JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI AFANYA TEUZI 5

- Mhandisi Emmanuel Korosso anaendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)

- Prof. Shadrack S. Mwakalila anakuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Zaidi, soma https://jamii.app/UteuziNov10-2019
POLISI AFRIKA KUSINI WAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU 380

> Wamewakamata wahamiaji haramu 380 ambapo watu 300 wamekamatwa mjini Johannesburg ktk eneo la Hillbrow

> Kati ya watu 380 waliokamatwa 353 ni wanaume na 27 ni wanawake ambao ni raia wa Malawi na Zimbabwe

Soma - https://jamii.app/UndocumentedMigrants
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: Kauli ya Prof. Ibrahim Lipumba juu ya kinachoendelea
KIMBUNGA CHAUA 13 HUKO INDIA NA BANGLADESH

> Kimbunga #BulBulCyclone kimesababisha vifo vya watu takriban 13 huku wengine zaidi milioni 2 wakiyakimbia makazi yao

> Kilikuwa na kasi ya Km 120 kwa saa

> Watu 5 kati ya 6 waliokufa nchini Bangladesh waliangukiwa na miti huku wengine 7 wafariki Nchini India

#JFLeo
DR CONGO: KIONGOZI WA KIKUNDI CHA WAASI CHA KABILA LA WAHUTU(FDLR) AUAWA

- Vikosi vya Serikali ya Congo vimemuua Musabyimana Juvenal ikiwa ni miezi 2 baada ya Kamanda mwingine wa FDLR, Sylvester Mudacumura kuuawa mnamo Septemba 2019

Soma > https://jamii.app/JuvenalVsDRCTroops
RAIS WA BOLIVIA AJIUZULU NA KUITISHA UCHAGUZI UPYA

- Rais Evo Morales amejiuzulu kutokana na vurugu zinazoendelea tangu ashinde uchaguzi wa Oktoba 20

- Akubali uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu na kutangaza nia ya kuitisha uchaguzi upya

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisBoliviaAjiuzulu-UchaguziMpya
SIFA ZA KUWA MBUNGE

- Mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo;

- Ni raia wa Tanzania, ametimiza miaka 21, awe anajua kusoma na kuandika (Kiswahili/Kiingereza), Mwanachama na mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa

#UmuhimuKatiba
ASKOFU MDEGELA: UCHAGUZI S/MITAA UAHIRISHWE ILI MAMBO YA KISIASA YAKAE SAWA KWANZA

> Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Owdenburg Mdegela amesema ni vizuri kwa wanasiasa kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kupata suluhisho linaloweza kusaidia Vyama vya Siasa kuingia kwenye chaguzi

> Ameonya nchi kwa sasa ikikosa upinzani itasababisha matatizo na ikiendelea hivi mwakani italeta doa kwenye uchaguzi wa Rais na Wabunge

Soma - https://jamii.app/AskofuUchaguziSMitaa
IRAN: SHIRIKA LA MAFUTA LAGUNDUA HIFADHI MPYA YENYE KIWANGO KIKUBWA CHA MAFUTA

> Kitengo cha utafutaji mafuta cha shirika la mafuta la Iran kimegundua hifadhi mpya ya mafuta ambayo ina mapipa bilioni 53 katika eneo la ukubwa wa Kilomita za mraba elfu 2,400 ambayo yanapatikana katika kina cha mita 80

Soma - https://jamii.app/NewOilReserves
WAZIRI MKUU, PEDRO SANCHEZ ASHINDA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA KITAIFA HISPANIA

> Chama cha Kisoshalisti kimeshinda katika Uchaguzi Mkuu wa Kitaifa wa Hispania kwa kupata viti 120 katika Bunge la Kitaifa

> Takriban wapiga kura milioni 37 walipiga kura Jumapili

Soma - https://jamii.app/SanchezWinsSpainElection
TUME YA HAKI ZA BINADAMU

- #Katiba inatambua: Tume ya Haki na Utawala Bora itatekeleza jukumu la kupokea malalamiko ya uvunjaji wa Haki za Binadamu

- Mdau wa Jamiiforums anahoji iwapo Wananchi wanalijua jukumu hili la Tume na je, Wananchi hufikisha malalamiko?

#UmuhimuKatiba
CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHATOA MASHARTI ILI KISHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

> Sharti la kwanza ni uchaguzi huo kufutwa na mchakato wake kurejewa upya na sharti la pili ni kanuni za uchaguzi huo zitungwe upya na zifanyike kwa maridhiano na wadau wote hususan wanasiasa sambamba na kuahirisha tarehe ya uchaguzi

> Sharti la tatu ni uundwaji wa Kamati Huru ya Uchaguzi na isisimamiwe na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na sharti la nne ni Seleman Jafo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuitisha kikao cha maridhiano na Vyama vya Siasa, juu ya namna ya kushiriki uchaguzi huo

Soma - https://jamii.app/ACTUchaguziSMitaa
MADARAKA YA UMMA KUPITIA SERIKALI ZA MITAA

- Ibara ya 146.-(1) ya #Katiba: Moja ya lengo la kuwapo Serikali ya Mitaa ni kupeleka madaraka kwa Wananchi

- Serikali za Mitaa zinahakikisha utekelezaji wa #Demokrasia pamoja na kuharakisha maendeleo ya Wananchi

#UmuhimuKatiba #JFLeo
MAMBO YA KUFANYA NA KUTOFANYA UNAPOKUWA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

> Kuongopa: Watu huongopa kwa kuogopa baadhi ya matibabu kama upasuaji na sindano. Watu wengi hawatambui kwamba kutotoa taarifa za kutosha kwa Daktari kutafanya Daktari kushindwa kutoa bainisho sahihi la kile unachoumwa

> Kujitolea bainisho la ugonjwa mwenyewe (Kujitibu): Wagonjwa waliosoma kwenye mitandao habari kuhusu wanachoumwa huwalazimisha madaktari kutoa matibabu kulingana na walivyosoma. Ni vyema kutambua ni daktari pekee ndiye anayeweza kutoa bainisho sahihi la ugonjwa unaoumwa

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MazingatioKituoAfya
#JFAfya
KATAVI: WAGANGA WA TIBA ASILIA KUJENGA HOSPITALI KWA FEDHA ZAO WENYEWE

> Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema wana mpango wa kujenga Hospitali itakayotumiwa na Waganga wa Tiba Asilia waliopo katika Mkoa huo, lengo likiwa kuondoa Ramli Chonganishi katika Mkoa ambazo husababisha matatizo katika jamii na kuwaondoa Waganga hao vichochoroni na kuwa sehemu moja

Soma - https://jamii.app/UjenziHospitaliTibaAsili
MICHEZO: SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU DUNIANI (FIFA) LAMFUNGIA JAMAL MALINZI KUJIHUSISHA NA SOKA KWA MIAKA 10

- Kamati ya Maadili ya Shirikisho hilo imemkuta Jamal Malinzi na hatia ya matumizi mabaya ya fedha kutoka FIFA na kufoji nyaraka

Soma > https://jamii.app/FIFAVsMalinzi
MEXICO YAIOMBA FBI KUSAIDIA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA RAIA WA MAREKANI

> Serikali ya Mexico imetoa mwaliko kupitia barua ya kidiplomasia na kuliomba Shirika la FBI kushiriki katika uchunguzi wa shambulio ambalo liliwauwa raia 9 wa Marekani na Mexico Jumatatu ya wiki iliyopita

> Watu wenye bunduki waliwauwa wanawake 3 na watoto 6 kutoka jamii ya Wamormoni Kaskazini mwa Mexico

Soma - https://jamii.app/MexicoInvitesFBI
PALESTINA: KIONGOZI WA KIKUNDI CHA JIHADI CHA UKANDA WA GAZA AUAWA

- Baha Abu Al-Atta amefariki kufuatia shambulio la anga lililotekelezwa na vikosi vya Serikali ya Israeli

- Licha ya kuuawa kwa Al-Atta, watu wengine 3 wamejeruhiwa

Zaidi, soma > https://jamii.app/Al-AttaAuawa
MICHEZO: RAHEEM STERLING AONDOLEWA KIKOSI CHA UINGEREZA

> Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuzuka ugomvi kati ya Raheem Sterling na Joe Gomes wakati wa mazoezi

Zaidi, soma => https://jamii.app/SterlingVsGomes

#JFSports