGUKA MTONI
-
Takriban Watu 26 wamepoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa nchini Indonesia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupoteza uelekeo na kuanguka katika korongo la Mto
-
Ajali hiyo ilitokea jana usiku katika Mkoa wa Sumatra Kusini mwa nchi hiyo ambapo basi hilo lilikuwa limebeba abiria karibu 50
-
Zoezi la uokoaji bado linaendelea kutokana na baadhi ya abiria kutoonekana na hivyo huenda wakawa wamepotelea ndani ya mto
BOLLEN NGETTI APATIKANA MAENEO YA TABATA SEGEREA, DAR

> Mwanaharakati huyo na Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, alipotea Desemba 23 kwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana

> Amekuwa akitekwa mara kwa mara na kutekwa kwake jana ilikuwa ni mara ya 4

Soma - https://jamii.app/NgettiApatikanaTabata
MAREKANI YAMUITA BALOZI WAKE WA ZAMBIA ALIYEKOSOA ADHABU KWA WAPENZI WA JINSIA MOJA

> Marekani imemuita Balozi Daniel Foote nyumbani baada ya kukosoa uamuzi wa Jaji nchini Zambia kuwafunga wanaume 2 kifungo cha miaka 15 kwa kupatikana wakifanya mapenzi mwaka 2017

> Rais Edgar Lungu alimtaja Balozi huyo kama miongoni mwa watu wasiotakiwa katika Taifa hilo na kuitaka Marekani kumuondosha

Soma - https://jamii.app/USCallsFooteHome
URUSI YAFANIKIWA KATIKA JARIBIO LA KUJITOA KWENYE INTANETI YA DUNIA

> Serikali ya Urusi imefanikiwa kufanya majaribio ya mtandao uitwao Runet, ambao ni mbadala wa mtandao wa intaneti unaotumika hivi sasa duniani

> Hata hivyo, Jaribio hilo linatafsiriwa kama mpango wa Serikali kuminya mawasiliano ya watu nchini Urusi

Soma - https://jamii.app/RussiaOwnInternet
KITUO CHA USALAMA KWA ALIYEKUWA RAIS WA NIGERIA CHASHAMBULIWA, ASKARI 1 AUAWA

> Kituo cha usalama cha nyumba ya Rais mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan katika jimbo la Bayelsa kimeshambuliwa na watu wenye silaha na askari 1 kuuawa

> Msaidizi wa Jonathan amesema watu hao walifanya shambulizi hilo kwa kutumia boti 5 za injini

Soma - https://jamii.app/ExPresdHouseAttacked
BURKINA FASO: WANAWAKE ZAIDI YA 30 WAUAWA KWENYE SHAMBULIO LA KIGAIDI

> Wapiganaji nchini Burkina Faso wamewaua raia 35, 31 kati yao wakiwa ni wanawake katika shambulio lililolenga kambi moja ya kijeshi

> Rais Roch Marc Christian Kabore ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa na mpaka sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulio hilo

Soma - https://jamii.app/CiviliansTerrorAttack
KIBRA, KENYA: AFARIKI KWA UMEME AKIJIANDAA KWA AJILI YA KRISMASI

- Mwanamke mmoja wa makamo amefariki dunia akiwa bafuni akioga

- Imeelezwa kuwa kifo chake kimetokana na hitilafu ya umeme

Zaidi, soma => https://jamii.app/AfarikiUmemeBafuni

#JamiiForums #JFLeo
MALEZI: MAMBO YA MUHIMU WAKATI WA KUANDAA RATIBA YA KILA SIKU YA MTOTO

> Mtoto ashirikishwe ktk kuandaa ratiba yake. Asipangiwe ratiba bali ushirikiane naye katika kuandaa ratiba kwani itamsaidia mtoto kuona ana wajibu katika familia

> Ni vizuri Ratiba iheshimiwe na kila mtu ndani ya familia. Muda wa kujisomea mtoto asitumwe dukani, muda wa mapumziko mtoto asiruhusiwe kwenda kucheza

> Mtoto asipoifuata ratiba aliyoshirikishwa kuiandaa zitafutwe njia za kumuwajibisha maana mafanikio yake yote hutegemea sana kwenye kupanga na kuheshimu ratiba yake

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UandaajiRatibaMtoto
#JFMalezi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
PIPI NA “BIG G” KAMA ZAWADI YA SIKUKUU KWA WAGONJWA TOKA KWA MBUNGE

> Katibu wa Mbunge Jimbo la Rorya(CCM), Lameck Airo (Lakairo) akigawa JoJo za ‘VEVE’ kwa Wagonjwa jimboni humo kama zawadi ya Sikukuu

> Video hii imeibua mjadala mitandaoni
KRISMASI: MAASKOFU WAKEMEA UCHU WA MADARAKA, UONEVU WA BINADAMU

> Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Frederick Shoo amekemea tabia za utekaji, utesaji, unyongaji haki, dhuluma na kiburi cha viongozi zinazolalamikiwa nchini

> Naye Askofu Liberatus Sangu wa Kanisa Katoliki Shinyanga amesema Uchu wa madaraka, maonevu, rushwa, tamaa ya mali na kutotenda haki huchochea machafuko ndani ya jamii

Soma - https://jamii.app/AskofuUtekajiUtesajiRaia
SUDAN YARUHUSU KRISMASI KUSHEREHEKEWA BAADA YA MIAKA 70

> Serikali ya Sudan imeruhusu siku ya Krismasi kuadhimishwa nchini humo na kuwa siku ya mapumziko kwa mara ya kwanza baada ya miaka 70

> Waziri anayeshughulikia masuala ya dini amesema hatua hii imekuja baada ya Katiba mpya kuruhusu uhuru wa kuabudu

Soma - https://jamii.app/SudanCelebratesChristmas
UFILIPINO: KIMBUNGA CHAUA WATU 16. WATU 58,000 WAHAMISHWA

> Kimbunga Phanfone kimeikumba nchi hiyo siku ya Sikukuu ya Krismasi

> Imeelezwa kuwa kiliambatana na mvua kubwa na upepo uliovuma kwa kasi ya Kilomita 120 kwa saa

Soma > https://jamii.app/PhanfoneManila
CHINA YAKAMATA WATU 99,000 WANAOJIHUSISHA NA WIZI KWA SIMU

> Polisi wamefungua kesi 118,000 za uhalifu wa utapeli kwa kutumia simu za mkononi na kuwakamata watu elfu 99 wakati wa operesheni ya "Cloud Sword" iliyoanza mwezi Juni 2019

> Kuanzia Januari hadi Novemba 2019, idadi ya kesi za uhalifu zilizofunguliwa zimeshuka kwa asilimia 3.9

Soma - https://jamii.app/ReportCyberFrauds
DODOMA: MMILIKI WA SHULE YA ZAMZAM AKUTWA AMEFARIKI OFISINI KWAKE. YADAIWA AMEUAWA

> Mwili wa Rashid Dalai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Islamic Foundation umekutwa ndani ya ofisi yake

> Baadhi ya viungo vimekutwa vimekatwa lakini hakuna damu

Soma > https://jamii.app/RIPDalai
KENYA: MWANAMKE AMUUA SHEMEJIYE BAADA YA KUMPIGA KOFI KWENYE MAKALIO

> Polisi wanamsaka Eunice Adhiambo aliyetoweka baada ya kumchoma kisu shemejiye baada ya kutokea mabishano kati yao na shemeji kudaiwa kumpiga kibao mwanamke huyo kwenye makalio

> Marehemu alikuwa amemtembelea mshukiwa ambaye alimkuta akichonga Mihogo

Soma - https://jamii.app/MauajiKofiMakalio