JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Timu ya taifa ya #Benin imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya #AFCON2019 baada ya kuifunga timu ya taifa ya #Morocco kwa changamoto ya mikwaju ya penati

> #Benin imeshinda kwa kupata penati 4 dhidi ya penati 1 ya #Morocco

#JFSPorts
Mchezo wa michuano ya #AFCON2019 wa hatua ya 16 bora kati ya #Uganda dhidi ya #Senegal umeenda mapumziko kwa #Uganda kufungwa goli 1 kwa 0

> Goli la #Senegal limefungwa na mshambuliaji wa Liverpool FC, Sadio Mane dakika ya 15

#JFSports
Timu ya Taifa ya #Uganda 'The Cranes' imeondoshwa katika michuano ya #AFCON2019 baada ya kukubali kipigo cha goli 1 kwa 0 kutoka kwa timu ya Taifa ya #Senegal

> #Uganda ndio timu pekee kutoka Afrika Mashariki iliyokuwa imesalia katika michuano hiyo

#JFSports
NEMC: KELELE ZA VIWANDA, NGOMA, MUZIKI, IBADA KUANZA KULIPIWA. WATAKAOKIUKA KUTOZWA FAINI

> NEMC imesema kwa Mtu atakayetaka kufanya shughuli hizo atapaswa kulipa milioni 10

> Watakaokiuka watatozwa faini isiyozidi milioni 50 ama kifungo jela

Soma > https://jamii.app/NEMCVsKelele
Mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya #Cameroon na #Nigeria umeenda mapumziko kwa #Cameroon kuongoza kwa magoli 2 kwa 1

> Je, #Nigeria wataweza kujitutumua na kurudisha goli hilo kipindi cha pili?

#AFCON2019 #JFLeo
RAIA WA KIGENI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia raia wawili wa Uingereza na mmoja wa Ireland kwa kosa la kusafirisha dhahabu gramu 1,044.95 bila kuwa na kibali kutoka Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam

Soma - https://jamii.app/UsafiriDhahabuWageni
MAREKANI: WANASAYANSI WAFANIKIWA KUONDOA VVU KWA PANYA

> Watafiti nchini Marekani wamesema wamefanikiwa kuondoa Virusi Vya Ukimwi kutoka kwenye vinasaba (DNA) vya panya 9 kati ya 23

> Kutokana na mafanikio hayo endapo mamlaka za chakula na dawa zitathibitisha tiba hiyo kwa binadamu inaweza kuanza kutumika mapema mwaka ujao

Soma - https://jamii.app/TibaVVUPanya
MICHEZO: Timu ya Taifa ya #Nigeria yafanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka timu ya Taifa ya #Cameroon kwa mabao 3 kwa 2

#AFCON2019 #JFLeo
Mchezo wa #AFCON2019 kati ya #Misri na #SouthAfrika maarufu kama #Bafanabafana umekwenda mapumziko kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 0 kwa 0

> Je, unaweza kubashiri timu gani itaibuka na ushindi katika kipindi cha pili?
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #SouthAfrica maarufu ‘#Bafanabafana’ imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Egypt goli 1-0

- Katika hatua ya robo fainali, South Africa itakutana na #Nigeria iliyofanikiwa kuitoa #Cameroon

#JFLeo #EGYRSA
#CopaAmerica2019: #Argentina imeibuka mshindi wa tatu katika michuano hiyo baada ya kuifunga #Chile goli 2-1

> Katika mchezo huo, Lionel Messi wa Argentina na Gary Medel wa Chile walipewa kadi nyekundu

> Mchezo wa Fainali utafanyika kesho kati ya #Brazil na #Peru mida ya saa 5 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki