JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI: NILIMTEUA MTU WA DARASA LA 7 KUWA MENEJA WA MKOA

> Amesema alipokuwa Waziri wa Ujenzi alimteua Mtu menye elimu ya Darasa la Saba kuwa Meneja wa TAMESA wa Mkoa wa Kagera

> Alimteua baada ya kuona utendaji wake kuwa zaidi ya wasomi

Soma > https://jamii.app/RaisMenejaSTD7
MISUNGWI: AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUZAA NA BINTI YAKE

> Jacob Shabani(30) alianza kufanya mapenzi na mwanaye baada ya kutengana na mama yake

> Alimpa ujauzito mara 3; mimba 1 iliharibika baada ya kumpiga sana na sasa ana mtoto wa mwaka 1

Soma https://jamii.app/BabaMimbaMtoto
RATIBA YA LIGI KUU SOKA UINGEREZA 2019/20 YATOKA

> Agosti 9, 2019 Liverpool v Norwich City

> 10 Agosti, 2019 West Ham v Manchester City, Tottenham v Aston Villa

> Agosti 11, 2019 Newcastle United v Arsenal, Man Utd v Chelsea

Zaidi, soma => https://jamii.app/RatibaEPL

#JFSports
SERIKALI: PATO LA WASTANI LA KILA MTANZANIA LIMEONGEZEKA

> Pato lilifikia Tsh. Milioni 2.4 mwishoni mwa mwaka 2018 kutoka Tsh. Milioni 2.3 mwaka 2017

> Ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 5.6 ambao ni sawa na Tsh. 100,000 kwa kila Mtanzania

Soma - https://jamii.app/OngezekoPatoRaia
KATIBU MWENEZI CHADEMA, MALINYI MOROGORO AUAWA KWA RISASI

> Inaelezwa kuwa Lucas Lihambalimu amevamiwa akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo

> Jeshi la Polisi limesema kuwa linafanya uchunguzi wa tukio hilo

Soma > https://jamii.app/RIPLihambalimu

#JFLeo
VIFUNGASHIO VYA KARANGA NA UBUYU VYAPIGWA MARUFUKU

> Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC), limepiga marufuku vifungashio vya kienyeji (plastiki) vinavyotumika kufungashia karanga, ice cream, miwa na ubuyu na atakayekutwa navyo atalipa faini kati ya Tsh 30,000 na Tsh 200,000 au kuwekwa mahabusu siku 7

Soma - https://jamii.app/ZuioVifungashioPlastiki
SERIKALI YAPENDEKEZA TOZO NA MUDA WA LESENI YA UDEREVA KUONGEZEKA

> Serikali imependekeza kuongezwa kwa muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi miaka mitano na kuongezwa kwa tozo ya leseni ya udereva kutoka Tsh. 40,000 kwenda Tsh. 70,000

Soma https://jamii.app/OngezekoTozoLeseni
#JFLeo
SERIKALI YAPENDEKEZA NYWELE BANDIA KUTOZWA USHURU

> Waziri wa Fedha ametoa pendekezo la kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa nchini na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi ili kuongeza mapato ya Serikali

Soma - https://jamii.app/OngezekoTozoLeseni
#JFLeo
UGANDA: MAMA AMLISHA MTOTO DAMU YA HEDHI

> Annet Namata amempa binti yake wa kambo chakula alichokichanganya na damu yake ya hedhi kwa madai kuwa mume wake anampenda sana mtoto huyo na kumnunulia zawadi nyingi kuliko yeye

> Alishauriwa na marafiki zake kwa lengo la kumfanya mtoto awe mwendawazimu

Soma - https://jamii.app/MotherChildAbuse
UCHAGUZI WAZIRI MKUU UINGEREZA: BORIS JOHNSON ASHINDA DURU YA KWANZA

> Mchakato umeanza ndani ya chama cha Conservative baada ya Waziri Mkuu, Theresa May kujiuzulu

> Boris Johnson ameshinda duru ya kwanza kwa kupata kura 114

Soma > https://jamii.app/BorisJohnson
DAR KINARA WA MSONGAMANO WA WATU MWAKA 2018

> Dar ilikuwa na msongamano wa watu 3,695 kwa kila kilomita moja ya mraba ikifuatiwa na Mwanza iliyokuwa na watu 373.1, Kagera watu 119.6 na Kilimanjaro watu 104

> Lindi imetajwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya watu kwa kilomita moja ya mraba ikiwa na wastani wa watu 14.9

Soma - https://jamii.app/OngezekoPatoRaia
KENYA: MBUNGE AKAMATWA KWA KUMPIGA MBUNGE MWENZAKE

> Rashid Kassim anatuhumiwa kwa kumchapa kibao Fatuma Gedi akimtuhumu kutopeleka fedha kwenye jimbo lake

> Fatuma Gedi ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

Zaidi, soma => https://jamii.app/MbungeApigaKE
IKULU: Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Antoine Tshisekedi amewasili nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais John Pombe Magufuli na amehudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake

> Tshisekedi amesema baada ya kumaliza changamoto za usalama nchini kwao anatarajia kushirikiana na Tanzania katika fursa mbalimbali zilizopo kwenye madini, nishati na miundombinu ikiwemo ya ujenzi wa reli itakayounganisha Tanzania na DRC

Soma - https://jamii.app/ZiaraDRCPresdnt
ULEVI NA UZEMBE WACHANGIA ASILIMIA 76 YA AJALI ZA BARABARANI

> Imeelezwa kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali za barabarani ni makosa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na ulevi na uzembe ambao huchangia kwa asilimia 76

> Ubovu wa Magari huchangia asilimia 16 na mazingira ya Barabara asilimia 8

Soma - https://jamii.app/UleviUzembeAjali
1
OFISI YA CHADEMA MKOANI LINDI YATEKETEZWA KWA MOTO

> Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na limetekelezwa na watu ambao hadi sasa hawajafahamika

> Taarifa hizi zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini, Cecil Mwambe

Soma => https://jamii.app/OfisiCDMLindi
WANANCHI KUTOA MIZIGO BANDARINI BILA KUTUMIA WAKALA WA FORODHA

> Waziri wa Fedha amesema kutakuwa na utaratibu mpya wa kuondoa mizigo bandarini ambapo wananchi wa kawaida wataruhusiwa kutoa mizigo yao bila ya kuwa na ulazima wa kutumia Wakala wa Forodha (Clearing and Forwarding Agents)

> Utaratibu huu hautahusisha mizigo inayopitishwa nchini kwenda nje ya nchi (Transit Cargo)

Soma - https://jamii.app/UtoajiMizigoBandari
KODI KUANZA KULIPWA BAADA YA MIEZI 6 TANGU KUPATA TIN

> Serikali imesema mfanyabiashara ama mwekezaji atakapopatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) atatakiwa kuanza kulipa kodi baada ya miezi 6

> Imeiagiza TRA kuanzisha dawati la kushughulikia mapingamizi ya makadirio ya kodi ambapo mapingamizi ya uthaminishaji na utambuzi yatashughulikiwa ndani ya saa 24

Soma - https://jamii.app/MudaKodiTIN
IRAN YASHUTUMIWA KUHUSIKA NA SHAMBULIZI LA MELI ZA MAFUTA

> Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo ameilaumu nchi ya Iran kuhusika na shambulizi la mwezi Mei dhidi ya meli za mafuta kwenye pwani ya nchi za Ghuba

> Mlipuko ulitokea katika meli moja ya Japan na nyingine ya Norway

Soma - https://jamii.app/IranShipOil
MAHITAJI NA HATUA ZA UPISHI WA MAKANGE YA KUKU

> Mahitaji kwa ajili ya upishi wa chakula hiki ni Kuku, mafuta ya kupikia, tangawizi, kitunguu saumu na maji, karoti, hoho, ndimu, chumvi

> Mahitaji mengine: chicken masala, Nyanya ya pakti na kawaida pamoja na Pilipili

Kwa maelezo ya idadi ya mahitaji na jinsi ya kupika, soma => https://jamii.app/MakangeKuku