JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Mahakama ya Juu imebatilisha uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wa uandikishaji wa Wapiga kura kwa Mfumo wa Kielektroniki pekee kwa kigezo cha kuepuka Uchakachuaji wa Kura katika Uchaguzi wa Agosti 9

Soma https://jamii.app/Kenya2022Uchaguzi

#KenyaDecides
πŸ₯°1
MAREKANI: Wanahabari wa #Reuters wamepanga kugoma kupinga ongezeko la Mishahara la 1% ambalo haliendani na Mfumuko wa Bei wa 9%

> Hivi karibuni Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari nchini humo wamelalamika kutotendewa haki na Waajiri wao

Soma https://jamii.app/MgomoReuters
πŸ‘4πŸ‘1😁1
MAREKANI: Rais Joe Biden amesaini amri inayolenga kulinda Haki ya kutoa Mimba

Amri hiyo inawataka Maafisa wa #Afya kuruhusu Fedha za Umma kutumika kuwasaidia Wanawake kusafiri kwenda kwenye Majimbo wanakoweza kutoa Mimba

Soma - https://jamii.app/BidenMimba

#HumanRights
πŸ‘Ž6πŸ‘5🀯3
INDIA: Bunge limetupilia Mbali Muswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha unaotajwa kuipa Serikali Mamlaka ya kudai taarifa za Wateja kutoka kwa Kampuni za Teknolojia

Wadau wamesema hatua hiyo italinda faragha za Raia

Soma https://jamii.app/DataProtectionAndPrivacy

#DigitalRights
πŸ‘3
Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Mawasiliano (ITU) Mataifa ambayo gharama za Intaneti zipo juu yana idadi kubwa zaidi ya watu wasiotumia Mtandao

Intaneti ni Huduma ambayo inategemewa na wengi katika shughuli zetu. Ni muhimu kila mmoja kuweza kuifikia ili kunufaika nayo kikamilifu

#DigitalRights
πŸ‘9
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) ulipitishwa mwaka 2006 kukabiliana na ukiukwaji mkubwa wa #HakiZaBinadamu unaofanywa dhidi ya Watu wenye Ulemavu duniani kote

Ni muhimu kwa Watu wenye Ulemavu kuwa washiriki hai katika Jamii zao na kuishi Maisha yenye kuridhisha

Fahamu zaidi - https://jamii.app/CRPD15

#HumanRights
πŸ‘2❀1
IRINGA: KINYOZI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Batista Ngwale (27) amekutwa na hatia katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa, ikielezwa alisababisha Binti kusitisha masomo

Binti huyo alikuwa anasoma Kidato cha Nne

Soma > https://jamii.app/HukumuIringa

#JFMatukio
πŸ‘6
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL). Amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa TPA

Vilevile, Stephen Kagaigai ameteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC

#Governance
πŸ‘5πŸ‘Ž3
FAIDA ZA MTOTO KUNYONYESHWA NDANI YA SAA MOJA BAADA YA KUZALIWA

1) Kusaidia Maziwa ya Mama kutoka mapema

2) Kusaidia kumpa Mtoto joto

3) Kujenga uhusiano wa kihisia na upendo kati ya Mama na Mtoto

Fahamu zaidi > https://jamii.app/KunyonyeshaMtoto

#WorldBreastfeedingWeek
πŸ‘12😁2❀1
SOMALIA: Umoja wa Mataifa umesema takriban 90% ya Raia wanakabiliwa na ukame Nchini humo, hali iliyopelekea watu 918,000 kuhama makazi yao

Pia Utapiamlo pamoja na milipuko ya magonjwa inaripotiwa kuongezeka

Soma - https://jamii.app/SomaliaDrought
πŸ‘9
FAIDA ZA STRAWBERRY MWILINI

- Husaidia kuimarisha uwezo wa Ubongo katika kuweka na kutunza kumbukumbu

- Yana kiwango kikubwa cha Madini ya Zinc ambayo husaidia kuimarisha #Afya ya Uzazi kwa Mwanaume
-
- Matunda haya yana Vitamini E ambayo hunyoosha mikunjo ya Ngozi na kupunguza mchakato wa kuzeeka

Soma - https://jamii.app/StrawberryFaida

#JFAfya
πŸ‘15πŸ₯°1
CHINA YARUSHA MAKOMBORA KARIBU NA TAIWAN

Imerusha Makombora kufuatia ziara ya Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi ktk kisiwa hicho

#Taiwan inadai Makombora yalikuwa 11, pia kulikuwa na Ndege za kijeshi zilizoonekana kuzunguka eneo

Soma https://jamii.app/MakomboraYaChina
#JamiiForums
πŸ‘12
RWANDA YATUHUMIWA KUWASAIDIA WAASI WA M23 NCHINI #DRC

Kwa mujibu wa ripoti ya Baraza la Usalama la UN, #Rwanda imefanya uingiliaji wa Kijeshi katika Ardhi ya Congo tangu Novemba 2021

Pia, ilitoa Wanajeshi kwaajili ya operesheni za M23

Soma - https://jamii.app/RWDM23UN
πŸ‘8
SUDAN KUSINI: SERIKALI YA MPITO KUBAKI MADARAKANI KWA MIAKA MIWILI ZAIDI

Sudan Kusini ilipaswa kufanya Uchaguzi Februari 2023, lakini hadi sasa Serikali hiyo imeshindwa kutimiza masharti muhimu ya makubaliano ikiwemo kuandaa #Katiba mpya

Soma - https://jamii.app/SudanMpito2

#Democracy
Ukatili/Uonevu Mtandaoni hupenya katika kila nyanja ya maisha ya Mwathirika, na unaweza kusababisha matatizo ya Kisaikolojia na Kijamii

Kuwa "Raia bora wa Mtandaoni" (Good Netizen) ni pamoja na kujua kile kinachofaa kufanya katika mazingira ya Mtandaoni

#JamiiForums #DigitalRights #CyberBullying
Mara baada ya kujifungua, Mama na Mtoto wagusane Ngozi kwa Ngozi ili kusaidia Maziwa kutoka

Virutubisho vilivyomo kwenye Maziwa ni:
Maji 87%
Wanga 7%
Mafuta 4%
Protini 1%
Vingine 1% (Vitamini, Madini, Kingamwili, Vimeng'enya, Kiinitete)

Soma > https://jamii.app/KunyonyeshaMtoto

#WBW2022
πŸ‘9
#JFDATA: Matumizi ya Intaneti Duniani yaliongezeka maradufu kutokana na Mlipuko wa COVID-19 uliopelekea wengi kuitumia kwa Kazi, Masomo, Huduma muhimu na Mawasiliano

Mwaka 2020, Watumiaji wa Intaneti waliongezeka kwa 10.2% ambayo inatajwa kuwa idadi kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10. Kwa Mwaka 2021, ongezeko hilo lilifikia 5.8%

Fahamu zaidi - https://jamii.app/DataInternet
πŸ‘5πŸŽ‰1
SENEGAL: Serikali imetia saini Mkataba wa Amani na Waasi wa Chama cha Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC) wanaotaka kujitenga

Mkataba huo unatajwa kuweza kumaliza mzozo uliodumu tokea Mwaka 1982 Nchini humo

Soma https://jamii.app/AmaniSenegal

#Governance
πŸ‘5
Mdau anasema kuficha wazo la #Biashara na huku ukiwa huna mtaji si ufahari ila ni kuendeleza Umasikini

Ameshauri kuwashirikisha Wadau wa maendeleo ili kupata msaada wa hali na mali wa utekelezaji wa wazo hilo na kulipa uhai

Msome - https://jamii.app/BusinessIdea

#JFBiashara
πŸ‘4
MDAU: NAWEZAJE KUTUMIA KOMPYUTA KUINGIZA KIPATO?

Mdau wa JamiiForums.com anaomba ushauri akisema ameshawahi kuitumia kwenye shughuli za Stationery na ana uwezo wa β€˜Video production’

Je, umewahi kuingiza kipato kupitia Kompyuta? Mshauri Mdau anavyoweza kujiajiri

Mjadala - https://jamii.app/ComputerKujiajiri

#Maisha #JFBiashara
πŸŽ‰2πŸ”₯1πŸ₯°1