JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: RAIA WA CHINA WAFUKUZWA KUFANYA BIASHARA

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang'i amewatimua nchini humo wafanyabiashara saba waliopatikana na hatia ya kufanya biashara zao kinyume cha sheria katika soko la mitumba la Gikomba

Soma - https://jamii.app/BiasharaChinaKE
UMOJA WA ULAYA(EU): MITANDAO YA KIJAMII IFANYE JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UPOTOSHAJI

> EU imetoa rai kwa Mitandao ya Kijamii na majukwaa ya mitandaoni baada ya tuhuma za Urusi kujaribu kuingilia uchaguzi wa Bunge la Jumuiya hiyo

Soma > https://jamii.app/UrusiVsEU
FAMILIA YAMUUA BABA ALIYEUA WATOTO WAKE WATATU

> Familia kwa kushirikiana na majirani imemuua Daudi Kipkoir Kamaril mkazi wa Kapker, katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet ambaye aliwaua kwa risasi watoto wake 3 na kuwajeruhi wengine 3

> Kwa mujibu wa Polisi, wananchi hao walitumia bunduki ileile aliyoitumia kuwaua wanawe

Soma - https://jamii.app/MauajiBabaWatoto
AFRIKA MASHARIKI: KENYA KINARA BAJETI KUBWA KWA MWAKA 2019/2020

> Nchi ya Kenya imetenga kiasi cha Ksh trilioni 3.02 sawa na Tsh trilioni 60 na Rwanda imepanga kutumia Rwf trilioni 2.8 sawa na Tsh trilioni 6

> Uganda inakadiria kutumia dola bilioni 10.9, ambayo ni Tsh trilioni 25 na Tanzania imetenga bajeti ya Tsh trilioni 33.1

#JFLeo
MEXICO KUPIGA MNADA NDEGE YA RAIS ILI KUDHIBITI UHAMIAJI HARAMU

> Rais Andres Manuel Lopez ametangaza kupiga mnada ndege ya Rais na fedha zitakazopatikana zitatumika kusaidia jitihada za kudhibiti uhamiaji haramu

> Ndege hiyo aina ya Boeing 787 Dreamliner ilinunuliwa mwaka 2016 kwa dola milioni 218 lakini sasa inaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua dola milioni 150

Soma https://jamii.app/MnadaNdegeRais
BRAZIL: CHUKI DHIDI YA WAPENZI WA JINSIA MOJA YAWA KOSA LA JINAI

> Majaji wa Mahakama ya Juu nchini humo wamepiga kura iliyotoa uamuzi huo

> Kura 8 kati ya 11 zimepitisha chuki dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuwa jinai

Soma > https://jamii.app/HomophobiaBrazil
TUME YA SHERIA YAPENDEKEZA UWEPO WA SHERIA MOJA YA UFILISI

> Tume ya Kurekebisha Sheria imependekeza kutungwa kwa sheria moja baada ya kubaini baadhi ya zilizopo kupitwa na wakati na baadhi zinatoa adhabu au faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kama vile Tsh. 200 au Tsh. 1,000

Soma - https://jamii.app/UtafitiSheriaUfilisi
WABUNGE 83 KUSAFIRI HADI MISRI KWENDA KUISHANGILIA TAIFA STARS

> Idadi hiyo ya Wabunge itakwenda nchini Misri kuiunga mkono timu ya Taifa katika mashindano ya AFCON 2019.

> Msafara huo utaongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Zaidi, soma => https://jamii.app/WabungeMisri
TUME YA SHERIA YAPENDEKEZA UWEPO WA SHERIA MOJA YA UFILISI

> Tume ya Kurekebisha Sheria imependekeza kutungwa kwa sheria moja baada ya kubaini baadhi ya zilizopo kupitwa na wakati na baadhi zinatoa adhabu au faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kama vile Tsh. 200 au Tsh. 1,000

Soma - https://jamii.app/UtafitiSheriaUfilisi
SUDAN KUSINI KUFUNGA BAADHI YA BALOZI ZAKE ILI KUBANA MATUMIZI

> Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kwamba Sudan Kusini imechukua hatua ya kuzifunga balozi zake katika nchi za Ufaransa, Norway, Ghana, Kuwait na Italia kutokana na kuzorota kwa uchumi na ukosefu wa utulivu wa kisiasa

Soma - https://jamii.app/FinancialCrisisSudan
#JFInternational
KYELA, MBEYA: POLISI ALIYEMPA UJAUZITO MWANAFUNZI ATOWEKA

> Konstebo Mlanda ametoroka baada ya kutuhumiwa kumbaka na kumpa ujauzito Mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye miaka 14

> Mwanafunzi adai alibakwa kwa shinikizo la Mama yake mlezi

Soma > https://jamii.app/AskariAbakaKyela
MOROGORO: POLISI WAWAZUIA CHADEMA KUFANYA MKUTANO
-
Mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo uliokuwa ufanyike tarehe Juni 16, 2019 umefutwa na Jeshi la Polisi kwa sababu za kiusalama
-
Hata hivyo, inadaiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wao wamepata kibali cha kufanya mkutano wao leo Mkoani humo
WATATU MBARONI KWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KATIBU WA CHADEMA

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kumuua Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42)

> Uchunguzi uliofanywa umebaini chanzo cha mauaji kuwa ni mgogoro wa mashamba

Soma - https://jamii.app/3MbaroniMauajiCDM
YEMEN: WATOTO WACHANGA 6 HUFARIKI KILA BAADA YA SAA MBILI

> Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limesema tangu kuongezeka kwa mapigano, vifo wakati wa kujifunga vimeongezeka kutoka vifo 5 kwa siku mwaka 2013 na kufikia 12 kwa siku mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/VifoVichangaWajawazito
HONG KONG: MUSWADA WA SHERIA WASITISHWA KUFUATIA MAANDAMANO

> Serikali inayoongoza Jimbo hilo imetangaza kusitisha muswada uliolenga kuruhusu watuhumiwa wa makosa mbalimbali kushtakiwa China

> Hong Kong ni Jimbo la China lenye mamlaka yake

Soma => https://jamii.app/MuswadaHongKong
KYELA, MBEYA: WATU ZAIDI YA 10 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI

> Wamejeruhiwa katika ajali inayoelezwa kuwa imesababishwa na mwendokasi wa basi aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria

> Ajali imetokea katika Kijiji cha Ikomelo mchana wa leo

Soma > https://jamii.app/AjaliKyela
HAPPY FATHER’S DAY: Leo ni Siku ya kusherekea, kuenzi na kutambua nafasi ya Baba kwenye maisha ya mtoto
-
Menejimenti na Wafanyakazi wa JamiiForums wanawatakia kina Baba wote Upendo na Amani kwenye siku hii muhimu
MOGADISHU: WATU 11 WAMEFARIKI NA 25 KUJERUHIWA KWENYE MILIPUKO

- Ni milipuko ya kujitoa muhanga iliyohusisha magari kwenye eneo la ukaguzi la Kasri ya Rais na eneo la ukaguzi la Uwanja wa Ndege

- Al-Shabab wamekiri kuhusika na milipuko hiyo

Soma https://jamii.app/MilipukoMogadishu
KOCHA WA CHELSEA, MAURIZIO SARRI AJIUNGA JUVENTUS

- Kocha huyo amejiunga na Juventus kwa kandarasi ya miaka 3 baada ya kukaa Chelsea kwa msimu mmoja

- Akiwa Chelsea, alifanikiwa kuchukua Kombe la Europa likiwa ndio taji lake kubwa katika maisha yake ya Ukocha