JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
LEO NI SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAHABARI DUNIANI

- Ripoti ya Kamati ya Kuwalinda Wanahabari Ulimwenguni(CPJ) imeeleza kuwa Mataifa 13 yamekumbwa na visa vya mauaji ya kikatili dhidi ya Wanahabari

- Mauaji haya yanatekelezwa na vikundi vya uhalifu, viongozi wa kisiasa, na Wafanyabiashara kwa lengo la kuficha uovu wao

Zaidi, soma https://jamii.app/CPJVsImpunity
MAKONDA APIGA MARUFUKU KAMPUNI YA NYANZA KUPEWA MRADI DAR

- RC Makonda aipiga marufuku TANROADS kuipa mradi Kampuni hiyo ya Ujenzi ndani ya mkoa wa Dar

- Ni baada ya Kampuni hiyo kutumia miezi 12 kujenga Barabara ya Km 3.2 ya Kitunda-Kivule

Zaidi, soma https://jamii.app/NyanzaMradiDar
MALI: WANAJESHI 35 WAFARIKI BAADA YA KAMBI YA JESHI KUSHAMBULIWA

- Wameuawa katika shambulio lililotokea jana kwenye Kambi ya Jeshi huko Indelimane

- Al-Qaeda na makundi yanayoshirikiana na kundi la Dola la Kiislamu yanahusishwa na shambulio

Zaidi, soma https://jamii.app/Wanajeshi35Wauawa-Mali
MAONI YA WANANCHI SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKATILI KWA WANAHABARI

- Watanzania wanasema wenye madaraka huwashawishi Polisi wawanyamazishe Wanahabari

- Raia wa Afrika Mashariki wanaunga mkono Uhuru wa Habari kuliko Udhibiti wa Serikali

Soma > https://jamii.app/UhuruHabari

#JFLeo
MAONI YA WANANCHI: Raia wa Tanzania na Kenya wanasema Uhuru wa Vyombo vya Habari ni nyenzo nzuri ya Demokrasia

- Watanzania na Waganda, wanaamini wana haki ya kuwakosoa viongozi wao lakini mara zote wameshindwa kutumia haki hii

Zaidi, soma > https://jamii.app/UhuruHabari
#EndImpunity
AFRIKA KUSINI MABINGWA WA MICHUANO YA DUNIA YA RUGBY

- South Africa imefanikiwa kunyakua taji la Dunia la Rugby kwa kuifunga England katika mchezo wa fainali kwa alama 32-12

- Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12, Nchi hiyo kuchukua taji hilo
BAKWATA: MAADHIMISHO YA MAULID KUFANYIKA NOVEMBA 09

- BAKWATA imetangaza kuwa Novemba 09, 2019 yatafanyika maadhimisho ya Kitaifa ya Maulid jijini Mwanza

- Baraza la Maulid litafanyika Novemba 10, katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Capripoint

Zaidi, soma https://jamii.app/Maulid2019
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: JENGO MOJA LATEKETEA KWA MOTO

- Ghorofa moja lililopo Kariakoo, Mtaa Livingstone na Mkunguni linawaka moto huku chanzo kikiwa hakijajulikana bado

- Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kimeshawasili na juhudi za kuuzima moto zinaendelea

Zaidi, soma https://jamii.app/MotoGhorofaKKoo
MICHEZO: Klabu ya Manchester United ikiwa ugenini katika uwanja wa Vitality imefungwa goli 1-0 na Klabu ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu England, Mzunguko wa 11

- Kwa matokeo hayo, Bournemouth ipo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi ikiwa na alama 16 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 8 na alama 13
WANAHABARI WATANZANIA WALIOFARIKI NA KUPATA MISUKOSUKO WAKIWA KAZINI

- Stanley Katabalo, alikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mfanyakazi, aliibua kashfa ya Pori Tengefu la Loliondo

- Yadaiwa, habari hizi zilimgharimu maisha yake

Soma > https://jamii.app/KumbukumbuWanahabari

#EndImpunity
- Daudi Mwangosi, alikuwa Mwandishi wa "Channel Ten', alifariki kwa kulipuliwa na Bomu la Machozi

> Alikuwa Nyololo, Iringa akiripoti kuhusu Mkutano wa CHADEMA

#EndImpunity #JFLeo
- Adam Mwaibabile maarufu 'Mwana' huyu aliwahi kuwekwa rumande na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Nicodemus Banduka kwa kukutwa na nyaraka za Serikali zenye Muhuri wa 'SIRI'

#EndImpunity #JFLeo
- Azory Gwanda, alitoweka wakati akiendelea kuripoti yanayojiri Kibiti, Mkuranga na Ikwiriri

- Maeneo hayo kulikuwa na mauaji ya raia yaliyokuwa yakitekelezwa na Watu wasiojulikana

#EndImpunity #JFLeo
MICHEZO: Michezo saba ya Ligi Kuu Nchini England imemalizika kwa timu za Manchester City na Liverpool kuibuka na ushindi
-
Kwa matokeo hayo, Liverpool inaendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 31 huku Manchester City ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa na alama 25
UFARANSA: WAHAMIAJI 31 WAKAMATWA NDANI YA LORI

- Kufuatia uchunguzi wa kawaida uliofanywa na Polisi barabarani, Wahamiaji 31 waliokuwa nyuma ya lori pamoja na watoto ambao hawakuwa na mzazi ama mlezi walikamatwa jana Jumamosi

Zaidi, soma https://jamii.app/Wahamiaji31LoriUfaransa
SUDAN KUSINI: KAMANDA WA JESHI AWAPIGA NA STENDI YA KAMERA WANAHABARI WANAWAKE

- Wanahabari hao wamelalamikia kitendo hicho walichofanyiwa na Mkurugenzi wa Habari wa Jeshi

- Tukio hilo limeonekana ktk Kituo cha Televisheni cha Taifa

Soma > https://jamii.app/JeshiVsWanahabariSudan

#EndImpunity
RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MPYA

- Leo Novemba 3 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akichukua nafasi ya Prof Mussa Assad

- Prof. Assad aliteuliwa na Rais Mstaafu Kikwete wakati wa utawala wake na kuapishwa Novemba 2014

Soma https://jamii.app/TeuziCAGKichere
RAIS MAGUFULI AMEAGIZA HALMASHAURI YA IFAKARA KUONGEZEWA KATA NA KILOMBERO KUBADILISHWA JINA

> Ifakara iongezewe idadi ya Kata kutoka Wilaya ya Kilombero na Makao Makuu yake yawe Ifakara

> Kilombero iitwe Mlimba na Makao Makuu yawe Mgeta

Soma > https://jamii.app/IfakaraKilomberoRais
ONGEZEKO LA JOTO MALAWI: MAHAKAMA YASITISHA UTARATIBU WA MAJAJI NA MAWAKILI KUVAA KOFIA

- Joto hufikia nyuzi 45 kwa baadhi ya maeneo ndani ya Malawi

- Wakili Chikosa Silungwe amesema joto limesababisha kazi kuwa ngumu Mahakamani

Soma > https://jamii.app/MalawiJudgesWigs