JamiiForums
โœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SAKATA LA JENEZA: Klabu ya Simba imewaomba Radhi waumini wa Dini ya Kikristo, Serikali na Jamii baada ya msanii Tundaman kutumia vifaa vya Dini ya Kikristo #SimbaDay

Simba imesema haikufahamu kama atatumia aina hiyo ya maudhui

Soma - https://jamii.app/SimbaRadhi

#JFSports
๐Ÿ‘21๐Ÿ‘Ž3
CHICHARITO YUPO TAYARI KURUDI MAN UNITED

Straika wa zamani wa #ManUnited, Javier Hernandez โ€œChicharitoโ€ amesema yupo tayari kuichezea timu hiyo bila malipo

Kwa sasa Chicharito (34) anaichezea LA Galaxy ya Marekani

Soma > https://jamii.app/Chicharito

#JFSports
๐Ÿ‘19๐Ÿ‘Ž2๐Ÿ˜1
UCHAGUZI KENYA: AJALI YAUA 7 WAKISHEREHEKEA USHINDI WA MBUNGE

Watu saba wamefariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea eneo la Longeld, Samburu Mashariki

Walikuwa wanakwenda kukutana na Mbunge Mteule wa Leerata kabla ya gari kupoteza mwelekeo na kupinduka
๐Ÿค”9๐Ÿ˜ข8๐Ÿ‘7
KENYA: Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) imetoa ruhusa kwa vyombo vya habari kutoa takwimu za kura kulingana na vyanzo vyao lakini matokeo rasmi yatatangazwa na IEBC baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika

Soma: https://jamii.app/KenyaVotesResults

#KenyaDecides2022 #Democracy #Kenya2022
๐Ÿ‘18๐Ÿ‘Ž1๐Ÿ˜ฑ1
UCHAGUZI KENYA: ANAYEDAIWA KUUA KWA RISASI ASHINDA UBUNGE

Didmus Barasa amechaguliwa tena kuwa Mbunge wa Kimilili baada ya kupata kura 26,000 dhidi ya kura 9000 za DAP-K Brian Khaemba

> Barasa anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Msaidizi wa Khaemba

Soma - https://jamii.app/BarasaMP

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘8๐Ÿ˜ฑ1
#SOC2022: BADO SIKU 35. ANDIKA, USHINDE!

Andiko linatakiwa kuchochea mabadiliko chanya katika jamii

Linaweza kujikita kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Uchumi, Kilimo n.k

Mwisho wa kuwasilisha ni Septemba 14, 2022

Taarifa zaidi > jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange
๐Ÿ‘2
STORIES OF CHANGE 2022: Mtanzania yeyote kuanzia miaka 18 anaruhusiwa kushiriki

Zawadi zitatolewa kwa Washindi 20

Kwa Maelezo zaidi > jamii.app/Shindano2

#StoriesOfChange #SOC2022
๐Ÿ‘7
#SIERRALEONE: Serikali imetangaza amri ya kutotoka nje kwa Nchi nzima huku kukiwa na maandamano makubwa dhidi ya Serikali

Waandamanaji wanashinikiza Rais Julius Maada Bio ajiuzulu kutokana na kuongezeka kwa mfumuko wa bei

Zaidi - https://jamii.app/SierraLeoneCurfew

#SierraLeoneProtests
๐Ÿ‘11
Kuhusu suala la kutosha au kutokutosha kwa Maziwa ya Mama, Wataalamu wa #Afya wanasema Tafiti zinaonesha asilimia kubwa ya wakina Mama Maziwa yao yanatosha kwa Watoto

Wengi hufikiri hawana Maziwa ya kutosha kwasababu utengenezaji wake pia unahusisha Saikolojia ya Mama mwenyewe. Mawazo mengi, Msongo wa Mawazo au kuchoka hupelekea utoaji wa Maziwa kupungua

#JamiiForums #BreastfeedingMom #WorldBreastfeedingWeek
๐Ÿ‘7
Uchambuzi wa Hoja za CAG unaonesha pamoja na kupata Hati Safi, Taasisi nyingi za Umma bado zina kasoro za Kiutendaji na zinahitaji kufuatiliwa ili kudhibiti uwezekano wa kuwepo kwa vitendo vya Rushwa na Ubadhirifu wa Rasilimali za Umma

Badala ya kuridhika na Hati Safi zilizotolewa na CAG, ni muhimu Bunge na Kamati zake kufuatilia utendaji wa Serikali na Taasisi zake na kuzingatia uzito wa Hoja pamoja na athari zake kwa Jamii

#JFUwajibikaji
๐Ÿ‘7๐Ÿ˜1
KENYA: ODINGA AMPITA RUTO KWA IDADI YA KURA

Kwa Mujibu wa Citizen, kufikia saa 6:30 mchana Raila Odinga alikuwa na Kura 6,431,752 (49.46%), William Ruto 6,389,957 (49.14%) Prof. Wajackoyah 56,430 (0.43%) na Waihiga 28,973 (0.22%)

Soma https://jamii.app/OdingaRuto

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘11
UCHAGUZI KENYA: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati amevionya Vyombo vya Habari kutotangaza Mshindi wa Kura ya Urais kabla ya Mamlaka hiyo

Amesema atakayeshinda atatangazwa na Tume

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘8
WAANGALIZI WAPONGEZA MCHAKATO WA UCHAGUZI KENYA

Kiongozi wa Wasimamizi hao kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jakaya Kikwete amesema Wasimamizi wamefuatilia Vituo vyote kuanzia wakati wa Kampeni, Upigaji Kura hadi sasa

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘10๐Ÿ˜2
KATAVI: Machia Mbasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga njama za kumuua Mabula Ntemange, anayedaiwa kuwa na Uhusiano na Mkewe yeye akiwa jela

Pia, amemtuhumu Mabula kwa kuchukua kodi katika Vibanda vyake vya Biashara

Soma https://jamii.app/NjamaMauaji

#JFMatukio
๐Ÿ‘7
UCHAGUZI #KENYA: Zoezi la kupokea kura za Uchaguzi Mkuu wa Rais limefikia 99.89% ambapo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati amesema anaamini zoezi litakamilika kufikia jioni ya leo

Soma > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
๐Ÿ‘8
#KENYA: Tume ya Uchaguzi (IEBC) imemtaka Didmus Barasa kuchukua cheti chake cha Ushindi mwenyewe badala ya kumtuma Msaidizi wake

Barasa ametoweka tangu alipodaiwa kumuua Msaidizi wa Mpinzani wake, Brian Olunga, Agosti 9 usiku

Soma - https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘7
UCHAGUZI KENYA: UDA YABEBA MAJIMBO YOTE ENEO LA MGOMBEA MWENZA WA AZIMIO

Chama cha Mgombea Urais William Ruto (UDA) kimenyakua viti vyote vya Ubunge kwenye Kaunti ya Kirinyaga

Ni anakotokea Martha Karua, Mgombea Mwenza wa Raila

Soma https://jamii.app/KE2022

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘8๐Ÿ˜3
MATOKEO KENYA: Mgombea Urais, William Ruto anaongoza kwa Kura 6,676,809 (50.20%) dhidi ya Raila Odinga aliye na Kura 6,534,171 (49.13%) kwa mujibu wa Nation Media

> Matokeo haya ni hadi kufikia saa 12:00 jioni, leo Agosti 11, 2022

Soma - https://jamii.app/KE2022

#KenyaDecides2022
๐Ÿ‘11๐Ÿคฏ2
#RWANDA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametoa wito wa kushughulikiwa kwa Ulinzi wa Kisheria Nchini humo hasa usawa ktk usikilizwaji wa Kesi

Amemrejelea mkosoaji wa Rais Paul Kagame, #PaulRusesabagina ambaye amefungwa kwa ugaidi

Soma https://jamii.app/HumanRightsRwanda

#HumanRights
๐Ÿ‘2๐Ÿคฎ1
KENYA: MCHEKESHAJI ASHINDA UBUNGE

Mchekeshaji Felix Odiwor "Jalangโ€™o" ameshinda nafasi ya Ubunge wa Langโ€™ata kwa tiketi ya ODM

Amepata kura 38,948 dhidi ya Nixon Korir wa UDA aliyepata kura 36,836

Soma > https://jamii.app/KenyaElect2022

#KenyaDecides2022 #Democracy
๐Ÿ‘10๐Ÿ‘2