JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBOWE NA MATIKO WARUDISHWA MAHABUSU KUSUBIRI RUFAA YA DPP

> Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe(Mbunge wa Hai) na Esther Matiko(Mbunge wa Tarime Mjini) warejeshwa gerezani kusubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu maombi yao ya dhamana

Zaidi, soma => https://jamii.app/MboweMatikoVsDPP
SUDAN KUSINI: GESI ILIYOTUMIKA KUWATAWANYA WAANDAMANAJI YASABABISHA KIFO

> Mwanaume muuza matunda ndani ya Mji wa Khartoum amefariki kwa kile kinachoelezwa kuwa alivuta gesi ya kutoa machozi iliyotumika kuwatawanya waandamanaji

Soma =>https://jamii.app/GesiKifoSudan

#JFInaternational
UINGEREZA: WABUNGE 7 WA CHAMA CHA LABOUR WAJIUZULU

> Wabunge saba kutoka Chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza (Labour) wamejiuzulu kutokana na kutokukubaliani kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya na vita dhidi ya ubaguzi

Soma - https://jamii.app/7PMsResignUK
#JFInternational
AFYA: UFAHAMU UGONJWA WA PUMU

> Ugonjwa wa pumu huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu zinazojulikana kama ''bronchioles''

> Kupitia JamiiForums, ipo mada inayochambua zaidi kuhusu ugonjwa huu

Zaidi, soma > https://jamii.app/UgonjwaPumu

#JFAfya
TANZANIA YATAJWA KUWA NA KIWANGO KIKUBWA CHA KODI KATIKA SEKTA YA MADINI

> Taarifa hii imetolewa na taasisi inayoshughulika na usimamizi wa rasilimali za asili na maendeleo endelevu dunia (NRGI)

> Imeleeza kuwa kiwango cha kodi kwa Tanzania ni asilimia 74

Soma => https://jamii.app/KodiMadiniTz
IJUE SHERIA: Je, naweza kumwita Askari Polisi wakati wowote ninapohitaji?

> Unapaswa kuwaita Askari Polisi kwa malalamiko au taarifa zinazohusu uhalifu muda wowote hata usiku wa manane

> Unaweza kuwaita Polisi kwa njia ya simu namba 112

Soma > https://jamii.app/Mambo101Polisi
#JFCivic
HALI YA RUGE MUTAHABA: MSAADA WA HALI NA MALI WAHITAJIKA TOKA KWA YEYOTE ATAYEGUSWA

> Mbaki Mutahaba(mdogo wa Ruge Mutahaba) amesema gharama za matibabu ni kubwa mno

> Kwa atayeguswa kuchangia matibabu ya Ruge Mutahaba wameombwa kufanya hivyo kupitia namba 0752 222 210

#JFLEO
WATUMISHI 3 WIZARA YA MADINI KUSIMAMISHWA KAZI

> Waziri wa Madini, Doto Biteko amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuwasimamisha na kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 3 kwa kugawa leseni za uchimbaji wa madini bila kufuata utaratibu

Soma https://jamii.app/WatumishiKusimamishwaKazi
KENYA: MBARONI KWA KUTAKA KUMTOROSHA MTOTO HOSPITALINI

> Bonface Murage Wangechi (22) amekutwa hatiani kwa kutaka kumtorosha mtoto wake baada ya kushindwa kulipa fedha za matibabu kwenye Hospitali ya Taifa, kiasi cha Ksh 56,937

Soma - https://jamii.app/ArrestedHospitalBill
IRAN YAZINDUA NYAMBIZI MPYA YENYE MAKOMBORA YA 'CRUISE'

> Rais Hassan Rouhani amezindua Nyambizi ya kisasa (Fateh) yenye uzito wa tani 527 na uwezo wa kubeba makombora ya cruise

> Inaweza kwenda mita 200 chini ya bahari kwa wiki 5

Soma- https://jamii.app/IranCruiseMissile
DAR: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MWANAMKE WA MIAKA 32

> John Julius mwenye umri wa miaka 33 anatuhumiwa kumbaka Ester Michael(32), Januari 26 2019

> Akana mashtaka na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutumiza masharti ya dhamana

Soma > https://jamii.app/MahakamaniUbakaji32
MAREKANI: MAJIMBO 16 YAUSHTAKI UTAWALA RAIS TRUMP

> Muungano wa majimbo 16 nchini Marekani yameushtaki utawala wa Rais Donald Trump kuhusu uamuzi wa kutangaza hali ya dharura ili kukusanya fedha za ujenzi wa ukuta mpakani na Mexico

Soma- https://jamii.app/MajimboYamshtakiTrump
UGANDA: KODI YA MITANDAO YA KIJAMII YAPUNGUZA WATUMIAJI MILIONI 5 NDANI YA MIEZI 6

> Kodi hii kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ilitambulishwa mwezi Julai 2018 imetajwa kupunguza watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo

Zaidi, soma => https://jamii.app/UgandaSMTax
WANANCHI WA MBEYA WAINGIWA NA HOFU JUU YA MATUKIO YA UBAKAJI

> Wananchi wa Mbalizi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, wameripoti kuwa, Februari 14 binti wa darasa la 7 alibakwa na mabinti wengine 3 walinusurika kubakwa Jumapili wakiwa Kanisani

Soma - https://jamii.app/UbakajiWatotoMbeya
KENYA: MUME AUA MKEWE BAADA YA KUKATAA KUMPIKIA UGALI

> Mwanaume mmoja(45) katika Kaunti ya Kakamega amenusurika kifo kwa kunywa sumu baada ya kumuua mkewe kisa kikiwa ni kukataa kumpikia ugali

> Alimvamia mkewe kwa kutumia kisu

Soma - https://jamii.app/ManKillsWifeOverUgali
ELIMU YA URAIA: NINI MAANA YA AMRI NA HATI YA UPEKUZI?

> Amri ya Upekuzi (Search Order) ni kibali kitolewacho na Mkuu wa Kituo cha Polisi

> Wakati Hati ya Upekuzi (Search Warrant) ni kibali kitolewacho na Mahakama

Zaisi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivic
UPDATE: Mahakama nchini Kenya yamwachilia huru Boniface Wangeci, baba aliyetaka kumtorosha mtoto wake Hospitali ya Taifa Kenya (KNH) ili kukwepa kulipa pesa ya matibabu kiasi cha Ksh 56,000

> Amepewa miezi 3 kudhihirisha kwa vitendo kuwa hakusudii kujitia hatiani tena
#JFInternational
MALKIA WA MENO YA TEMBO NA WENZAKE WAKUTWA NA HATIA

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani raia wa China, Yang Feng Glan(66) na wenzake 2 baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa katika kesi yao ya kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo

> Imewahukumu kifungo cha miaka 17 jela kila mmoja

Zaidi, soma https://jamii.app/MalkiaMenoTemboHatiani
TANZANIA YAPEWA SIKU 45 KUJIBU KUHUSU MATOKEO YA UCHAGUZI KUPINGWA MAHAKAMANI

> Mahakama ya Afrika ya haki za binaadamu (ACHPR) imeipa siku 45 Serikali ya Tanzania kutoa utetezi wake juu ya, kwanini matokeo ya Urais hayapingwi Mahakamani?

Soma - https://jamii.app/ACHPRVsTZGovernment
KESI YA MWANARIADHA CASTER SEMENYA YAANZA KUSIKILIZWA

> Mwanariadha huyo(SA) anapinga Sheria zinazopendekezwa na Shirikisho la Riadha Duniani kuhusu viwango vya Homoni ya testosterone kwa wanariadha ktk Mahakama ya michezo

Soma - https://jamii.app/SemenyaVsIAAFCourt