JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAZIRI JAFO: WATENDAJI WASIFUNGE OFISI LEO ILI WATU WOTE WALIOCHUKUA FOMU WAZIREJESHE

> Waziri wa TAMISEMI amepiga marufuku kwa Mtendaji katika eneo lolote nchini kufunga ofisi kabla wagombea watarajiwa wa Uchaguzi Serikali za Mitaa hawajarejesha fomu zao labda kama mgombea huyo atakuja baada ya saa 10 jioni

> Amesema, baada ya hapo hawataongeza muda wa kuchukua fomu, hivyo wananchi watumie vizuri muda uliobaki

Soma - https://jamii.app/OfisiWatendajiFomuUchaguzi
MSUMBIJI: TUME YA UCHAGUZI YAKIRI KULIKUWA NA DOSARI KWENYE UCHAGUZI MKUU

> Tume ya Uchaguzi imekiri kuwa kuliwepo na dosari kadhaa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 15, ambapo Rais Filipe Nyusi alichaguliwa kwa Muhula wa Pili

> Ni baada ya Chama Kikuu cha Upinzani (RENAMO) kufungua kesi wiki iliyopita katika Mahakama ya Katiba kupinga ushindi wa Rais Nyusi, kikitaka uchaguzi huo ufutwe

Soma - https://jamii.app/MassiveElectoralFraud
DR CONGO: MWANAHABARI ALIYEKUWA AKIHAMASISHA MAPAMBANO DHIDI YA EBOLA AUAWA

- Papy Mumbere Mahamba ameuawa na mkewe kujeruhiwa huku nyumba yao ikichomwa moto

- Chanzo hakijafahamika bado na Mamlaka zinachunguza kujua kama kinahusiana na kazi yake

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanahabariEbolaAuawa-DRC
TABORA: AFARIKI BAADA YA KUNYANG'ANYWA HIRIZI NA POLISI WAKATI WA UPEKUZI

> Michael Paschal (33), dereva bodaboda anadaiwa kupoteza maisha baada ya kuporwa hirizi zake na Polisi wakati akifanyiwa upekuzi baada ya kumkaba na kumchania sare Askari aliyekuwa katika majukumu ya usalama barabarani

Soma - https://jamii.app/KifoKuporwaHirizi
DODOMA: WABUNGE WAPATIWA 'TABLETS'

- Wabunge wote wa Tanzania wapewa 'tablets' kwa ajili ya kuwasaidia katika matumizi ya shughuli za Bunge

- Wamegawiwa vifaa hivyo leo, siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 17, lengo likiwa ni kuondoa matumizi ya karatasi Bungeni
ALIYEMTISHA MWENZAKE KWA BASTOLA AFIKISHWA MAHAKAMANI

- Shabani Hamisi ambaye ni mume wa Mtangazaji Zamaradi Mketema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni

- Ilisambaa video ikimuonesha akimtisha kwa bastola Venance John

Zaidi, soma https://jamii.app/MumeZamaradiKizimbani
MICHEZO: Mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) kati ya Mawenzi Market na Geita Gold ulilazimika kusimama baada ya Mwamuzi Msaidizi, Abdalah Uhako kupokea kipigo na kushindwa kuendelea na mchezo huo kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro
-
Tukio hilo lilitokea dakika chache kabla ya mapumziko baada ya wachezaji na mashabiki wa Mawenzi Market kupandwa na hasira zinazodaiwa kusababishwa na uamuzi wa mwamuzi wa kati, Mussa Gabriel na Abdallah Uhako kukataa bao lao katika dakika ya 39
-
Abdallah Uhako alipatiwa huduma ya kwanza na baadaye kukimbizwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi ambako amelazwa
HATUA 5 ZA KUFUATA ILI KUTATUA TATIZO UNALOPITIA KWENYE MAISHA

> Hatua ya kwanza ni kujua kwa undani tatizo ni nini. Watu wengi huangalia madhara ya tatizo, badala ya kuangalia chanzo cha tatizo. Kujua chanzo ni nusu ya kutatua tatizo hilo

> Baada ya kujua tatizo, anza kuorodhesha kila hatua unayoweza kuchukua. Andika kila suluhisho linalowezekana kwenye tatizo ulilonalo

> Baada ya kuorodhesha hatua zote, anza kuandika faida na hasara za kila suluhisho uliloliona linafaa. Andika kila kitu ambacho unakifikiria kuhusu suluhisho husika

> Ukishajua faida na hasara, sasa chagua suluhisho lenye faida kubwa/nzuri na hasara kidogo. Hakikisha unaweza kusimamia suluhisho hilo bila ya kutetereka na kuweza kulitetea kwa wengine

> Ukishachukua hatua siyo mwisho, bali unahitaji kuwa unafanya mapitio na tathmini ya ile hatua uliyochagua. Angalia kama inaleta matokeo ambayo ulitarajia kupata?

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HatuaKutatuaTatizo
#JFMaisha
UMOJA WA MATAIFA WATOA MSAADA SOMALIA BAADA YA MVUA KULETA MADHARA

> Misaada hiyo imetumwa hasa katika Wilaya ya Beletweyne ambapo taarifa zinasema watu zaidi ya 270,000 wameachwa bila makazi baada ya nyumba zao kuharibika katika mafuriko

> Mvua kubwa na mafuriko yameendelea kuzikumba Somalia, Sudan Kusini na Kenya mwaka huu na Watabiri wa Hali ya Hewa wanatarajia mvua hizo kubwa zitaendelea kunyesha hadi Desemba

Soma - https://jamii.app/UNCharityFloodsSomalia
UGANDA: POLISI YAWATAWANYA NA KUKAMATA BAADHI YA WAANDISHI

- Polisi imetumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wanahabari wapatao 50 waliokuwa wanaandamana kuelekea Makao Mkuu ya Polisi kuwasilisha kero zao juu ya ukatili wa Polisi dhidi yao

Zaidi, soma https://jamii.app/UkatiliPolisi-Wanahabari
KWANINI KATIBA NI MUHIMU?: Katiba ni kichocheo cha Serikali Bora, pia inashughulika na mapungufu yanayoweza kujitokeza kwenye uongozi

> #Katiba imeundwa kwa minajili ya kuzuia utumiaji wa mabavu wakati wa maamuzi ya watumishi wa Serikali na wa Sekta Binafsi

#UmuhimuKatiba
NIGERIA: WANAJESHI 3 MBARONI KWA UTEKAJI NA UNYANG'ANYI

- Wanajeshi hao na raia mmoja wamekamatwa ktk maeneo ya Edo na sasa wanahojiwa

- Watuhumiwa ni Koplo Collins Ameh, Koplo Balogun Taiwo na Private Evans Isibor na raia Goodluck Igbenebor

Zaidi, soma https://jamii.app/WanajeshiRaiaMbaroni-KE
UN: MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAONGEZEKA AFRIKA HUKU VIJANA WAKIATHIRIKA ZAIDI

> Ripoti mpya ya Ofisi ya Kupambana na Mihadarati ya Umoja wa Mataifa imesema matumizi ya #DawaZaKulevya yameongezeka mara 10 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 Magharibi mwa Afrika

> Asilimia 18 ya watu wanaopewa huduma za kuachana na Dawa hizo wana umri kati ya miaka 10 hadi 19

Soma - https://jamii.app/OngezekoMatumiziMihadarati
CAG CHARLES KICHERE AKABIDHIWA OFISI NA MTANGULIZI WAKE, PROF. ASSAD

- Prof. Assad ameomba wote aliowakosea wamsamehe na yeye amesamehe

- CAG Kichere amesema kama kulikuwa na mahusiano hafifu kati ya Ofisi ya CAG na Bunge atayaimarisha

Soma https://jamii.app/AssadAkabidhiOfisi
JAJI MKUU KENYA: NAPANGIWA NJAMA ZA KUONDOLEWA MADARAKANI

- David Maraga ametishia kujiuzulu kufuatia kukatwa kwa bajeti ya Mahakama akidai inalenga kuidhibiti Mahakama

- Amedai ni njama za Serikali kumuondoa madarakani kabla ya Desemba 31

Soma https://jamii.app/MalalamikoJajiMkuu-KE
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Prof. Assad akiondoka baada ya kukabidhi ofisi kwa CAG mpya, Charles Kichere leo jijini Dar

> Prof. Assad amemaliza kipindi chake kimoja akihudumu kama CAG na ameondoka huku ukiibuka mjadala mkali juu ya kuondoka kwake
MKWASSA KUINOA YANGA

> Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amemtangaza Charles Boniface Mkwassa kuwa kocha wa muda wa Yanga akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera kwa muda wa wiki mbili

Zaidi, soma https://jamii.app/MkwasaKochaYanga
MAHAKAMA YAIGOMEA SERIKALI

> Mahakama ya Kisutu imetupilia mbali maombi yaliyotolewa na upande wa Serikali kutaka kuwaondolea shtaka la Utakatishaji Fedha aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange

Zaidi, soma https://jamii.app/NyangeAvevaDhamana