JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BUNGE KUPITISHA SHERIA YA KURUHUSU WATU KUJIPIMA VVU MAJUMBANI

> Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia Ijumaa Bunge la Tanzania litaipitisha Sheria inayotoa mamlaka kwa mtu kujipima UKIMWI, lakini itampasa mtu kwenda hospitali kupima tena ili ajiridhishe na majibu ya afya yake

> Aidha, kuna Mapendekezo ya Sheria itakayoruhusu umri wa mtu kupima VVU ni uanzie miaka 15

Soma - https://jamii.app/HIVSelfTesting
BANGLADESH: TAKRIBAN WATU 15 WAFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI

> Takriban watu 15 wamefariki na wengine 58 wamejeruhiwa baada ya Treni mbili za abiria kugongana katika Wilaya ya Brahmnbaria Mashariki mwa Bangladesh leo

> Aidha, usafiri wa Treni katika Miji ya Dhaka, Sylhet na Chittagang umesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi la ukoaji

Soma - https://jamii.app/PassengerTrainsCollide
SIKU YA HOMA YA MAPAFU: KILA BAADA YA SEKUNDE 39 MTOTO HUFARIKI

> Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema ugonjwa huo uliua watoto zaidi ya 800,000 mwaka 2017, ukiwa unasababisha asilimia 15 ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5)

> Unawaathiri watu wote Duniani, lakini zaidi ni katika maeneo ya Asia Kusini na Afrika (Kusini mwa Jangwa la Sahara)

Soma - https://jamii.app/WorldPneumoniaDay
UCHUMI: BENKI KUU YAWAONYA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA SARAFU ZA MTANDAO NCHINI

- BoT imeeleza kuwa inatambua juu ya uwepo wa watu wanaofanya malipo kwa kutumia sarafu hizo na yapo matukio ya uhamasishaji wa sarafu hizo

Zaidi, soma > https://jamii.app/BoTCryptocurrency
CUF: HATUUTAMBUI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

- Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba amebainisha hayo na kusema viongozi watakaotangazwa watawahesabu sio halali

- Pia, CUF imewataka Wanachama wake kutoshiriki Uchaguzi huo kwa namna yoyote ile

Soma https://jamii.app/CUFhawatambui-USMitaa
UGANDA: POLISI WADAIWA KUKAMATA WATU 120 AMBAO NI WAPENZI WA JINSIA MOJA

> Polisi imedai kukamata watu 120 katika Baa moja Mjini Kampala kwa tuhuma za kujihusisha na Dawa za Kulevya

> Baa hiyo ni mahususi kwa ajili ya Wapenzi wa Jinsia Moja, lakini Polisi wamekana kuwa walikuwa wamekusudia kukamata Wapenzi Jinsia Moja

Soma - https://jamii.app/HomosexualPeopleArrested
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Rais Magufuli alipowasili katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre kwa ajili ya kuzindua kitabu cha Rais Mstaafu wa Awamu wa 3, Benjamin William Mkapa kiitwacho 'My Life, My Purpose'
ARUSHA: WATUHUMIWA WA UJANGILI WAKAMATWA NA SILAHA NA MINOFU YA NYAMA PORI

- Watuhumiwa hao 2 wamekamatwa wakiwa na silaha mbili za kivita na za jadi

- Aidha, wamekamatwa na meno 2 ya Tembo na minofu ya Nyamapori, kinyume cha Sheria

Soma > https://jamii.app/WatuhumiwaUjangiliArusha
UGANDA: MAMA ADAIWA KUMZIKA MTOTO WAKE AKIWA HAI

> Polisi katika Wilaya ya Apac nchini Uganda wameanza uchunguzi dhidi ya Mwanamke (19) anayedaiwa kumzika mwanaye wa kiume (miezi 2) akiwa hai siku ya jana (Jumatatu)

> Imesemekana alifikia hatua hiyo baada ya wazazi wake kumnyima chakula wakidai kuwa amezaa Mtoto Haramu

Soma - https://jamii.app/MamaAzikaMtotoHai
SERIKALI: AMBAYE HARIDHIKI NA SHUGHULI ZA UCHAGUZI AENDE MAHAKAMA ZA AFRIKA MASHARIKI

> Serikali imewataka watu ambao hawaridhiki na mwenendo wa shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, bado wanayo fursa ya kufungua kesi kwenye Mahakama za Afrika Mashariki au kushtaki katika Bunge la Afrika Mashariki

> Imesema Tanzania inafuata misingi ya Utawala Bora ya Afrika Mashariki

Soma - https://jamii.app/ShughuliUchaguziSMitaa
UGANDA: MWANANCHI ALISHTAKI SHIRIKA LA TAIFA KWA KUTOCHAPISHA SHERIA YA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU

> James Mubiru ameliburuza Shirika la Uchapishaji la Uganda (UPPC) katika Mahakama Kuu huko Kampala kwa tuhuma za kushindwa kutangaza na kuchapisha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (2019)

> Rais Yoweri Museveni alikubali Muswada huo mnamo Machi 31, lakini bado haujaanza hadi leo

Soma - https://jamii.app/MashitakaShirikaUchapishaji
BENJAMIN MKAPA: MAMA, BIBI NA BIBI YAKE MAMA WALITESWA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA

- Mzee Mkapa amesimulia jinsi imani za kishirikina huko kwao Lupaso, Mtwara zilivyosababisha Mama, Bibi na Bibi wa Mama yake kupigwa na kuteswa kwa tuhuma za kusababisha ukame

Soma > https://jamii.app/HistoriaMkapa
KENYA: HOSPITALI YA MOMBASA YATEKETEA KWA MOTO, WAGONJWA WAOKOLEWA

- Hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza Wagonjwa 125 na hakuna majeruhi walioripotiwa kutokana na ajali hiyo

- Wauguzi 117 walikuwa Hospitalini hapo wakiendelea na majukumu yao

Soma > https://jamii.app/MotoHospMombasa
NIGERIA: MUSWADA WA ADHABU YA KIFO KWA WANAOTOA KAULI ZA CHUKI WAWASILISHWA BUNGENI

> Muswada huo wa Sheria ya Kuzuia kauli zenye chuki wa mwaka 2019 unaeleza kuwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa itolewe kwa yeyote atakayekutwa na hatia ya kueneza chuki dhidi ya mwingine ambayo itapelekea kifo

> Unaelekeza kuundwa kwa “Tume Huru ya Kitaifa ya Kauli za Chuki” itakayozuia kauli hizo na kuishauri Serikali

Soma - https://jamii.app/MuswadaKauliChuki
HONG KONG: MIUNDOMBINU YA USAFIRI YAVURUGIKA KUTOKANA NA MAANDAMANO

> Waandamanaji mjini Hong Kong wamesababisha kuvurugika kwa usafiri mjini humo kwa siku ya pili mfululizo

> Vikundi vidogo vya waandamanaji vilifunga barabara na kutupa vitu katika reli na kuzuia Treni za mjini za chini ya ardhi na kusababisha mapambano na Polisi wa kutuliza ghasia

Soma - https://jamii.app/HongKongTransportDamages
1
WANAOAMBUKIZWA UKIMWI MAKUSUDI KUANZA KULIPWA FIDIA

> Bunge limefanya marekebisho ya Sheria ya Udhibiti wa Virusi vya UKIMWA (VVU) na UKIMWI, ambapo imeipa Mahakama kutoa amri ya fidia kwa mtu ambaye ameambukizwa VVU kwa makusudi

> Pia, limepitisha Umri wa Mtoto kujipima VVU kuwa ni miaka ni 15, huku Wabunge wa upinzani wakitaka iwe miaka 12

Soma - https://jamii.app/FidiaMaambukiziVVU
MAHAKAMA YAWAHUKUMU KUNYONGWA WATU 4 KWA HATIA YA KUMUUA KWA RISASI ALIYEKUWA RPC WA MWANZA

- Waliokutwa na hatia ni Abdallah Petro, Abdulrahman Ismail, Magige Mwita na Muganyizi Michael

- Imeelezwa walitenda kosa hilo Oktoba 13 mwaka 2012

Zaidi, soma > https://jamii.app/WaliomuuaBarlowKifo