JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YATAKIWA KUANZISHA PROGRAMU YA UZAZI WA MPANGO KWA WANAUME

> Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Khadija Nassir, ameitaka Serikali kuanzisha Programu za Uzazi wa Mpango kwa wanaume kwa kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha wana uwezo wa kuwapa mimba wanawake 9 kwa siku 1

> Tafiti mbalimbali Duniani zinaonesha mwanaume 1 ana uwezo wa kuwapa mimba wanawake 9 kwa siku 9, wakati mwanamke 1 ana uwezo wa kushika mimba 1 kwa miezi 9

Soma - https://jamii.app/UzaziMpangoMeVsKe
MICHEZO: Mshambuliaji wa Misri, Mo Salah ameripotiwa kuondolewa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri kinachojiandaa kucheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya (Harambe Stars) kuwania kufuzu michuano ya AFCON 2021 kutokana na kupata majeraha kwenye kifundo cha mguu
-
Chama cha Soka cha Egypt (EFA) kimethibitisha hilo na kimefafanua kuwa Nyota huyo wa Klabu ya Liverpool ataikosa michezo yote 2 ambayo Misri itacheza
SENETA AJITANGAZA KUWA RAIS MPYA WA BOLIVIA KWENYE KIKAO CHA WABUNGE

> Spika wa Bunge la Seneti la nchi hiyo, Jeanine Anez (52) amejitangaza kuwa Kaimu Rais katika kikao cha Bunge siku chache baada ya Rais wa Bolivia, Evo Morales kujiuzulu

> Anez amesema uamuzi huo ni hatua ya kujitolea ambayo amechukua kwa ajili ya nchi hiyo na kwamba ataitimiza kwa kuitisha uchaguzi haraka

Soma - https://jamii.app/AnezBoliviaPresident
SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO ILI KUNUNUA NDEGE YA MIZIGO

> Waziri wa Uchukuzi, Isack Kamwelwe amesema Serikali imeshaanza mazungumzo ya namna ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya mbogamboga ili kuyapeleka nje na kuwasaidia wakulima

> Asema, wana mpango wa kuanza kukodisha ndege kwaajili ya kusafirisha mazao ya 'HortiCulture' na minofu ya samaki kutoka Mwanza

Soma - https://jamii.app/SerikaliNdegeMizigo
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa kwanza kushoto) enzi hizo akiwa na wanafunzi wenzake
ARUSHA: WANAKIKUNDI WAZIMIA BAADA TSH. MILIONI 39 ZA KIKOBA KUDAIWA KUYEYUKA KWENYE KIBUBU

> Sherehe ya kugawana faida ktk Kikundi cha Imani imeingia doa baada ya baadhi yao kuzimia kutokana na taarifa ya upotevu wa zaidi ya Tsh. Milioni 39, zinazodaiwa kuyeyuka kwa njia ya kishirikina

> Fedha hizo zinadaiwa ziliyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa Mweka Hazina

Soma - https://jamii.app/UpotevuMil39Kikoba
KAKAMEGA, KENYA: KIJANA WA MIAKA 35 AMCHINJA MAMA YAKE. WALIKUWA WAKIGOMBEA UMILIKI WA MTI

- Kijana huyo anashikiliwa na Vyombo vya Dola kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano
-
Mashuhuda wamedai Kijana huyo ni muathirika wa Uraibu wa Bangi

Soma > https://jamii.app/KijanaAmchinjaMama
WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA UMEME (TANESCO) WATEULIWA

- Uteuzi huu wa wajumbe 8 wa Bodi hiyo umefanywa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani baada ya Rais Magufuli kumteua Dkt. Alexander Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi

Soma > https://jamii.app/BodiTANESCO
MICHEZO: BERNARDO SILVA AFUNGIWA KUCHEZA MCHEZO MMOJA KWA KUMBAGUA BENJAMIN MENDY

- Aliposti ujumbe wa kibaguzi dhidi ya Mendy kupitia Twitter

- Atalipa faini ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 147

- Ataukosa mchezo dhidi ya Chelsea Fc

Soma > https://jamii.app/SilvaVsMendy
WATANZANIA SITA WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MTO RUVUMA

> Watu 6 Raia wa Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 7 kujeruhiwa wakiwa katika Kisiwa cha Mto Ruvuma na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji

> Serikali imesema itahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao

Soma - https://jamii.app/Watz6WauawaRuvuma
KITABU GANI UMESOMA NA KIKABADILI MAISHA YAKO?

> Vitabu vina uwezo wa kubadili kabisa maisha ya mtu yeyote. Kuna wengi wamebadilishwa au kuboreshwa katika maisha yao kiafya, kijamii, kibiashara, kitaaluma, kimitazamo, kiimani, kimwili na mahusiano kupitia vitabu

> Kitabu gani ambacho kiligusa maisha yako au kukubadilisha na unatamani wenzako wajifunze pia. Je, kimekusaidiaje?

Soma - https://jamii.app/VitabuKubadiliMaisha
#JFHoja
SERIKALI: LAINI HAZITAFUNGWA KWASABABU YA KUKOSA USAJILI WA ALAMA ZA VIDOLE

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema ni maelekezo ya Rais Magufuli kwamba, hakuna Mtanzania atakayezuiwa kutumia laini yake ya simu kutokana na kukosa kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

> Hadi sasa zaidi ya laini milioni 20 zimesajiliwa

Soma - https://jamii.app/MatumiziLainiSimu
CHADEMA DODOMA: HATUTASUSIA TENA CHAGUZI ZIJAZO

> Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Dodoma kimesema hakitaendelea kujitoa katika chaguzi zinazofuata ikiwemo Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020, bali kinaanza kutafuta majibu ya changamoto zilizopo kupitia Wananchi na vikao vya chama

Soma - https://jamii.app/CDMDodomaKutosusaUchaguzi
ZIMBABWE YAANZA KUTUMIA NOTI MPYA

> Benki za Zimbabwe zimeanza kutoa Noti na Sarafu mpya zilizotolewa na Benki Kuu ya nchi hiyo (RBZ) ili kupunguza ukosefu wa sasa wa Pesa Taslim

> Watu walitarajia kuanza kupata pesa hizo kuanzia Jumatatu kutokana na tangazo la awali la Benki Kuu, lakini noti hizo hazikupatikana

Soma - https://jamii.app/MatumiziNotiMpyaZMW
DRC NA UGANDA ZAKUBALIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YAO ILI KURAHISISHA BIASHARA

> Rais Yoweri Museven na Rais Felix Tshisekedi wamebaini kuwapo kwa vizingiti vingi vya kibiashara kati ya Uganda na Congo ambavyo vimekuwa vinasababishwa na kuwapo kwa miundombinu mibovu inayounganisha nchi hizo

> Changamoto hiyo imesababisha nchi hizo kuagiza bidhaa nyigi kutoka China ilihali bidhaa hizo zinaweza kutengenezwa ndani ya nchi zao

Soma - https://jamii.app/MiundombinuBiasharaUGDRC
KAMBI YA UPINZANI INAKOSA NAFASI YA KUULIZA SWALI LA 1 KUTOKANA NA KIONGOZI WAKE KUTOKUWEPO BUNGENI

> Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Kambi ya Upinzani Bungeni inakosa nafasi ya kuuliza Swali la Kwanza kwa Waziri Mkuu kutokana na kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe kutokuwepo Bungeni mara kwa mara

> Asema, kama hujaja Bungeni na Spika hana taarifa zako wewe ni mtoro

Soma - https://jamii.app/UtoroMboweBungeni
BASATA YAMFUNGIA MSANII ROSA REE KWA MIEZI 6 KUTOKANA NA VIDEO YA VITAMIN U

> Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia Msanii huyo wa Bongofleva kutokana na Video ya Wimbo wa Vitamin U aliyoshirikishwa na Msanii Timmy Tdat kutoka Kenya

> Pia, limempiga faini ya Tsh. milioni 2 kwa kufanya kazi nje ya nchi bila idhini ya BASATA

Soma - https://jamii.app/BasataBanRosaRee
KUWAIT: BAADA YA MAANDAMANO MAKUBWA YA WANANCHI, WAZIRI MKUU AWATAKA MAWAZIRI WAJIUZULU

- Waziri Mkuu, Shaikh Jaber Mubarak amelazimika kufanya hivyo ili apate kibali cha kuunda Serikali Mpya

- Pia, anakwepa kutolewa madarakani na Wabunge

Soma > https://jamii.app/KuwaitGvtResigns
RWANDA: ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA VIJANA ASHITAKIWA KWA ULAGHAI

> Waziri wa Zamani wa Vijana, Michezo na Utamaduni, Robert Bayigamba amefikishwa Mahakamani kwa udanganyifu na kujipata mali ya mtu kwa njia za udanganyifu

> Upande wa Mashtaka umeomba aendelee kushikiliwa rumande kwani anaweza kukimbia kwasababu ana familia nje ya nchi

Soma - https://jamii.app/MashtakaUlaghaiWaziri