JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SINGIDA: MWALIMU WA MADRASA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

> Daudi Idd Karata(26) amepewa hukumu hiyo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida kwa hatia ya kumnajisi Mtoto wa kike(8)

> Ajitetea kuwa yeye ni Mwalimu wa Dini na hawezi kutenda kosa hilo

Soma > https://jamii.app/JelaUnajisiMtoto
MAFURIKO BUKOBA: Mvua zinazoendelea kunyesha, zimesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara baada ya daraja la Kanoni kufunikwa na maji

- Daraja la Kanoni ndilo linalounganisha barabara Kuu ya kwenda mikoani, lipo Hamugembe

Soma https://jamii.app/MafurikoBukoba
KENYA: KIJANA MBARONI KWA KUMPIGA MPENZI WA MAMA YAKE

- Mwenyekiti wa Polisi Jamii amesema, mtuhumiwa alimfuata mwanaume huyo na kumtaka amueleze kwanini yupo kwenye mahusiano na mamake huku akijua ameolewa

- Majeruhi amepelekwa hospitali

Soma > https://jamii.app/AmpigaMpenziMama
AFRIKA KUSINI YAAHIDI KUAJIRI WALIMU WA KISWAHILI KUTOKA TANZANIA

> Katika Mazungumzo na Rais Magufuli, Rais Ramaphosa amesema nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili wafundishe somo hilo katika shule za msingi na sekondari

Soma https://jamii.app/SwahiliTeachersSATZ
BRAZIL: WAFUNGWA 15 WAFARIKI KWENYE VURUGU ZILIZOTOKEA GEREZANI

- Wamefariki jana Mei 26 katika gereza moja lililopo kwenye jimbo la Amazonas baada ya vurugu baina yao(Wafungwa) kuzuka

- Walifariki ama kwa kukosa hewa au kuchomwa na vitu vya ncha kali ikiwemo miswaki

Zaidi, soma https://jamii.app/RiotBrazilPrison15Dead
IRAQ: WANACHAMA 3 WA DOLA YA KIISLAMU WAHUKUMIWA KUNYONGWA

- Mahakama moja nchini humo jana iliwahukumu kifo wanachama hao ambao ni raia wa Ufaransa

- Watuhumiwa hao ni miongoni mwa Wafaransa 13 waliokamatwa katika mapambano huko Syria

Zaidi, soma https://jamii.app/Wafaransa3KunyongwaIraq
UCHUMI: SEKTA ZINAZOONGOZA KWA KUTAKATISHA FEDHA ZATAJWA

> Ripoti ya Utakatishaji Fedha na Ugaidi ya mwaka 2016 iliyotolewa hivi karibuni imezitaja sekta zinazoongoza ni biashara ya magari, maduka ya kubadilishia fedha, biashara ya nyumba na madini

Zaidi, soma > https://jamii.app/SektaUtakatishajiFedha
TANGA: ANAYEDAIWA KUWA MGONJWA WA AKILI AUAWA BAADA YA KUUA WATU 2

- Mgonjwa huyo anayedaiwa kutoroka kwa mganga wa kienyeji amewaua Wanakijiji wa Kilometa 7, Wilayani Muheza

- Aliwaua kwa kuwapiga kwa fimbo huku yeye akiuawa na Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/MgonjwaAkiliAua2-TA
RAIS MAGUFULI AONDOKA AFRIKA KUSINI, AELEKEA NAMIBIA

- Ameelekea Windhoek, Namibia baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Rais Cyril Ramaphosa na kuzungumza naye

- Atafanya ziara rasmi nchini Namibia kutokana na mwaliko wa Rais Hage Geingob

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAendaNamibia
MWANZA: ASKARI MAGEREZA MABARONI KWA UTAPELI

- Kibemba Warioba(27) mwenye namba B.9205 WDR, amekamatwa akiwa na simu 5 za mitandao tofauti

- Mtuhumiwa akitumia mitandao ya simu alianzisha SACCOS bandia iliyojulikana kama 'Info Tell CCM'

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariTapeliMbaroni-MWZ
RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI NAMIBIA

- Amepokelewa na Mwenyeji wake, Rais Hage Geingob katika Ikulu ya nchi hiyo, Jijini Windhoek leo Mei 27

- Rais Magufuli atakuwa nchini Namibia kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku mbili

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAendaNamibia
SERENGETI: BINTI AUAWA NA TEMBO WALIOKUWA WAKIFUKUZWA SHAMBANI

> Tukio hili limetokea usiku katika kijiji cha Bukore kata ya Kyambahi, ambapo binti wa miaka 26, Motondi Shakanyi ameuawa kwa kushambuliwa na Tembo waliofukuzwa shambani

Zaidi, soma => https://jamii.app/BintiAuawaTembo
EDEN HAZARD ASHINDA TUZO YA 'PFA FANS' PLAYER OF THE YEAR'

- Mshambuliaji huyo wa Chelsea amewashinda Bernardo Silva, Sergio Aguero, Raheem Sterling, Sadio Mane na Virgil van Dijk

- Msimu huu amefunga magoli 16 na kutoa pasi za magoli 15 katika Ligi Kuu ya England
WATANZANIA WAONGOZA KWA MATUMIZI YA BANGI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

> Utafiti huu ni kwa mujibu wa taasisi ya New Frontier Data ya Uingereza ambapo licha ya Tanzania kuongoza kwa Afrika Mashariki pia imeshika nafasi ya 5 kwa nchi za Afrika

Soma > https://jamii.app/TzMarijuana
SINGIDA: TAKUKURU INAMSHIKILIA LAZARO NYALANDU

- Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa imemkamata Mwanachama huyo wa CHADEMA, aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa mahojiano

- Amekamatwa akiwa kwenye kikao cha chama katika Kata ya Itaja, mkoani Singida

Zaidi, soma https://jamii.app/NyalanduAkamatwaTAKUKURU
KILIMO: JIFUNZE AINA KUU 5 ZA ZAO LA KAROTI

> Kuna aina kuu 5 za Karoti ambazo ni Nantes, Chantenay Red Core, Oxheart, Cape Market, Flacoro

> Zao hili hustawi vizuri kwenye sehemu zenye joto la wastani (nyuzi joto 15 hadi 27 za Sentigredi)

Zaidi, soma => https://jamii.app/AinaKaroti

#JFKilimo
DAR: WAFANYABIASHARA 116 WA MTAA WA TANDIKA WAFUNGA MADUKA KISA KODI KUBWA

- Wamedai Mkurugenzi anataka kodi kubwa isiyo rafiki na isiyokuwepo kisheria

- Anataka kodi kuanzia Tsh. 600,000 kwa miezi 3 wakati sasa kodi ya juu ni Tsh. 150,000

Zaidi, soma https://jamii.app/MadukaYafungwaTandika