JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NEMC: KELELE ZA VIWANDA, NGOMA, MUZIKI, IBADA KUANZA KULIPIWA. WATAKAOKIUKA KUTOZWA FAINI

> NEMC imesema kwa Mtu atakayetaka kufanya shughuli hizo atapaswa kulipa milioni 10

> Watakaokiuka watatozwa faini isiyozidi milioni 50 ama kifungo jela

Soma > https://jamii.app/NEMCVsKelele
Mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya #Cameroon na #Nigeria umeenda mapumziko kwa #Cameroon kuongoza kwa magoli 2 kwa 1

> Je, #Nigeria wataweza kujitutumua na kurudisha goli hilo kipindi cha pili?

#AFCON2019 #JFLeo
RAIA WA KIGENI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia raia wawili wa Uingereza na mmoja wa Ireland kwa kosa la kusafirisha dhahabu gramu 1,044.95 bila kuwa na kibali kutoka Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam

Soma - https://jamii.app/UsafiriDhahabuWageni
MAREKANI: WANASAYANSI WAFANIKIWA KUONDOA VVU KWA PANYA

> Watafiti nchini Marekani wamesema wamefanikiwa kuondoa Virusi Vya Ukimwi kutoka kwenye vinasaba (DNA) vya panya 9 kati ya 23

> Kutokana na mafanikio hayo endapo mamlaka za chakula na dawa zitathibitisha tiba hiyo kwa binadamu inaweza kuanza kutumika mapema mwaka ujao

Soma - https://jamii.app/TibaVVUPanya
MICHEZO: Timu ya Taifa ya #Nigeria yafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka timu ya Taifa ya #Cameroon kwa mabao 3 kwa 2

#AFCON2019 #JFLeo
Mchezo wa #AFCON2019 kati ya #Misri na #SouthAfrika maarufu kama #Bafanabafana umekwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 0 kwa 0

> Je, unaweza kubashiri timu gani itaibuka na ushindi katika kipindi cha pili?
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #SouthAfrica maarufu ‘#Bafanabafana’ imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Egypt goli 1-0

- Katika hatua ya robo fainali, South Africa itakutana na #Nigeria iliyofanikiwa kuitoa #Cameroon

#JFLeo #EGYRSA
#CopaAmerica2019: #Argentina imeibuka mshindi wa tatu katika michuano hiyo baada ya kuifunga #Chile goli 2-1

> Katika mchezo huo, Lionel Messi wa Argentina na Gary Medel wa Chile walipewa kadi nyekundu

> Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kati ya #Brazil na #Peru mida ya saa 5 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki
MSAIDIZI WA MEMBE, ALLAN KILUVYA ANADAIWA KUTEKWA NA WATU ‘WASIOJULIKANA’

> Taarifa kwa kina zinafuata...
MSUMBIJI: IS IMEKIRI KUHUSIKA KWENYE SHAMBULIO LILILOUA WATU 7

- Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumatano kwenye kijiji cha Lidjungo huko Nangade

- Hii ni mara ya pili kwa kikundi hicho kukiri kuhusika kwenye mashambulio Nchini humo

Soma https://jamii.app/ISAttackInMoz
#JFLeo
RAIS MAGUFULI AMZAWADIA TAUSI RAIS KENYATTA

- Amemzawadia Tausi wanne kama kumbukumbu ya Uhusiano, Urafiki na Ujirani mwema baina ya Nchi hizo mbili

- Rais Kenyatta alifika wilayani Chato Julai 5, kwaajili ya ziara binafsi ya siku 2

Soma https://jamii.app/KenyattaApewaTausi
#JFLeo
WAZIRI LUGOLA ARUHUSU MABASI YA ABIRIA KUSAFIRI SAA 24

- Amewataka makamanda wa Polisi kutozuia mabasi kwa kisingizio cha kuhofia majambazi

- Amesisitiza mabasi yanayotoka Kanda ya Ziwa kutozuiwa Morogoro na yanayotoka Dar kutozuiwa Shinyanga

Soma https://jamii.app/MabasiKusafiriSaa24
#JFLeo
Mchezo wa #AFCON2019 kati ya #Madagascar na #DR Congo umekwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 1 kwa 1

> Je, unaweza kubashiri timu gani itaibuka na ushindi katika kipindi cha pili?