JamiiForums
55.4K subscribers
33.4K photos
2.03K videos
30.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Nidhamu ni Msingi wa Mafanikio, kipaji pekee hakitoshi.

Ili kufikia ndoto zako, unahitaji nidhamu isiyoyumba. Nidhamu ndiyo inageuza uwezo wako kuwa matendo na hatimaye, mafanikio unayoyatamani

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa tamko kuwa kuna hali ya hatari inayojitokeza kwa kasi dhidi ya Vyama vya Siasa vinavyopigania mabadiliko ya kweli nchini

Chama hicho kimedai kuna juhudi za kurejea kwa enzi za Utawala wa Kiimla unaotumia Vyombo vya Dola na Mahakama kama zana za kukandamiza sauti mbadala, badala ya kulinda haki za Wananchi na Utawala wa Sheria

CHADEMA imetoa wito kwa Viongozi, Wanachama, Wafuasi wake na wote wanaoamini katika misingi ya uhuru, haki, na demokrasia, kuwa tayari kupokea maelekezo kutoka kwa Viongozi Wakuu wa Chama na kuwa hawatarudi nyuma katika kudai Tanzania yenye Mfumo wa Haki, Uhuru na Utawala wa Sheria.

Soma https://jamii.app/TamkoLaCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #Democracy
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupinga kifungo cha Maisha jela walichohukumiwa aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Clinton Damas, maarufu Nyundo na wenzake Amin Lema, Nickson Jackson na aliyekuwa Askari Magereza, Praygod Mushi, huku upande wa Jamhuri ukiomba kuzijibu Juni 12, 2025

Akiwasilisha hoja Mahakamani, Juni 10, 2025, Wakili wa Warufani hao, Godfrey Wasonga amedai kulikuwa na dosari za Kisheria katika kesi hiyo kuanzia hati ya mashtaka hadi hukumu. Amedai Mahakama ilioneshwa vipande Vinne vya Video ambavyo ni 6, 7, 8 na 9 lakini kwenye hukumu, vipande vya Video vilivyowatia hatiani ni namba 1, 2, 3 na 4 ambavyo havikuoneshwa Mahakamani hapo

Aidha, kwa mujibu wa Wakili huyo, vipande vya Video vilivyooneshwa viliwaonesha washtakiwa wakijirekodi wakiwa wanacheza Muziki, huku wakiwa na chupa za Vinywaji lakini hazikuonesha wakiwa wanatenda kosa la kubaka kwa kikundi wala kulawiti

Soma https://jamii.app/UpdatesKesiYaNyundo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, ameibua hoja #Bungeni leo Juni 11, 2025 akidai kuwepo kwa Mazingira yasiyo rafiki kwa Viongozi na Familia zao wanapopita maeneo ya VIP katika Viwanja vya Ndege

Soma https://jamii.app/MusukumaJuni11

#JamiiAfrica #Siasa #Govevernance #JamiiForums
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Leo Juni 11, 2025, Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amependekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu zitakazowatambulisha Barabarani kwenye misafara au kwenye shughuli zao za kila siku

Zaidi https://jamii.app/WabungeSpecialPlateNumbers

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Kuelekea2025 #Governance
Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga, Wakili Mwandamizi Martha Karua, pamoja na watu wengine wanne wamefungua kesi katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) dhidi ya Serikali ya Tanzania, wakidai kuwekwa kizuizini kinyume cha Sheria, kunyimwa kuingia nchini na kufukuzwa kati ya Mei 18 hadi 19, 2025, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Kundi hilo ambalo pia linajumuisha Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu wanne ambao ni Gloria Kimani, Lynn Ngugi, Hussein Khalid na Hanifa Adan wamedai kuwa haki zao kama raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zilikiukwa waziwazi walipozuiwa kuingia Tanzania kushuhudia kesi ya uhaini dhidi ya Kiongozi wa Upinzani, Tundu Lissu

Aidha, Kesi hiyo inatarajiwa kuhamishiwa Makao Makuu ya EAC - Arusha ambako tarehe ya kusikilizwa itapangwa na Mahakama hivi karibuni

Soma https://jamii.app/KenyaKuiburuzaTZ

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza #Bungeni, leo Juni 11, 2025, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema Jengo la Bunge ni la Wananchi na hakuna Mwananchi anayekatazwa kutembelea hivyo ni lazima kuwe na Utaratibu wa Kiusalama kwa Wabunge wenyewe na Wageni, akisisitiza suala la Wabunge kukaguliwa ni la muhimu na lazima

Soma https://jamii.app/ZunguUsalamaBungeni

#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica
KENYA: Bunge la Seneti limesitisha shughuli zake za kawaida ili kujadili na kujibu maswali kuhusu uchunguzi wa kifo cha Albert Ojwang, ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen, Mkuu wa Polisi Douglas Kanja, na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) Amin Mohammed walikuwepo Bungeni kujibu maswali kuhusu kesi hiyo

Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja kwenye Vyombo vya Habari, Makamu Mwenyekiti wa IPOA, Anne Wanjiku, ameliambia Bunge kuwa Mifumo ya CCTV katika ofisi ya Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi alipokuwa akishikiliwa Albert ilichezewa, huku akiongeza kuwa uchunguzi wa awali kuhusu kifo hicho unatupilia nadharia kuwa Albert alijiua

Soma https://jamii.app/KikaoBungeKE

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance #HumanRights
Mdau wa Jukwaa la 'JF Chit chats and Jokes' ndani ya JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akihoji ni nani akija nyumbani kwako bila kukupa taarifa hutakuwa na tatizo naye?

Mjadala https://jamii.app/Kutembeleana

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeStyle
SINGIDA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai baadhi ya Maafisa Utumishi na Ofisi ya Mkurugenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanachelewa kupitisha barua za uhamisho wa Watumishi na kutoa wito kwa UTUMISHI au TAMISEMI kufuatilia na kuchukua hatua, ufafanuzi umetolewa

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imesema inatekeleza mchakato wa uhamisho wa Watumishi kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za Utumishi wa umma kupitia Mfumo rasmi wa maombi ya Uhamisho (Employee Self Service ESS)

Kuhusu Watumishi wanaohama kufuata wenza wao, Halmashauri hiiyo imeeleza mara ya mwisho walipokea barua Mei 2025 na zile zilizokidhi vigezo zimepitishwa na wahusika wamekabidhiwa kwa ajili ya Utekelezaji

Soma https://jamii.app/MkalamaDC

#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica #Uwajibikaji
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza na Wanahabari, leo Juni 11, 2025, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema "Wakati mwingine unaona vikampeni havina mbele wala nyuma. Vijana tutumie mitandao kwa njia za kimanufaa, ukifanya makosa tutakupata tu, jinai haifi."

Ameongeza “Tunaelekea katika Uchaguzi, mihemko imekuwa mingi, uhamasishaji wa Kijingajinga umekuwa mwingi, Vijana ‘watch out’, ukikamatwa utakuwa peke yako.”

Soma https://jamii.app/MsigwaKuhusuMitandao

#JamiiForums #DigitalRights #Governance #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekanusha kuwa mtu aliyetambulika kuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Igunga aliyeonekana akimuomba msamaha Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, John Heche, si mtumishi wa Jeshi hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Abwao, amesema baada ya msako wamemkamata mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Daud Paul Delim (49), Mkazi wa Mbagala A Wilayani Igunga aliyejifanya ni Mkuu wa Kituo cha Polisi

Ameongeza kuwa anaendelea kuhojiwa ili kujua alioshirikiana nao kuandaa picha mjongeo hiyo hasi na potofu na kuisambaza ili hatua stahiki za kisheria dhidi yao zichukuliwe

Soma https://jamii.app/RPCTabora

#JamiiAfrica #JFMatukio #JamiiForums