JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MTWARA: WAUGUZI WAFUTIWA LESENI KWA KUSABABISHA KIFO CHA MJAMZITO

Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limechukua uamuzi huo kwa wauguzi wasaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkomaindo ambao ni Elizabeth Njenga na Pascal Mnyalu

Soma https://jamii.app/KifoChaMjamzito

#JFUwajibikaji
πŸ‘5πŸ€”4
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege #Zanzibar (ZAA) inadaiwa kuiteua Kampuni ya DNATA toka nchini Dubai kuwa mtoa huduma pekee katika jengo la tatu la (Terminal III) la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume

Kutokana na hatua hiyo Wafanyakazi karibu 600 wapo katika hatari ya kupoteza Ajira katika Kampuni ya huduma za Uwanja wa Ndege (ZAT) pamoja na Kampuni ya Trans Word zinazotoa Huduma Uwanjani hapo.

Soma https://jamii.app/ZnzAirport

#Governance
πŸ‘12πŸ‘Ž12πŸ€”4
CHAD: WATU 50 WAUAWA NA 300 WAJERUHIWA KATIKA MAANDAMANO

Serikali imesema baadhi ya Waandamanaji walikuwa na silaha na kati ya waliouawa ni Askari wa Vikosi vya Usalama

> Amri ya Kutotoka Nje imetangazwa katika Miji mitatu

Soma https://jamii.app/ChadChaos

#Democracy
πŸ‘3
ASTON VILLA YAMFUTA KAZI STEVEN GERRARD

Ni baada ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa Fulham katika mchezo wa Premier League

Villa imeshinda mechi 2 za EPL kati ya 11 msimu huu, pia ni kati ya timu 4 za mwisho katika msimamo wa ligi hiyo

Soma https://jamii.app/VillaGerrard

#JFSports
πŸ‘7
#Indonesia imesitisha uuzaji wa Dawa za Kutibu kifua kufuatia vifo vya Watoto 99 huku kukiwa na visa 206 vya majeraha ya papohapo ya Figo kwa Watoto

Dawa hizo ni #Promethazine Oral solution, Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold syrup

Soma https://jamii.app/DawaMaumivuFigo

#JFAfya
πŸ‘6
RIPOTI YA KIKOSI KAZI: Rais Samia Suluhu anapokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, Ikulu-Dar, Oktoba 21, 2022

Prof. Rwekaza Mukandala, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi anasema β€œKikosi kazi kinapendekeza Mikutano ya Hadhara na ya Ndani ya Vyama vya Siasa iruhusiwe.”

#Democracy
πŸ‘9
RIPOTI YA KIKOSI KAZI: MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA IRUHUSIWE

Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, Prof. Rwekaza Mukandala, amesema Kikosi hicho kinapendekeza Mikutano ya Hadhara ya Vyama vya Siasa iruhusiwe, pia mikutano ya ndani ya vyama hivyo

Pia, Sheria ya Vyama vya Siasa itamke kuwa 20% ya fedha za ruzuku inayotolewa na Serikali kwa Vyama vya Siasa katika mwaka wa fedha igawiwe kwa Vyama vyenye Madiwani wa kuchaguliwa kwa idadi ya Madiwani ambao wapo kwenye Chama

Aidha, Kikosi kimependekeza Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi isiyolazimika kufuata amri ya yeyote, na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa Mahakama ya Juu

#JamiiForums #Democracy #KikosiKazi
πŸ‘16πŸ‘Ž1πŸ”₯1
RIPOTI YA KIKOSI KAZI: IWEPO KAMATI YA UTEUZI, VITI MAALUM KUWE NA UKOMO WA MUDA

#KikosiKazi kimependekeza Kamati ya Uteuzi itakayokuwa na MwenyeKiti ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Makamu Mwenyekiti ambaye ni Jaji Mkuu wa Zanzibar na Wajumbe wengine

Kuhusu utaratibu wa kuwa na Viti Maalum vya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani Wanawake uendelee, isipokuwa Sheria iweke Ukomo wa Miaka 10 ili iwe njia ya kupata uzoefu na kuwapa nafasi wengine

#Democracy #JFDemokrasia
πŸ‘14πŸ‘Ž6πŸ”₯2
KENYA: Maafisa 21 wa Kitengo Maalumu cha Upelelezi (SSU) wanaodaiwa kuua Watu, wametaka aliyekuwa Kiongozi wao ahojiwe kwasababu walifanya kazi kwa maagizo yake

> DCI George Kinoti alijiuzulu baada ya Serikali mpya kuingia Madarakani

Soma https://jamii.app/SSUSagaKE

#SocialJustice
πŸ‘15
KIKOSI KAZI: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UENDELEE, RUSHWA ITAJWE KWENYE KATIBA

Kimependekeza Mchakato wa #Katiba Mpya uendelee, Mjadala wa Kitaifa kuhusu Katiba hiyo uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuiandika ili kujadili ajenda muhimu za Muungano, Mamkala ya Rais, Rushwa, Tume ya Uchaguzi n.k

Pia, #Rushwa itamkwe katika Katiba ya Nchi ili Wananchi watambue Vitendo vya namna hiyo havitavumiliwa na Katiba ya Chama cha Siasa iwe na adhabu ya kumuondoa katika Mchakato wa Uchaguzi Mgombea aliyedhaminiwa na Chama akithibitika kuhusika na vitendo vya Rushwa

#Accountability #KemeaRushwa #Democracy
πŸ‘11πŸ”₯3
RAIS SAMIA: RUSHWA NI KIDONDA NDUGU, TUJIANGALIE SOTE

Akitoa Majibu ya baadhi ya Mapendekezo ya #KikosiKazi, Rais Samia Suluhu amesema, β€œRushwa ni kidonda Ndugu, hakuna hata Chama kimoja kimenusurika hapa. Hakuna Chama ambacho hakifanyi, nadhani ni tabia ambayo tunatakiwa kuibadilisha. Watu wajue kuchaguliwa si mimi, ni Chama. Tujitazameni sote"

Kuhusu Zuio la Mikutano ya Vyama Vya Siasa amesema, β€œSuala la Mikutano hakuna anayekataa, lakini lazima kuwe na jicho. Hatutaki kurudi tulipotoka. Tukifanya Mikutano kwa sheria na kanuni hizi Polisi wataingia tena kupiga Watu kwasababu ndivyo sheria inavyomwambia

#JamiiForums #Democracy #KemeaRushwa
πŸ‘7
DAR: Hawa Mwaifunga shahidi upande wa Wabunge 19 wanaopinga kuvuliwa Uanachama na CHADEMA ameshindwa kutoa ushahidi baada ya kuugua Mgongo akiwa Mahakamani

> Kesi imeahirishwa hadi Novemba 3,4,8 na 9 na kurudi tena Desemba 6 na 7, 2022.

Soma https://jamii.app/ShahidiCDM

#JFSiasa
😁21πŸ‘3πŸ‘Ž1
WAZIRI MAKAMBA: TUMEKUWA WAKWELI, BWAWA LA NYERERE LITAISHA JUNI 2024

Amesema hawaoni aibu kusema litaenda miaka miwili mbele kwasababu isingewezekana kukamilika Juni 2022

> Hadi kufikia 2021 ujenzi ulikuwa 37%, Okt. 2022 umefika 74%

Soma https://jamii.app/MakambaJNHPP

#JFGovernance #Uwajibikaji
😁21πŸ‘11πŸ‘Ž4
MSUMBIJI: RAIS FILIPE NYUSI ATOA MSAMAHA KWA MAGAIDI 25

Ni waliojisalimisha kwa hiari baada ya Majeshi ya Msumbiji, Rwanda na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuingilia kati kudhibiti vitendo ya Ugaidi eneo hilo

Soma https://jamii.app/NyusiMagaidi

#HumanRights
πŸ€”7πŸ‘Ž6πŸ‘1
SIMIYU: Levinus Kidanabi amehukumiwa kwenda Jela Miaka 7 na faini Tsh Mil 15 kwa Makosa 2 ya kumkashifu Rais Samia kupitia kundi la WhatsApp

> Pia, amekutwa na Laini ya Simu isiyo na usajili wake bila Kibali cha TCRA

Soma https://jamii.app/JelaKashfa

#DigitalRights
πŸ‘Ž12πŸ”₯7πŸ‘5πŸ‘1
MAKETE, NJOMBE: WAZAZI WAWATISHIA WATOTO KIFO ILI WASIFAULU MITIHANI YA DARASA LA 7

Baadhi ya Wazazi wamewaaminisha Watoto wao kuwa kufanya kwao vizuri kutawafanya Wazazi wafariki kwa kuwa watashindwa kumudu gharama za kuwasomesha

Soma https://jamii.app/ElimuKwaWatoto

#HakiMtoto
😁10😱7πŸ€”4πŸ‘3
#JFAFYA: Ugonjwa wa Homa ya Manjano husababishwa na vimelea vya Virusi kutoka #Genus (jinasi) ya #Flavivirus ambao huenezwa na Mbu

Dalili za Ugonjwa huu huanza kuonekana kati ya Siku 3 hadi 6 tangu kuambukizwa

Soma https://jamii.app/YellowFeverTips

#JFAfyaJamii
πŸ‘6
#JFAFYA: Njia ya kujikinga na Ugonjwa huu ni kupata Chanjo ambayo hutolewa mara moja pekee, kwa Watoto wenye umri wa Miezi 9 na kuendelea

Wajawazito hawashauriwi kupata Chanjo hii labda kama kuna hatari ya Mlipuko

Soma https://jamii.app/YellowFeverTips

#JFAfyaJamii
πŸ‘5
πŸ‘19
INDONESIA: WATOTO WALIOFARIKI KWA MATATIZO YA FIGO WAFIKA 133

Chanzo cha vifo hivyo kinatajwa kuwa ni matumizi ya Dawa za Kifua

> Aidha, kuna Wagonjwa 241 wa Majeraha ya Figo na wengi wao ni Watoto chini ya miaka mitano

Soma https://jamii.app/TatizoLaFigo

#PublicHealth
πŸ”₯3πŸ€”3😒2