JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WATUMIAJI WA INTANETI TANZANIA NI ZAIDI YA MILIONI 23

> Serikali imesema kuwa idadi ya watumiaji wa Intaneti imeongezeka kutoka 520,000 mwaka 2009 na kufikia zaidi ya watu milioni 23 kwa mwaka 2018 ambayo ni sawa na asilimia 43 ya watanzania

Soma - https://jamii.app/WatumiaIntanetiMil23
#JFLeo
WAHAMIAJI 12 RAIA WA ETHIOPIA WAKAMATWA PWANI

> Wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia, wamekamatwa Mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali kinyume na sheria

> Aidha, watu wengine 14 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi

#JFLeo
TANZIA: DIWANI WA MVULENI, LINDI AFARIKI DUNIA

> Idarous Yusuf Manzi (CUF) amefariki leo, Machi 09 ktk Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar alipokuwa anapatiwa matibabu ya Kifua

> Mazishi yatafanyika kesho, Machi 10 ktk Makaburi ya Kijijini kwao, Kijiweni Mchinga Lindi

#JFLeo
CHAMA CHA WAFANYAKAZI WASHAURI PAYE IPITIWE UPYA

> Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), kimeshauri Serikali kufanya mapitio ya viwango vya kodi ya mtu binafsi kwenye makato ya mshahara ili kuleta unafuu

Soma - https://jamii.app/WafanyakaziMabadilikoPAYE
#JFLeo
RAIS MAGUFULI: MABALOZI KAMA KUNA TATIZO MSIANDIKE MITANDAONI

> Rais Magufuli amewaasa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini kuacha kuandika mitandaoni kama kuna tatizo badala yake wakamuone Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje

Zaidi, soma => https://jamii.app/MagufuliVsMalalamikoMabalozi

#JFLeo
MFUMUKO WA BEI MWEZI FEBRUARI WABAKI 3% HUKU VYAKULA VIKISHUKA BEI

- Ofisi ya Takwimu(NBS) imebainisha kuwa asilimia hizo ni sawa na Januari 2019

- Inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma haijabadilika kwa miezi miwili

Zaidi, soma https://jamii.app/MfumukoBei-Feb2019
IRAN: WAPENZI WAKAMATWA BAADA YA KUCHUMBIANA HADHARANI

- Ni kwa kukiuka maadili ya kidini ambapo kuonesha hadharani mapenzi kumepigwa marufuku nchini humo

- Polisi imedai kitendo hicho kimechochewa na utamaduni wa mataifa ya Magharibi

Zaidi, soma https://jamii.app/MbaroniKuchumbianaHadharani-IRN
TCRA YAFICHUA ‘MADUDU’ VITUO VYA REDIO KANDA YA ZIWA

> Yawapa miezi 4 kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyobainika walipofanya ukaguzi kwenye vituo takribani 36

> Wafanyakazi hawana mikataba, wana elimu zisizokidhi na baadhi ya vituo havina vyoo

Zaidi, soma https://jamii.app/TCRA-RedioKandaZiwa
COLOMBIA: WATU 14 WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE

- Imepata ajali jana huko San Carlos de Guaroa ikiwa inatokea San Jose del Guaviare kuelekea Villavicencio

- Ni muda mchache baada ya rubani kutuma ishara ya dharura kwa kituo cha udhibiti

Zaidi, soma https://jamii.app/14WafaAjaliNdege-CLMB
NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA YAPATA AJALI, WENGI WAHOFIWA KUFARIKI

- Boeing 737 imepata ajali ikiwa safarini kutoka Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya

- Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege hiyo ilikuwa na abiria 149 pamoja na Wafanyakazi 8

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
WATU WOTE KWENYE NDEGE ILIYOPATA AJALI LEO ETHIOPIA WAFARIKI

> Ni 157, idadi ikijumuisha abiria 149 na wafanyakazi 8 wa ndege

> Imetajwa kuwa na raia kutoka nchi 33 tofauti

> Sababu za ajali bado hazijafahamika

Zaidi, soma https://jamii.app/ETHAirlines-Boeing737Crashes
ALGERIA: WANAFUNZI WA VYUO WAPEWA LIKIZO YA MAPEMA

- Ni ili kudhoofisha maandamano ya Wanafunzi hao ambao wanapinga Rais Abdelaziz Bouteflika kugombea kwa muhula wa 5

- Likizo hiyo huwa ya wiki 2 kuanzia Machi 21 hadi Aprili 5 kila mwaka

Zaidi, soma https://jamii.app/VyuoVyafungwaMapemaALG
MANUFAA YA KULA WADUDU KIAFYA NA KIMAZINGIRA

> Wana virutubisho karibu vyote yaani protini, madini mengi na asidi za amino

> Pia wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazoongeza joto duniani, hawahitaji maji mengi wala eneo kubwa la kuwafuga

Zaidi, soma https://jamii.app/FaidaKulaWadudu
SERIKALI: WAPINZANI WANAOMTUKANA RAIS KWENYE VIKAO VYA NDANI WAKAMATWE

- Waziri Lugola ametoa agizo hilo kwa Polisi akiwataka washirikiane na Wakuu wa Mikoa na Wilaya

- Asema baadhi ya wapinzani wanatukana, wanabeza na kuchonganisha Wananchi na Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/WapinzaniWanaotukanaWakamatwe
SHINYANGA: AUAWA KATIKA UGOMVI WA RABA

> Daniel Gudugudu(30) ameuawa kwa kuchomwa kisu kwenye mkono wa kushoto na Rashid Mustapha(48) huko Nyihogo wilayani Kahama

> Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na kudaiana viatu aina ya raba zenye rangi nyeusi

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiKisuSHY
NHC KUWAFUKUZA WADAIWA SUGU KATIKA MAJENGO YAKE

- Ni kwa wale walioshindwa kulipa kodi ya pango ya jumla ya Tsh. Milioni 44.3

- Ni mpango wa kutaka kumaliza kukusanya kodi ambapo hadi sasa shirika limekusanya zaidi ya Tsh. Bilioni 1.9(73%)

Zaidi, soma https://jamii.app/WadaiwaNHCKuondolewa
TUNISIA: WAZIRI AJIUZULU KUTOKANA NA VIFO VYA WATOTO

> Waziri wa Afya, Abdurrauf esh-Sherif amejiuzulu baada ya kutokea vifo 11 vya watoto ktk Hospitali ya Serikali mjini Tunis

> Uchunguzi unafanyika kubaini sababu ya vifo hivyo

Soma - https://jamii.app/WaziriAjiuzuluVifoWatoto
#JFInternational
SERIKALI YATAKA TAARIFA ZA WAAJIRI WALIOFUKUZA KAZI WANAWAKE BAADA YA KUPATA UJAUZITO

> Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametaka apewe taarifa hasa za sekta binafsi za waliowafukuza Wanawake kazi au kuwashusha vyeo kwa sababu wamepata ujauzito

Soma > https://jamii.app/UjauzitoKazi

#JFLeo
CHINA, ETHIOPIA ZASITISHA KUTUMIA BOEING 737 MAX 8

> China imeyaamuru mashirika ya ndege ya ndani ya nchi kusimamisha matumizi ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 kufuatia ajali iliyotokea Ethiopia na nyingine nchini Indonesia

> Shirika la ndege la Ethiopia nalo limetangaza kusitisha safari za ndege zake zote aina ya Boeing 737 Max 8 kuanzia Machi 10 mwaka huu kama tahadhari ya ziada licha ya kuwa bado chanzo cha ajali iliyotokea jana na kuua watu 157 bado hakijafahamika mpaka sasa

Soma - https://jamii.app/ChinaBansBoeing737
#JFInternational