JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: ALIYEKUWA MENEJA WA KAMPENI WA RAIS DONALD TRUMP AFUNGWA JELA

> Paul Manafort(69) amefungwa miezi 47 jela sawa na miaka 3 na miezi 11 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi na udanganyifu wa kibenki

Zaidi, soma => https://jamii.app/ManafortConvicted

#JFInternational
SAME, KILIMANJARO: WATU 5 WAMEFARIKI BAADA YA PETROLI KULIPUKA

> Tukio hili la kusikitisha limetokea katika kijiji cha Marwa huku ikielezwa kuwa Petroli hiyo ilikuwa ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi

Zaidi, soma => https://jamii.app/PetroliYauaSame

#JFLeo
UFARANSA: KADINALI AHUKUMIWA KWA KUSHINDWA KUKEMEA UNYANYASAJI

> Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ufaransa, Kadinali Philippe Barbarin amehukumiwa kifungo cha miezi 6 jela kwa kushindwa kukemea vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto

Soma - https://jamii.app/KadinaliJelaUdhalilishaji
#JFInternational
MPANDA & GEITA: JESHI LA POLISI LAZUIA MAADHIMISHO YA WANAWAKE WA ACT NA CHADEMA

> Wametakiwa kuungana na Wanawake wengine katika maadhimisho ya kiserikali

> Imeelezwa kuwa hatua hiyo itazuia matangazo yenye mlengo wa kisiasa

Soma > https://jamii.app/WanawakeACTCDM

#BalanceForBetter
DR CONGO: SERIKALI YADAIWA KUWA MBIONI KUJENGA SANAMU YA TSHISEKEDI

> Ni ya Etienne Tshisekedi baba wa Rais wa sasa, Felix Tshisekedi aliyefariki dunia mwaka 2017

> Inatarajiwa kugharimu zaidi ya billioni 5 za Kitanzania

Soma > https://jamii.app/TshesekediStatue

#JFInternational
HILLARY CLINTON KUTOGOMBEA TENA 2020

> Hillary Clinton ametangaza kuwa hatowania urais ktk uchaguzi ujao wa mwaka 2020 bali ataendelea kuunga mkono na kufanyia kazi kile anachoamini kuwa ni sawa bila ya kushiriki kama mgombea

Soma - https://jamii.app/ClintonOut2020
#JFInternational
MBEGU FEKI ZASABABISHA HALI YA USALAMA WA CHAKULA AFRIKA KUWA MBAYA

> Katibu Mkuu wa Shirikisho la mbegu la kimataifa amesema, kuingia kwa mbegu feki na zisizo na ubora kumefanya hali ya usalama wa chakula Kusini mwa Sahara izidi kuwa mbaya

Soma - https://jamii.app/NjaaAfrikaVsMbeguFeki
#JFLeo
KATAVI: MWANAHABARI WA MAJIRA ADAIWA KUKAMATWA

> George Mwigulu wa Gazeti la Majira amekamatwa wakati akiupiga picha msafara wa Wanawake wa ACT Wazalendo

> Wanawake hao walikuwa katika shamrashamra za kusheherekea siku ya Wanawake Duniani

Soma > https://jamii.app/MwanahabariKatavi

#JFLeo
MOSHI: RAIA WA LIBERIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

> Grace Teta (40), amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukamatwa Desemba 1, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) akisafirisha gramu 10,064 za #DawaZaKulevya aina ya Heroini

Soma - https://jamii.app/LiberianJailedHeroine
#JFLeo
VENEZUELA: UMEME WAKATWA SEHEMU KUBWA YA NCHI

> Rais Nicolás Maduro amewatupia lawama wapinzani wa Serikali yake na kusema wanaijumu nchi

> Wafuasi wake wasema kiongozi wa upinzani, Juan Guaidó anataka kuipindua serikali halali

Soma > https://jamii.app/UmemeWakatwaVenezuela

#JFInternational
WANAUME: JINSI YA KUVAA KWA MTOKO WA USIKU

> Vaa fulana (Tshirt) na suruali ya Jeans ila usivae fulana yenye michoro mingi au urembo mwingi usiokuwa na maana na chini unaweza kuvaa raba

> Unaweza kuvaa suruali ya Jeans na shati halafu juu ukaweka koti la kawaida na si lazima liwe koti la suti

> Vaa shati la kawaida na suruali nyeusi ndiyo itapendeza zaidi. Hakikisha unapata kiatu cheusi au rangi ya ugolo na unaweza ukavaa mkanda au usivae

Zaidi, soma - https://jamii.app/VaziUsikuWanaume
#JFUtanashati
HIZI NDIO NGUVU 7 ALIZONAZO MWANAMKE

> Kuona ya mbeleni, Nguvu katika kinywa chake, Uwezo wa kuendeleza uumbaji, Nguvu ya ushawishi, Kustahimili na kubeba mazito, Uwezo wa kujadili bei na Uwezo wa kuwaathiri watoto kitabia

Soma > https://jamii.app/NguvuMwanamke

#BalanceForBetter
MWILI WA KIM JONG II WAWEKWA KAMA KIVUTIO CHA UTALII

> Serikali ya Korea ya Kaskazini imeuweka hadharani Mwili wa Rais wa zamani, Kim Jong-Il kwa ajili ya watalii na raia wake kumtazama na kuna taratibu maalumu za kuzuru eneo hilo

Soma - https://jamii.app/KimHongIIBodyTourism
#JFInternational
CHANGAMOTO ZA MWANAMKE WA KITANZANIA KATIKA UJASIRIAMALI

> Ikiwa ni siku ya Wanawake Duniani, ndani ya JamiiForums zimechambuliwa baadhi ya sababu zinazomfanya mjasiriamali wa kike asifanikiwe

Kwa mjadala, fungua > https://jamii.app/MwanamkeUjasiriamaliChangamoto

#BalanceforBetter
MUHEZA, TANGA: WATATU WAFARIKI NA WENGINE 54 KUJERUHIWA BAADA YA LORI KUPINDUKA

> Waliofariki na kujeruhiwa ni Wafanyakazi wa kampuni ya Chai ya East Usambara(EUTCO)

> Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Shebomeza

Zaidi, soma => https://jamii.app/AjaliVifoEUTCO

#JFLeo
MIRERANI: WANAWAKE WATAKIWA KUACHA KUFICHA MADINI SEHEMU ZA SIRI

> Wanawake wenye tabia hiyo wetakiwa kuiacha kwani ni hatari kwa afya zao na ni ukwepaji wa kodi

> Watakao kamatwa picha zao zibandikwe ili wasiruhusiwe kuingua mgodini

Soma > https://jamii.app/WanawakeMadini

#JFLeo
RASMI: Kocha wa zamani wa vilabu vya Leicester and Chelsea, Claudio Ranieri(67) ameteuliwa kuinoa klabu ya AS Roma hadi mwisho wa msimu huu

- Alifukuzwa kazi katika klabu ya Fulham siku 8 zilizopita baada ya kushinda michezo 3 kati ya 17 tangu awe kocha wa timu hiyo

#JFLeo