JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
- Azory Gwanda, alitoweka wakati akiendelea kuripoti yanayojiri Kibiti, Mkuranga na Ikwiriri

- Maeneo hayo kulikuwa na mauaji ya raia yaliyokuwa yakitekelezwa na Watu wasiojulikana

#EndImpunity #JFLeo
MICHEZO: Michezo saba ya Ligi Kuu Nchini England imemalizika kwa timu za Manchester City na Liverpool kuibuka na ushindi
-
Kwa matokeo hayo, Liverpool inaendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 31 huku Manchester City ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 25
UFARANSA: WAHAMIAJI 31 WAKAMATWA NDANI YA LORI

- Kufuatia uchunguzi wa kawaida uliofanywa na Polisi barabarani, Wahamiaji 31 waliokuwa nyuma ya lori pamoja na watoto ambao hawakuwa na mzazi ama mlezi walikamatwa jana Jumamosi

Zaidi, soma https://jamii.app/Wahamiaji31LoriUfaransa
SUDAN KUSINI: KAMANDA WA JESHI AWAPIGA NA STENDI YA KAMERA WANAHABARI WANAWAKE

- Wanahabari hao wamelalamikia kitendo hicho walichofanyiwa na Mkurugenzi wa Habari wa Jeshi

- Tukio hilo limeonekana ktk Kituo cha Televisheni cha Taifa

Soma > https://jamii.app/JeshiVsWanahabariSudan

#EndImpunity
RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MPYA

- Leo Novemba 3 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akichukua nafasi ya Prof Mussa Assad

- Prof. Assad aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete wakati wa utawala wake na kuapishwa Novemba 2014

Soma https://jamii.app/TeuziCAGKichere
RAIS MAGUFULI AMEAGIZA HALMASHAURI YA IFAKARA KUONGEZEWA KATA NA KILOMBERO KUBADILISHWA JINA

> Ifakara iongezewe idadi ya Kata kutoka Wilaya ya Kilombero na Makao Makuu yake yawe Ifakara

> Kilombero iitwe Mlimba na Makao Makuu yawe Mgeta

Soma > https://jamii.app/IfakaraKilomberoRais
ONGEZEKO LA JOTO MALAWI: MAHAKAMA YASITISHA UTARATIBU WA MAJAJI NA MAWAKILI KUVAA KOFIA

- Joto hufikia nyuzi 45 kwa baadhi ya maeneo ndani ya Malawi

- Wakili Chikosa Silungwe amesema joto limesababisha kazi kuwa ngumu Mahakamani

Soma > https://jamii.app/MalawiJudgesWigs
HAKI ZA MTEJA: MWANASHERIA APANIA KUYASHTAKI MAKAMPUNI 4 YA MAWASILIANO

> Mwanasheria, Mwanachama wa JamiiForums Bashir Yakub analalamikia utaratibu wa kuisha vifurushi pamoja na kuchanganywa kwa vifurushi na muda wa kawaida

Habari zaidi, soma > https://jamii.app/KampuniSimuKushtakiwa
MTATIRO: NILIKUWA KIONGOZI CUF HUKU NIKIAMINI CCM NDIO BORA

- DC wa Tunduru, Julius Mtatiro amesema kwa miaka yote aliyokuwa CUF aliamini CCM ndiyo chama bora

- Amesema ameachana na madai ya mabadiliko ya Katiba na kujikita kwenye maendeleo

Zaidi, soma https://jamii.app/Mtatiro-CCMBora
JE, UNAFAHAMU NINI MAANA YA KATIBA NA UMUHIMU WAKE?

> Katiba ni mpangilio wa sheria zilizoandikwa au zisizoandikwa zinazotumika kuongoza Nchi, Taasisi au Kikundi

> Nchi zote zinahitaji Katiba ili ziweze kujiendesha vizuri. Nchi isiyo na katiba inaweza kuingia kwenye machafuko

Zaidi, soma > https://jamii.app/UmuhimuKatiba

#UmuhimuKatiba
MAREKANI: DENI LA TAIFA LAZIDI KUONGEZEKA, NI SAWA NA KILA RAIA ANADAIWE ZAIDI YA TSH. MILIONI 160

> Taarifa ya Wizara ya Hazina inasema deni la ndani limeongezeka hadi kufikia Dola Trilioni 23 ambapo Dola Trilioni 17 ni madeni kutoka kwa raia na taasisi za fedha huku Dola Trilioni 6 ni deni kutoka mashirika ya Serikali.

Soma - https://jamii.app/IncreaseUSNationalDebt
MTIHANI YA TAIFA KWA KIDATO CHA 4 WAANZA LEO, WATAHINIWA 485,866 WASAJILIWA

> Jumla ya watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2019 na kati yao wa shule ni 433,052 na 52,814 wa kujitegemea

> Kati ya watahiniwa hao wavulana ni 206,420 sawa na asilimia 47.67 na wasichana 226,632 sawa na asilimia 52.33 huku wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa 842

Soma - https://jamii.app/MtihaniTaifaKidato4
IKULU: RAIS MAGUFULI KUWAAPISHA VIONGOZI WATEULE WAKIWEMO MAJAJI WA MAHAKAMA KUU

- Rais Magufuli anatarajiwa kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua

- Charles Kichere aliyeteuliwa kuwa CAG wa 6 wa Tanzania tangu nchi ipate uhuru, ataapishwa

Zaidi, soma https://jamii.app/UapishajiCAGKichere
MICHEZO: Beki wa Klabu ya mpira ya Simba, Shomari Kapombe ametangaza rasmi kuhusu uamuzi wake wa kuandika barua ya kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
-
Kapombe ametangaza kufikia uamuzi huo baada ya kutathmini afya yake, kwani anadai Taifa Stars inahitaji wachezaji watakaokuwa vizuri kiafya kwa asilimia 100 na upande wake haoni kama anaweza kujitoa kwa asilimia 100 kwa kuwa amekuwa akikumbwa na majeraha
-
Hata hivyo ameomba aendelee kuitumikia Timu yake ya Simba ambayo haina mashindano mengi ya Ligi
IKULU: Charles Kichere akiapa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad aliyekuwa CAG kwa miaka mitano

- CAG Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe na awali alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA

Fuatilia https://jamii.app/UapishajiCAGKichere
UMUHIMU WA KATIBA: #Katiba huainisha jinsi Raia wake wanaweza kupigania haki zao za Kibinadamu.

- Kwa hivyo #Katiba ni nyenzo muhimu sana ambayo husaidia kuzuia unyanyasaji na uvunjifu wa wa Haki za Binadamu

- #Katiba bora ni mlinzi wa Haki na Usawa ndani ya Taifa. Katiba inaweka na kuzitambulisha Haki za Watu wa Nchi yake

Soma > https://jamii.app/UmuhimuKatiba
TETESI: WACHEZAJI WA ARSENAL WACHOSHWA NA MBINU ZA KOCHA WAO

- Inadaiwa Kocha wa Arsenal, Unai Emery anajaribu kuokoa kazi yake huku Wachezaji wakiwa na wasiwasi juu ya mbinu za Kocha huyo

- Inadaiwa idadi kubwa ya Wachezaji hawaridhishwi na mbinu za Kocha huyo na kudai hataki kubadilika
PROF. ASSAD: SIWEZI KUSEMA CHOCHOTE JUU YA UTEUZI WA CAG MPYA, SIJAPATA TAARIFA RASMI

> Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amesema alipoteuliwa alipewa barua ya uteuzi iliyoeleza mambo kadhaa ya kisheria na vifungu vya kisheria kuhusu uteuzi wake, lakini utenguzi huu umekuja bila taarifa hivyo anaendelea kusubiri huenda akapelekewa barua

Soma - https://jamii.app/ProfAssadUteuziCAG
IKULU: Maneno ya Rais Magufuli kwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere wakati akimuapisha kutumikia Wadhifa huo katika hafla iliyofanyika leo Novemba 04, 2019

Zaidi, tembelea https://jamii.app/UapishajiCAGKichere