JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAONI YA WANANCHI: Raia wa Tanzania na Kenya wanasema Uhuru wa Vyombo vya Habari ni nyenzo nzuri ya Demokrasia

- Watanzania na Waganda, wanaamini wana haki ya kuwakosoa viongozi wao lakini mara zote wameshindwa kutumia haki hii

Zaidi, soma > https://jamii.app/UhuruHabari
#EndImpunity
WANAHABARI WATANZANIA WALIOFARIKI NA KUPATA MISUKOSUKO WAKIWA KAZINI

- Stanley Katabalo, alikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mfanyakazi, aliibua kashfa ya Pori Tengefu la Loliondo

- Yadaiwa, habari hizi zilimgharimu maisha yake

Soma > https://jamii.app/KumbukumbuWanahabari

#EndImpunity
- Daudi Mwangosi, alikuwa Mwandishi wa "Channel Ten', alifariki kwa kulipuliwa na Bomu la Machozi

> Alikuwa Nyololo, Iringa akiripoti kuhusu Mkutano wa CHADEMA

#EndImpunity #JFLeo
- Adam Mwaibabile maarufu 'Mwana' huyu aliwahi kuwekwa rumande na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Nicodemus Banduka kwa kukutwa na nyaraka za Serikali zenye Muhuri wa 'SIRI'

#EndImpunity #JFLeo
- Azory Gwanda, alitoweka wakati akiendelea kuripoti yanayojiri Kibiti, Mkuranga na Ikwiriri

- Maeneo hayo kulikuwa na mauaji ya raia yaliyokuwa yakitekelezwa na Watu wasiojulikana

#EndImpunity #JFLeo
SUDAN KUSINI: KAMANDA WA JESHI AWAPIGA NA STENDI YA KAMERA WANAHABARI WANAWAKE

- Wanahabari hao wamelalamikia kitendo hicho walichofanyiwa na Mkurugenzi wa Habari wa Jeshi

- Tukio hilo limeonekana ktk Kituo cha Televisheni cha Taifa

Soma > https://jamii.app/JeshiVsWanahabariSudan

#EndImpunity
MCT: WANAHABARI 23 WALIKUMBWA NA MIKASA WAKITEKELEZA MAJUKUMU

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2021, Wanahabari 23 Nchini walikumba na mikasa mbalimbali wakati wakitimiza majukumu yao

Soma https://jamii.app/WaandishiTz
#EndImpunity
Maadhimisho ya Siku ya Kukomesha Ukatili Kwa Wanahabari ni Muhimu kutokana na Sekta ya #Habari kuwa moja ya Nguzo muhimu za kuimarisha #Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji, ambavyo ni vigezo muhimu katika Maendeleo ya Nchi

Soma https://jamii.app/EndImpunity2022

#EndImpunity
Utafiti wa UNESCO unaonesha asilimia 73% ya Waandishi Wanawake wamekuwa wakikabiliwa na madhila mbalimbali ikiwemo Kudhalilishwa, Kuonewa, Kushambuliwa, Vitisho vya Kuhatarisha Usalama wao na hata Kuuawa wakiwa Kazini

Soma https://jamii.app/EndImpunity2022

#EndImpunity
👍3🥰1
Takwimu za Dunia zinaonesha katika Miaka 5 iliyopita ni asilimia 13% tu ya Kesi za Madhila dhidi ya Wanahabari, ikiwamo Mauaji, ndizo zilizoshughulikiwa huku asilimia kubwa ya Kesi hizo zikiwa bado hazijapatiwa ufumbuzi

Soma https://jamii.app/EndImpunity2022

#EndImpunity
👍6