JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PEMBA: MELI YA SEASTAR YAPATA HITILAFU, ABIRIA WASHUSHWA

> Abiria wa meli hiyo wameshushwa Wete baada ya kutokea mlipuko mdogo kwenye moja ya mashine zake

> Mpaka sasa haijaelezwa mlipuko huo umesababishwa na nini

Zaidi, soma => https://jamii.app/MeliSeastarPemba

#JFLeo
KAGERA: RUGE MUTAHABA KUZIKWA, KIJIJINI KIZIRU

> Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele leo

> Uongozi wa Clouds Media Group watangaza kuzima vituo vyake kwa dakika 3 wakati mwili wa Ruge ukishushwa kaburini

#RIPRuge #RIPRugeMutahaba
Kutoka Kabale K’Omukama
UINGEREZA: KIONGOZI WA UPINZANI JEREMY CORBYN APIGWA NA YAI

> Kiongozi wa chama cha Labour alikuwa kwenye ziara ya kutembelea kituo cha Waislamu kilichopo Kaskazini kwa Jiji la London

> Mwanaume Mmoja amekamatwa akihusishwa na tukio hilo

Soma > https://jamii.app/EggCorbyn

#JFInternational
ZAMBIA: SERIKALI YAKIFUNGIA KITUO CHA RUNINGA KUFUATIA MALALAMIKO YA CHAMA TAWALA

> Prime Tv imefungiwa kwa siku 30 baada ya kukalamikiwa na chama tawala cha Patriotic Front (PF)

> Chatuhumiwa kuendesha propaganda chafu dhidi ya Serikali

Soma > https://jamii.app/PFvsPrimeTv

#JFLeo
KENYA: RUBANI WA RUTO NA RAIA 4 WA MAREKANI WAFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE

> Sababu za ajali hiyo iliyoondoa uhai wa Mario Magonga na Wamarekani hao bado hazijawekwa wazi

> Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada wakati ikiwa ziwa Turkana

Soma > https://jamii.app/AjaliRubaniRuto

#JFLeo
BASI LA BM COACH LAPINDUKA LIKIJARIBU KUKIKWEPA KICHWA CHA TREN, DEREVA AJERUHIWA VIBAYA

> Ajali hiyo imetokea Chekelei Wilaya ya Korogwe, Tanga wakati basi hilo likiwa safarini kutoka Arusha - Morogoro

> Abiria wachache wamejeruhiwa

Soma => https://jamii.app/AjaliBMTanga
ELIMU YA URAIA: ASKARI POLISI WANAFANYA KAZI HATARISHI. JE, WANA BIMA?

> Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania hawana bima ya maisha ila wana bima ya afya ambayo haikidhi haja kulingana na hatari zinazowakabili

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace #JFLeo
JE, UNAIJUA SHERIA YA TAKWIMU YA MWAKA 2015 INAYOLALAMIKIWA NA WADAU?

> Inaelezwa kuwa inakinzana na kanuni za uwazi wa taarifa na takwimu pamoja na uendeshaji wa Serikali kwa uwazi

> Sheria hii inaipa namlaka NBS kuwa chombo pekee cha kusimamia na kutoa takwimu

#JFCivicSpace
HOMA YA DEGEDEGE, VISABABISHI NA WANAOATHIRIKA

> Degedege ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono, ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili

> Hutokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano

> Kama mama au baba aliwahi kuumwa ugonjwa huu basi mtoto ana asilimia 10-20 zaidi ya kuumwa ugonjwa huu

Tembelea - https://jamii.app/UfahamuDegedege
#JFAfya
FAHAMU KUHUSU KILIMO CHA MAPAPAI NA YA KUZINGATIA KATIKA KILIMO CHAKE

> Ekari moja ya papai inachukua miche 1,000 hadi 1,200 kwa maana ya mita 2×2 kutoka mti hadi mti kwa mbegu fupi

> Kuanzia kupanda hadi kuanza kuvuna huchukua miezi 8 hadi 10

> Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropiki ambayo haina baridi kali na joto kiasi

> Udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji kwasababu maji yakisimama kwa saa 48 tu mpapai unaweza kufa

Zaidi, soma - https://jamii.app/KilimoMapapai
#JFKilimo
FAHAMU KUHUSU CHEMBE YA MOYO NA VISABABISHI VYAKE

> Chembe ya moyo (Angina Pectoris) ni tatizo linalotokea pale moyo unapopata hewa ya Oksijeni kidogo tofauti na mahitaji yake

> Inaelezwa kuwa Watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ni; Wanaovuta sigara, Wanene kupita kiasi na wenye ugonjwa wa kisukari

> Dalili kubwa ni maumivu katikati ya kifua yanayokua kuelekea kwenye mkono wa kushoto

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UgonjwaChembeMoyo
#JFAfya
NDEGE ZA ISRAEL ZAISHAMBULIA NGOME YA HAMAS

> Ndege za kijeshi za Israel zimeishambulia ngome ya Hamas Kaskazini mwa Gaza

> Hatua hiyo imekuja baada ya Hamas kuulipua upande wa Israel katika eneo la Gaza

Soma - https://jamii.app/IsraelVsHamasGaza
#JFInternational
MAWAZIRI WA FEDHA AFRIKA WAKUTANA KUJADILI HATUA NA SERA ZA KIUCHUMI

> Mawaziri wa fedha na wataalamu wa nchi za Afrika wamekutana Yaoundé, Cameroon kwenye mkutano wa siku 5, kujadili sera na hatua zinazohitajika kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya kiuchumi

#JFInternational
PUTIN ASITISHA MKATABA WA UTEKELEZAJI WA SILAHA ZA NYUKLIA

> Rais Vladimir Putin amesaini amri ya kusitisha mara moja utekelezaji wa Mkataba wa Silaha za Nyuklia za masafa ya Kati(INF) hadi Marekani itakapoacha kupuuza wajibu wake

Soma - https://jamii.app/PutinSuspendsNuckearTreaty
#JFInternational
FAHAMU HAYA KUHUSU IPTV (KUANGALIA RUNINGA KWA KUTUMIA INTANETI)

> Hii ni aina ya uangaliaji runinga kupitia mtandao (intaneti) ambapo kituo cha runinga badala ya kutumia satelite dish au cable wenyewe wanarusha matangazo kwa intaneti

> Utahitaji kifaa chenye intaneti na uwezo wa kurusha matangazo ili kuweza kuangalia kama vile simu janja (smartphone), kompyuta au runinga zenye intaneti (smart tv)

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/UfahamuTvIntaneti
#JFTeknolojia
SERIKALI: MARUFUKU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRISHA MIZIGO NA BARUA

> Ni marufuku kusafirisha vifurushi na barua bila ya kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA)

> SUMATRA imeagizwa kuendesha oparesheni kali ili kudhibiti vitendo hivyo

Soma > https://jamii.app/GvtVsUsafirishajiMizigo

#JFLeo
MAREKANI: MGONJWA WA PILI WA UKIMWI APONA

> Wanasayansi wamefanikiwa kumtibu mgonjwa wa pili aliyeathirika na VVU tangu ugonjwa huo uanze kuathiri Wanadamu miaka ya 1980

> Mchakato wa kutengeneza tiba hiyo umechukua takribani miaka 12

Soma > https://jamii.app/USTibaHIV

#JFLeo
NEC YAONGEZA VITUO 858 VYA KUPIGIA KURA

> Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage leo Machi 5 amesema wameongeza vituo vya kupigia kura 858 na kufanya idadi ya vituo kupanda kutoka 36,549 hadi 37,407

> Ni maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 2020

Soma - https://jamii.app/OngezekoVituoKura
#JFLeo
UCHAGUZI YANGA SASA KUFANYIKA MACHI 10, 2019

> Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Yanga, uliosimamishwa kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi Mahakamani, sasa umepangwa kufanyika Machi 10

> Awali, ulipangwa kufanyika Januari 13, 2019

Soma - https://jamii.app/UchaguziYangaMachi10
#JFMichezo