JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHAMIMU NA MUMEWE WARUDISHWA RUMANDE, MAHAKAMA BADO INASUBIRI RIPOTI YA MKEMIA MKUU

- Jamhuri imesema inasubiri majibu ya ripoti hiyo ili iwasilishe kama kielelezo Mahakamani hapo

- Kesi imeahirishwa hadi Julai 22, 2019 kwa ajili ya kutajwa

Zaidi, soma https://jamii.app/ShamimuMumeweWasotaRumande
LIGI KUU BARA 2019/20 KUANZA AGOSTI 23. SIMBA NA YANGA KUKUTANA JANUARI 04, 2020

- Pazia la ligi hiyo litafunguliwa kwa mchezo mmoja kati ya Simba SC na JKT Tanzania

- Bodi ya Ligi nchini imesema Msimu huu imezingatia ratiba za Kimataifa

Zaidi, soma https://jamii.app/LigiKuuBara2019-20
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars”, Emmanuel Amunike wafikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba baina yao

> TFF imesema itatangaza Kocha wa muda atakayekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN
THE HAGUE: ALIYEKUWA KIONGOZI WA WAASI CONGO, BOSCO NTAGANDA ATIWA HATIANI

- Ni kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita wa mwaka 2002 na 2003 katika eneo la Ituri

- Ntaganda(45) maarufu ''Terminator'' anakabiliwa na kifungo cha maisha

Ziadi, soma https://jamii.app/BoscoNtagandaAtiwaHatianiICC
MAHUSIANO: Mtoa mada ndani ya JamiiForums anawashauri Wanaume kwamba “unapotaka kuoa hakikisha unaoa Mwanamke ambaye unamzidi Elimu, Kipato na Mali kwa wakati huo”

- Anasema kuwa kuoa Mwanamke aliyekuzidi vitu hivyo utateseka kwenye ndoa na maisha yako yatakuwa mafupi kwani utakufa kwa msongo wa mawazo

Je, una maoni gani kuhusu suala hili?

Kutoa maoni, Tembelea > https://jamii.app/MwanamkeVsKipato
FAMILIA YA ALLAN KILUVYA, ANAYEDAIWA KUTEKWA YAJITOKEZA KUOMBA MSAADA

- Imeomba msaada kwa Rais Magufuli, Serikali na Watanzania kusaidia kumpata ndugu yao

- Imedai gari lililomteka ni Land Cruiser lenye namba T 810 BQS, rangi ya kijivu

Zaidi, soma https://jamii.app/FamiliaAllanYaombaMsaadaKumtafuta
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Mali katika mchezo wa hatua ya mtoano

- Ivory Coast imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano na sasa itapambana na Algeria iliyoitoa Guinea
MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.2 NDANI YA MWEZI

- Umeongezeka hadi asilimia 3.7 kwa mwezi Juni kutoka asilimia 3.5 kwa mwezi Mei, 2019

- Hali hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Juni imeongezeka

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBeiWaongezeka-Juni2019
HANDENI, TANGA: MBARONI KWA KUMCHINJA MKEWE

- Juma Hemedi(45) mkazi wa Kwamaraho, anashikiliwa na polisi kwa kumuua mkewe Amina Hussein(38)

- Kamanda Bukombe amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na amesema polisi inaendelea na uchunguzi

Soma https://jamii.app/AmchinjaMkewe
MIILI YA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM MEDIA GROUP YAAGWA

- Miili ya Wafanyakazi hao waliofariki jana inaagwa leo katika ofisi za Azam Media zilizopo Tabata jijini Dar

- Viongozi kadhaa wamehudhuria akiwemo Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe

Zaidi, soma https://jamii.app/WafanyakaziAzamWaagwa
Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi-Chato unaofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita ambapo Rais Magufuli ni mgeni rasmi
KATIBU MKUU CCM AMUONYA WAZIRI WA VIWANDA

- Dkt. Bashiru Ally amesema Waziri Innocent Bashungwa atatumbuliwa ikiwa atashindwa kutizima azma ya Serikali ya kufufua viwanda

- Amehoji “Barabara zinajengwa unaziona, SGR unaiona, kwa nini hatuoni viwanda vinafufuliwa?”

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruAmuonyaWaziriViwanda
IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU

- Imesema Uingereza kukamata meli yao ya mafuta iitwayo Grace 1, nje ya eneo la Gibraltar hakutapita bila majibu

- Ilikamatwa Alhamisi ikishutumiwa kuvunja vikwazo kwa kupeleka mafuta Syria

Zaidi, soma https://jamii.app/IranKisasiUK
RAIS MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA BURIGI-CHATO, AMPONGEZA FARU RAJABU

- Amempongeza Faru huyo kwa kuzalisha Watoto 40 na hivyo kuongeza idadi ya Faru

- Aidha, amesema “Nadhani wajina wangu John(baba wa Faru Rajabu) alikuwa hajitumi vizuri”

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAmpongezaFaruRajabu
KENYA: MZEE WA MIAKA 60 MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 9

> Tukio hilo limetokea wakati wakiwa kwenye usafiri maarufu kama ‘Matatu’

> Mtoto alizimia, alipoamka alisimulia kisa hicho

> Mtoto anafanyiwa uchunguzi Kituo cha Afya Kiganjo

Soma https://jamii.app/MzeeMbaroniKwaUnyanyasaji
PSG: NEYMAR ANAWEZA KUONDOKA IWAPO OFA YA KUNUFAISHA PANDE ZOTE ITAPATIKANA

- Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu ya Paris St-Germain(#PSG), Leonardo ameongeza kuwa hawajapokea ofa yoyote kwa ajili ya #Neymar ila kulikuwa na mawasiliano madogo sana na Barcelona
MSAIDIZI WA BERNARD MEMBE, ANAYEDAIWA KUTEKWA APATIKANA

- Allan Kiluvya amepatikana baada ya kuachwa na wanaodaiwa kuwa watekaji katika eneo la Njia Panda ya Segerea

- Amesema hapo palikuwa sehemu salama kwani aliweza kupata usafiri na kuwa Watu hao walimuacha hapo baada ya kumuuliza wapi wamuache

Zaidi, soma https://jamii.app/AllanApatikanaNjiaSegerea
XABI ALONSO AJITOSA KWENYE UKOCHA

- Mchezaji huyo wa zamani aliyewika katika vilabu vya Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich amekubali kuinoa timu ya Real Sociedad B

- Miaka 20 iliyopita, Alonso alianza kucheza soka la kulipwa katika Klabu hiyo ya Uhispania
WAZIRI KALEMANI: CHATO ITAKUWA MIONGONI MWA MAJIJI MAKUBWA

- Amewataka Wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kwenda kuwekeza katika Wilaya hiyo akisema kuna fursa

- Amesema licha ya Hifadhi iliyozinduliwa leo pia kuna madini na Ziwa Victoria

Zaidi, soma https://jamii.app/WilayaChatoJiji
UBALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA KUTOSHUGHULIKIA MASUALA YA ‘VISA’

- Kuanzia Agosti 01, 2019 maombi ya ‘visa’ za safari au Makazi kwa Watanzania wanaotaka kwenda Norway, yatatumwa na kushughulikiwa katika Ubalozi wa Norway uliopo Nairobi

Zaidi, soma https://jamii.app/NorwegianVisa-Nairobi