JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Abdallah Possi, ametoa utetezi katika Baraza la Haki za Binadamu ofisi ya Geneva, Uswisi, kuhusu madai ya kutesa na kudhalilisha Wanaharakati Juni 18, 2025

Amesema "Pamoja na kuwa shutuma zao dhidi ya Serikali zina mashaka makubwa, tunayachukulia kwa uzito mkubwa madai ya kuteswa, Unyanyasaji wa Kingono na vitendo vya ukiukaji wa Maadili. Ndio maana Serikali kwa sasa inachunguza, na ikithibitika, wahusika watachukuliwa hatua"

Aidha, ameeleza kuwa "Serikali imejizatiti kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa Amani, Uwazi, na kwa kuzingatia viwango vya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa vya Haki za Binadamu, Tanzania inaendelea kulinda Uhuru wa Kujieleza, Haki ya kupata Taarifa, na Ushiriki wa Vyombo vya Habari. Tunaamini katika Usawa mbele ya sheria kwa Watu wote, wakiwemo watetezi wa Haki za Binadamu"

Soma https://jamii.app/TanzaniaKujiteteaUN

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia #HumanRights #KuelekeaUchaguzi2025
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
GEITA: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema muda wa Miaka mitano hauwezi kumaliza matatizo yote ndani ya Nchi na wale wanaodhani hilo linawezekana ni Watu wa ajabu

Amesema hayo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM katika kikao cha ndani, jana Juni 18, 2025, Geita Mjini

Soma https://jamii.app/WasiraGeita

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Juni 18, 2025, Mwanachama wa Chama cha #ACTWazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewasisitiza Wanachama wa Chama hicho kuwa washiriki katika Uchaguzi wa 2025 na muhimu wanatakiwa kulinda Kura wanazopiga

Soma https://jamii.app/PondaJuni18

#JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
#KENYA: Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) imemuita Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIG), #EliudLagat kutoa maelezo kuhusiana na kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang, aliyefariki akiwa Mikononi mwa Polisi akidaiwa kupigwa kwa amri ya DIG na OCS

Lagat, ambaye alitangaza kujiondoa kwa muda Ofisini ili kuruhusu uchunguzi kufanyika, ndiye Mlalamikaji aliyedai kuchafuliwa kupitia chapisho la #Ojwang kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter), na anatarajiwa kufika katika Ofisi za IPOA, leo Alhamisi Juni 19, 2025

Mwenyekiti wa IPOA, Issack Hassan amethibitisha kuwa Mamlaka hiyo “imeona msingi" wa kumuita Afisa huyo wa ngazi ya juu.

Soma https://jamii.app/IPOACallsDIGLagat

#JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Accountability #HumanRights
2
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com akitaja mambo mbalimbali ya kumfundisha Mtoto wako anasema, akiingia Darasa jipya, awaangalie wenzake wasio na uwezo mkubwa, awape Vitabu vyake watumie kusoma badala ya kuviacha vikiharibika ndani

Pia, wajue kwa Majina Marafiki zake kadri unavyoweza, jua Maendeleo yao, wakiwa Wagonjwa mpe nafasi akawasalimie, utamjengea Ushirika mkubwa kwenye Maisha yake ya ukubwani.

Unakubaliana na Mdau?

Soma zaidi https://jamii.app/WatotoElimuNetwork

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Uwajibikaji #JFStories #JFChitChats
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese, Juni 18, 2025, Mwanachama wa Chama cha #ACTWazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda, amewasisitiza Wanachama wa Chama hicho kuwa washiriki katika Uchaguzi wa 2025 na muhimu wanatakiwa kulinda Kura wanazopiga

Soma https://jamii.app/PondaJuni18

#JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church(Ufufuo na Uzima), Askofu Baraka Thomas Tege, amedai tangu Kanisa hilo lilipofungwa Juni 2, 2025 na majengo yao kulindwa na Jeshi la Polisi, hakukuwa na makabidhiano yoyote ya Mali zikiwamo Fedha za Sadaka, Vyombo vya Muziki na Samani

Askofu Tege amedai Polisi wameweka Makufuli kwenye Milango ya Makanisa na kuwaondoa waliokuwa Walinzi

Soma https://jamii.app/GwajimaKanisaMali

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #Governance
1
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka Wasafiri wa Ndege ndani na nje ya Nchi kutositisha safari zao za kuja Tanzania kutokana na hofu ya tangazo la Umoja wa Ulaya (EU) la Juni 3, 2025 kuhusu kuzuia baadhi ya Mashirika ya Ndege kutumia Anga lake, ikisisitiza kuwa hatua hiyo haijahusisha Ndege zilizosajiliwa nje Tanzania sababu haziko chini ya TCAA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TCAA Juni 18, 2025 imesema kuwa tayari imeanza kuchukua hatua za kufanyia kazi matakwa ya Kiusalama yaliyoainishwa na Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa yao Juni 3, 2025 ya katazo la Ndege zilizosajiliwa Tanzania katika Anga la Bara la Ulaya kutokana na masuala ya Kiusalama

Soma https://jamii.app/SafariNdegeEU

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#SIASA: Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Constantine Sima, amedai kufanyiwa hujuma na fitina na baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa maslahi yao binafsi

Sima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mhandu amesema “Limekuwepo kundi ambalo limekuwa likipita kwenye maeneo yetu kutuchafua, kutweza Utu lakini pia, kufanya mambo ambayo Mtu akikwambia unaweza kubaki mdomo wazi."

Ameongeza "Tuwaogope sana Watu ambao wanakuja kutafuta nafasi kwa mambo makubwa matatu, kwanza kuja kulipa kisasi, anakuja kwasababu ya uadui na Mtu lakini anakuja kumkomoa Mtu fulani."

Soma https://jamii.app/SiasaMwanza

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025
1
Kushinda ni zawadi. Kushindwa ni darasa. Vyote vina maana, cha muhimu ni kujifunza

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
👍1
Ungependa Mwanao afanye Kazi/Shughuli unazozifanya kwa sasa, au unatamani iwe tofauti?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MtotoKaziKamaYako

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFStories #JFChitChats #Maisha
1