JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MADHARA YA KUTUMIA SHISHA

Baadhi yanayoweza kujitokeza kwa mtumiaji; Saratani, Matatizo ya Moyo, Kuharibika Fizi, Fangasi na Kifua kikuu

Kuzaa Njiti (wanaotumia wakiwa wajawazito), Kupoteza Uwezo za Kujamiiana, Kuchakaa kwa ngozi

Soka > https://jamii.app/MadharaYaShisha

#JFAfya
👍9
UTAFITI: KUKOSA USINGIZI HUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Utafiti huo wa kwenye jarida la habari za #Afya, LiveScience unasema Wanaume ambao hulala chini ya Saa sita wanaweza kutungisha Mimba kwa 31% huku wanaolala kwa Saa tisa wakiwa na asilimia 49

Soma - https://jamii.app/UsingiziKiume
#Afya
👍15🤔3💩3👏1
MDAU: JINSI YA KUJIANDAA MWENZA WAKO ANAPOPATA UJAUZITO

- Mnapogundua ana Mimba anzeni kuweka akiba kulingana na uwezo wenu. Kama mnaishi pamoja, Mimba ikifikisha Miezi Minne anzeni kuomba na Mtoto aliye Tumboni

- Mjamzito azingatie vyakula vyote vyenye virutubisho. Kama una kipato kidogo anza kununua vitu vya Mtoto taratibu usisubiri mpaka Mama ajifungue

Zaidi, soma - https://jamii.app/MimbaMaandalizi

#JFMaisha
👍14
UCHAGUZI KENYA: Watu wa Jamii ya Washona watapiga kura kwa mara ya kwanza ktk Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, 2022

Kundi la kwanza la Washona liliwasili Kenya likitokea #Zimbabwe takriban Miaka 60 iliyopita na kupewa uraia Mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/WashonaElectKE

#KenyaDecides2022
👍6
HUDUMA YA INTANETI: GHARAMA ZINAKUATHIRI KWA KIWANGO GANI?

Kutumia Intaneti bado ni gharama kubwa kwa Wananchi katika Nchi nyingi zenye Uchumi wa Chini na Kati

Gharama kubwa za kujiunga zinakwamisha Mamilioni ya Watu kutumia Huduma ya Intaneti kikamilifu

Unatumia kiasi gani kugharamia Huduma hii ili kufanikisha shughuli zako za kila siku?

Zaidi, soma > https://jamii.app/Internet001

#DigitalRights
👍10
KIFO CHA MWENYEKITI: FAMILIA YADAI KAUAWA, POLISI YAKANUSHA

Mwili wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Byamtemba Mkoani Kagera, Jonathan Bunyaga uliokotwa kando ya barabara ya Bukoba - Mtukula

Ndugu wamedai kubaini majeraha yaliyoonesha alichomwa na kitu chenye ncha kali. Kamanda wa Polisi, William Mwampaghale amesema chanzo cha kifo ni ajali ya pikipiki kugongana

Soma - https://jamii.app/UtataKifoKagera
👍5🤯3
Kwa mwaka 2020/21, Serikali ilishindwa kukusanya 10% ya Bajeti iliyoidhinishwa, ikiwa ni ongezeko la 5% ukilinganisha na mwaka 2019/20. Hii inafanya utekelezaji wa Bajeti kutofikia Malengo yaliyopangwa

Kushindwa kukusanya Mapato kulingana na Bajeti iliyoidhinishwa inadhihirisha Bajeti Iliyopangwa haikuwa na uhalisia, hivyo matarajio ya Wananchi kutofikiwa

#JFUwajibikaji
👍7
#JFSPORTS: Kocha wa #ManUnited, Erik ten Hag amekasirishwa na Cristiano Ronaldo kuondoka uwanjani wakati mchezo dhidi ya Rayo Vallecano ukiendelea

> Kocha huyo amesema "Sikubaliani na alichofanya, sisi ni timu unatakiwa kukaa hadi mwisho"

Soma https://jamii.app/CR7AmkeraKocha
👍14👏1
UINGEREZA: Upigaji kura kwa njia ya Mtandao ili kumpata Mrithi wa #BorisJohnson umesogezwa hadi Agosti 11, 2022 kutokana na hofu ya kudukuliwa

Wataalamu wa Mtandao wa Serikali wameibua wasiwasi juu ya uwezekano wa kubadilishwa kwa kura

Soma: https://jamii.app/HofuUdukuzi

#Democracy
👍7👎3
SERIKALI YASITISHA MABADILIKO HUDUMA ZA NHIF

Imesitisha mabadiliko ya utaratibu mpya ulioanza kutumika Agosti 1, 2022 baada ya malalamiko ya Wateja

Mabadiliko yaliweka idadi ya mahudhurio hospitalini na utoaji kibali kwa huduma kama MRI, CT SCAN

Soma https://jamii.app/TamkoLaBima
#JFAfya
👍8👎1
MDAU: KWANINI BEI YA MAFUTA INAZIDI KUPANDA NCHINI?

Anasema gharama za maisha zinazidi kupanda kutokana na ongezeko la bei ya mafuta japokuwa Takwimu za Soko la Dunia zinaonesha mafuta yamekuwa yakishuka miezi ya karibuni

Anahoji: Mamlaka inatumia kigezo gani kupandisha bei?

Mjadala > https://jamii.app/KupandaKwaMafuta
👍13😢1
DR-CONGO: Serikali imemtaka Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, Mathias Gillmann kuondoka Nchini humo haraka iwezekanavyo

> Ameshutumiwa kwa kutoa "taarifa zisizoeleweka na zisizofaa" kuhusiana na Nchi hiyo

Soma: https://jamii.app/MsemajiUN

#Diplomacy
👏8👍4😱1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
BONDIA MTANZANIA AINGIA NUSU FAINALI JUMUIYA YA MADOLA

Yusuf Changalawe amemtoa kwa TKO Arthur Lingelier na kutinga Nusu Fainali katika michezo ya Jumuiya ya Madola

Kwa matokeo hayo, Tanzania imepata uhakika wa medali

Soma - https://jamii.app/BondiaMadola2022

#JFSports
👍16👏5
57% YA WATOTO WACHANGA NCHINI WANANYONYESHWA INAVYOTAKIWA

Watoto hao ni wenye umri chini ya miezi sita

Vilevile, Tafiti zinaonesha asilimia 43 tu ya Watoto hunyonyeshwa hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea

Soma - https://jamii.app/Unyonyeshaji

#WorldBreastfeedingWeek
👍8
- Mdau wa JamiiForums.com anaomba msaada wa mbinu anazoweza kuzitumia ili kumfanya Mtoto wake mwenye Miaka 8 aache kukojoa Kitandani na kunyonya kidole

- Licha ya kumwamsha Mtoto usiku hata mara mbili ila bado atakojoa. Mtoto anaweza kulala hata nusu saa na akakojoa. Alianza tabia hizi akiwa na Miaka mitatu

Tembelea - https://jamii.app/MtotoKukojoa
#JFMalezi #Malezi
👍6
RWANDA: MISHAHARA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI KUONGEZWA KWA 88%

Nyongeza hiyo ni sehemu ya Mikakati inayolenga kuboresha Maslahi ya Walimu na kukuza ubora wa Elimu

Waziri wa Elimu amesema Mishahara ya Walimu wa Shule za Sekondari nayo itaongezeka kwa 40%

Soma - https://jamii.app/WalimuRW

#Governance
👍28🥰3
BURKINA FASO: Jeshi limekiri kuua raia wa kawaida kimakosa katika mashambulizi yake ya anga Kusini Mashariki mwa Nchi hiyo

> Burkina Faso imekuwa ikipambana na Waasi wanaohusishwa na Makundi ya Al-Qaeda na ISIL (ISIS)

Soma https://jamii.app/MapiganoBurkinaFaso

#JamiiForums
👍5👎1
#COVID19: Shirika la Madawa la Ulaya linapendekeza Chanjo ya Novavax kubeba onyo la uwezekano wa Mtumiaji kupata madhara Moyo ya aina mbili ambayo ni 'Myocarditis' na 'Pericarditis'

> Hadi sasa chanjo hiyo imetolewa kwa Watu 250,000 Barani Ulaya

Soma https://jamii.app/NovavaxEffects
#JFAfya
👍5
Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Mwananchi nafasi ya kushiriki katika shughuli za Maendeleo ya Nchi

Ushirikishwaji Wananchi katika mchakato wa Bajeti ni muhimu kwasababu husaidia kuifanya izingatie vipaumbele vyao

Pia, huongeza ufanisi katika usimamizi wa Mapato na Matumizi ya Fedha za Umma katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji/Mitaa na Kata

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji
👍9
CHELSEA YAWAWINDA AUBAMEYANG NA DE JONG

Frenkie de Jong na Pierre-Emerick Aubameyang wote ni Wachezaji wa Barcelona

> Barcelona inataka kuwauza Wachezaji hao ili kuweka sawa vitabu vya mahesabu ya klabu

Soma https://jamii.app/TransferBarca

#JFSports
👍6