JamiiForums
โœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AJALI YAUA TAKRIBAN WATU 18: Watu wapatao 18 wamefariki dunia baada ya basi dogo (Coaster) kugongana na lori la mizigo Mkoani Iringa

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Allan Bukumbi amethibitisha ajali kutokea leo Juni 10, 2022

Soma - https://jamii.app/AjaliIringa

#JFLeo
๐Ÿ˜ข27๐Ÿ‘6๐Ÿ‘Ž2๐Ÿ˜ฑ1
#ZIMBABWE: Mamia ya Watumishi wa Umma wa Sekta ya #Afya wamefanya Mgomo kutokana na mishahara midogo na mazingira duni ya Kazi

> Inaelezwa Serikali imetangaza kuongeza mishahara kufikia Mwezi Julai, kiwango ambacho bado wanadai hakiridhishi

Soma - https://jamii.app/MgomoZimbabwe

#JFLeo
๐Ÿ‘10๐Ÿ”ฅ1
SERIKALI YAENDELEZA MARUFUKU YA โ€˜LUMBESAโ€™

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango amezuia vipimo visivyo rasmi ktk ununuzi wa mazao ikiwemo โ€˜lumbesaโ€™

Hii si mara ya kwanza โ€˜lumbesaโ€™ kuzuiwa. Waziri Mkuu Majaliwa aliizuia akisema inatumika kuwaibia Wakulima

Soma https://jamii.app/Mpango-lumbesa

#JFLeo
๐Ÿ‘10
RIPOTI MAUAJI WATU 33 MALI: UN wameeleza Wanajeshi wa #Mali na Wanamgambo wa Kundi la Wagner la Urusi ndio waliua raia 33 (29 wa Mauritania, 4 wa Mali)

Tukio hilo la Machi 5, 2022 lilisababisha mvutano kati ya Nchi ya Mali na #Mauritania

Soma > https://jamii.app/RipotiYaUN

#JFLeo
๐Ÿ‘6๐Ÿค”1
Wakiongozwa na Misri, #Israel na #Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa #Gaza yaliyofanyika kwa Siku tatu mfululizo

Watu 44 wameuawa ambapo kati yao Watoto ni 15, huku Wapalestina 350 wakijeruhiwa

Soma > https://jamii.app/IsraelGazaChaos

#JFLeo #GazaUnderAttack
๐Ÿ‘6
TANGA: Miili ya Watu wawili imeokotwa ikiwa imefungwa ndani ya Mifuko ya Sandarusi (viroba) katika Kitongoji cha Dibabara

Mashuhuda wanadai waliona Gari - Toyota Landcruiser eneo la tukio na baada ya kuondoka wakabaini uwepo wa Miili hiyo

Soma > https://jamii.app/TukioTanga

#JFLeo
๐Ÿค”14๐Ÿ‘4๐Ÿ˜ข3
MAREKANI: RAIS BIDEN ASAINI MUSWADA WA KODI, AFYA NA TABIA NCHI KUWA SHERIA

Rais #JoeBiden ametia saini Muswada wa Dola Bilioni 700 ambao unalenga kupambana na Mabadiliko ya #TabiaNchi na gharama za #Afya huku akipandisha kodi kwa Matajiri

Soma - https://jamii.app/BidenSheria

#JFLeo
๐Ÿ‘6๐Ÿ˜1
RC TANGA: WALIOWEKA MIILI KWENYE VIROBA WATAKUWA WAZOEFU WA UHALIFU

RC Omari Mgumba amesema Miili ilikunjwa kama ipo ktk viroba vya Kilo 20 na kuongeza kuwa dalili za awali zinaonesha mauaji hayajafanyika Tanga bali pametumika kuitupa Miili

Soma > https://jamii.app/MauajiTanga2022
#JFLeo
๐Ÿ‘5
PWANI: 21 WASHIKILIWA KWA KUHUSIKA NA MTANDAO WA WIZI

Wanaoshikiliwa wanatuhumiwa kwa wizi uliotokea Julai 27, 2022 eneo la Mkenge

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuiba Ngโ€™ombe 8 na kuumua mmoja wa Walinzi wa Zizi huku wakimjeruhi Mlinzi mwingine

Soma https://jamii.app/WeziMifugo
#JFLeo
UGANDA: Watu 14 wamefariki Dunia ktk Mji wa #Arua baada ya kudaiwa kunywa Pombe aina ya City 5 inayodhaniwa kuwa na sumu

Watu 4 wanashikiliwa kufuatia vifo hivyo, huku Kiwanda kinachotengeneza Pombe kikifungwa hadi uchunguzi utakapokamilika

Soma - https://jamii.app/14PeopleDie
#JFLeo
๐Ÿ‘4
TRA imewataka Wapangaji wa nyumba kuwa Wazalendo na kulipia 10% ya kodi wanazowalipa wenye nyumba ili kulipia kodi ya pango

Agosti 20, 2021 Wananchi walianza ulipaji wa Kodi ya Majengo kupitia manunuzi ya mfumo wa LUKU

Soma https://jamii.app/WapangajiKodi

#JFLeo
๐Ÿค”14๐Ÿ‘4
KAMATI YA BUNGE (PIC) YABAINI MATUMIZI MAKUBWA NHIF

- Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imebaini Mfuko wa Taifa wa Bima ya #Afya una matumizi makubwa mno na udhaifu ktk Mifumo ya TEHAMA unaochangia kuwepo kwa udanganyifu

Soma - https://jamii.app/NakisiNHIF
#JFLeo
๐Ÿ‘5
DODOMA: Jeshi la Polisi limethibitisha kuuawa kwa Nada Songo (45) kwa Risasi baada ya kuwashambulia Askari na Wananchi kwa mishale iliyodhaniwa kuwa na sumu

- Marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa kwa tuhuma za kutishia kuua Agosti 27, 2022

Zaidi - https://jamii.app/AuawaNaPolisi

#JFLeo
๐Ÿ‘7
KENYA: #RailaOdinga amesema ana ushahidi thabiti kwamba alishinda Urais na ana imani Mahakama ya Juu itakubali ombi lake la kutengua matokeo ya Uchaguzi

Asema uamuzi wa Mahakama unaweza kuwa na athari kubwa ktk michakato ya Uchaguzi Afrika

Soma - https://jamii.app/MatokeoOdinga

#JFLeo
๐Ÿ‘18๐Ÿค”1
#SENSA2022: Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anne Makinda amesema Wananchi ambao hawajahesabiwa, wafike Ofisi za Serikali za Mitaa au Watendaji na kuacha Mawasiliano yao

> Taarifa zao zitawezesha Makarani kuwafuata walipo na kuwahesabu

Soma - https://jamii.app/Sensa7

#JFLeo
๐Ÿ‘4โค1
NJOMBE: Mahakama ya Wilaya ya Ludewa imemhukumu kifungo cha Miaka 5 jela John Chale (60) kwa kosa la kumfanyia vitendo vya kishirikina Mpwa wake, Videana Chale(18) na kupelekea kupata ukichaa

Pia, anadaiwa kumiliki Nyoka Nyumbani kwake

Soma - https://jamii.app/JelaUshirikina

#JFLeo
๐Ÿ‘5๐Ÿ‘Ž3๐Ÿ˜3๐Ÿค”2
#MADAGASCAR: POLISI WAUA WATU 18 KWENYE MVUTANO NA RAIA

Takriban Watu 500 wenye visu na mapanga walijaribu kuingia kwa nguvu kwenye kituo cha Polisi ambako washukiwa wa utekaji nyara wa Mtoto mwenye Ulemavu wa Ngozi walikuwa wakishikiliwa

Soma - https://jamii.app/18DeadMDG

#JFLeo
๐Ÿ‘5
WAZIRI UMMY: NHIF INAKARIBIA KUFA

Waziri wa #Afya amesema Mfuko huo umeelemewa na madeni makubwa ya Matibabu ya Wanachama

Sababu za kuelemewa kuwa ni ongezeko la madai yanayohusu Magonjwa yasiyoambukiza yanayochangia 71% ya vifo Duniani

Soma - https://jamii.app/NHIFDies

#JFLeo
๐Ÿ‘Ž10๐Ÿคฏ3๐Ÿ‘1
RIPOTI: BANGI INATUMIWA ZAIDI TANZANIA

Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya #Tanzania (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Dawa ya Kulevya inayotumiwa zaidi Nchini ni Bangi ikifuatiwa na Heroine

Soma > https://jamii.app/RipotiYaBangi

#JFLeo
๐Ÿ‘7๐Ÿ˜ฑ2๐Ÿ”ฅ1๐Ÿ‘1๐Ÿคฏ1
TANESCO imetangaza mgao wa Umeme katika baadhi ya Mikoa Nchini kwa vipindi tofauti kuanzia Saa 2 asubuhi hadi 4 Usiku 

Hii ni kutokana na ukarabati wa mitambo na Kupungua kwa kina cha Maji katika Vituo vya kufua Umeme vya Pangani na Kihansi

Zaidi https://jamii.app/PowerCrisis

#JFLeo
๐Ÿคฎ10๐Ÿ˜ข7๐Ÿ‘Ž4๐Ÿ‘3๐Ÿ’ฉ3๐Ÿ˜1