JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: WANASAYANSI WAFANIKIWA KUONDOA VVU KWA PANYA

> Watafiti nchini Marekani wamesema wamefanikiwa kuondoa Virusi Vya Ukimwi kutoka kwenye vinasaba (DNA) vya panya 9 kati ya 23

> Kutokana na mafanikio hayo endapo mamlaka za chakula na dawa zitathibitisha tiba hiyo kwa binadamu inaweza kuanza kutumika mapema mwaka ujao

Soma - https://jamii.app/TibaVVUPanya
MICHEZO: Timu ya Taifa ya #Nigeria yafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka timu ya Taifa ya #Cameroon kwa mabao 3 kwa 2

#AFCON2019 #JFLeo
Mchezo wa #AFCON2019 kati ya #Misri na #SouthAfrika maarufu kama #Bafanabafana umekwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 0 kwa 0

> Je, unaweza kubashiri timu gani itaibuka na ushindi katika kipindi cha pili?
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #SouthAfrica maarufu ‘#Bafanabafana’ imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Egypt goli 1-0

- Katika hatua ya robo fainali, South Africa itakutana na #Nigeria iliyofanikiwa kuitoa #Cameroon

#JFLeo #EGYRSA
#CopaAmerica2019: #Argentina imeibuka mshindi wa tatu katika michuano hiyo baada ya kuifunga #Chile goli 2-1

> Katika mchezo huo, Lionel Messi wa Argentina na Gary Medel wa Chile walipewa kadi nyekundu

> Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kati ya #Brazil na #Peru mida ya saa 5 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki
MSAIDIZI WA MEMBE, ALLAN KILUVYA ANADAIWA KUTEKWA NA WATU ‘WASIOJULIKANA’

> Taarifa kwa kina zinafuata...
MSUMBIJI: IS IMEKIRI KUHUSIKA KWENYE SHAMBULIO LILILOUA WATU 7

- Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumatano kwenye kijiji cha Lidjungo huko Nangade

- Hii ni mara ya pili kwa kikundi hicho kukiri kuhusika kwenye mashambulio Nchini humo

Soma https://jamii.app/ISAttackInMoz
#JFLeo
RAIS MAGUFULI AMZAWADIA TAUSI RAIS KENYATTA

- Amemzawadia Tausi wanne kama kumbukumbu ya Uhusiano, Urafiki na Ujirani mwema baina ya Nchi hizo mbili

- Rais Kenyatta alifika wilayani Chato Julai 5, kwaajili ya ziara binafsi ya siku 2

Soma https://jamii.app/KenyattaApewaTausi
#JFLeo
WAZIRI LUGOLA ARUHUSU MABASI YA ABIRIA KUSAFIRI SAA 24

- Amewataka makamanda wa Polisi kutozuia mabasi kwa kisingizio cha kuhofia majambazi

- Amesisitiza mabasi yanayotoka Kanda ya Ziwa kutozuiwa Morogoro na yanayotoka Dar kutozuiwa Shinyanga

Soma https://jamii.app/MabasiKusafiriSaa24
#JFLeo
Mchezo wa #AFCON2019 kati ya #Madagascar na #DR Congo umekwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 1 kwa 1

> Je, unaweza kubashiri timu gani itaibuka na ushindi katika kipindi cha pili?
FIFAWWC: Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya USA imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwenye mchuano ya Kombe la dunia kwa kuifunga Netherland goli 2-0

- Marekani inachukua Kombe hilo mara ya 4 sasa na kuwa timu iliyochukua Kombe hilo mara nyingi zaidi
IRAN KUVUNJA MKATABA WA NYUKLIA

- Imesema itaanza kuvunja mkataba huo na kupunguza uzingatiaji wake baada ya kila siku 60

- Itafanya hivyo iwapo mataifa yaliyosaini mkataba huo hayatachukua hatua za kuilinda dhidi ya vikwazo vya Trump

Soma https://jamii.app/IranKurutubishaUranium
INDIA: WATU 29 WAFARIKI NA ZAIDI YA 20 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI

- Ajali hiyo imetokea leo asubuhi ambapo basi hilo limepinduka karibu na mji wa Agra, Kaskazini mwa India

- Inadaiwa dereva wa basi hilo la ghorofa moja alikuwa amesinzia

Soma https://jamii.app/BusCrashKills29-India
DKT. BASHIRU: JIMBO LA HAI SI NGOME YA CHADEMA

- Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema hayo jana wakati akieleza sababu ya ziara yake Mkoani Kilimanjaro

- Amesema katika ziara yake ameanzia Hai kimkakati na mahesabu yametumika kuamua

Soma https://jamii.app/BashiruJimboMbowe
MCHEZAJI WA AJAX, MATTHIJS DE LIGT KUJIUNGA NA JUVENTUS

- Meneja wake, Mino Raiola amethibitisha kuwa beki huyo raia wa Uholanzi amefikia makubaliano binafsi na klabu ya Juventus

- Inaaminika kuwa De Ligt amekubali malipo ya Paundi 230,000(Tsh. 661,958,247) kwa wiki
SINGIDA: WATU 7 WAKIWEMO WAFANYAKAZI 5 WA AZAM TV WAFARIKI AJALINI

- Wafanyakazi wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea wakati wakielekea Chato mkoani Geita

- Ni baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na Lori

Zaidi, soma https://jamii.app/WafanyakaziAzamWafarikiAjalini