JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Wanasiasa wa Upinzani kukosa ushirikiano wenyewe kwa wenyewe ni chanzo kikuu cha kukosekana kwa Upinzani imara nchini. Udhaifu wetu mkubwa ni kukosa umoja

> Katiba sio mwarobaini bali utashi ndio unatakiwa. Nilimwambia Mnyika 'Hamuwezi kuandamana kama tulivyokuwa tunafanya sisi'

> Nilikuwa tayari kukaa ndani kutetea wenzangu lakini wao wakisikia kuna kukamatwa watakimbia watajificha uvunguni

Soma - https://jamii.app/KongamanoTLS

#Democracy30 #30YrsOfMultipartism
👍13
SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

Usafirishaji Haramu unatajwa kuwa janga linaloendelea kukua na Wanawake na Watoto ndio wahanga wakubwa

Maadhimisho ya Mwaka 2022 yanaangazia nafasi ya Teknolojia katika kuwezesha na kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu

Fahamu zaidi https://jamii.app/HumanTRF2022

#EndHumanTrafficking
👍4😢1
USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU MITANDAONI

Usafirishaji Haramu wa Binadamu kupitia Mitandao unashika kasi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya Teknolojia

Majukwaa ya Kidigitali yamekuwa fursa kwa Watuhumiwa wa Biashara hii Haramu

Wanayatumia kuwatambua na kuwapata Wahanga, miongoni mwao wakiwemo Watoto

Soma zaidi - https://jamii.app/HumanTRF2022

#EndHumanTrafficking
👍6😢1
Teknolojia inaweza kuwa na nafasi muhimu katika Mapambano dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu endapo itatumika ipasavyo

Utoaji Elimu zaidi juu ya Matumizi Salama ya Intaneti na Mitandao ya Kijamii unaweza kusaidia kupunguza hatari ya Watu kuwa Wahanga

Soma > https://jamii.app/HumanTRF2022

#EndHumanTrafficking
👍3
FATMA KARUME: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa ovyo kuliko chaguzi zote zilizopita. Hakujawahi kutokea chaguzi yoyote tangu Mfumo wa Vyama Vingi uanzishwe kusiwe na kesi Mahakamani isipokuwa wa 2020, na hii ni kwa sababu Watu hawana Imani na Mahakama

> Tumetengeneza Mhimili wa Mahakama usioweza kufanya kazi yake. Rais kuwa na Uwezo wa Kumteua na Kumuondoa Jaji Mkuu kunaondoa Uhuru wa Mahakama

> Pia, Mahakama kutegemea Bajeti ya Serikali kufanya shughuli zake hudunisha uhuru wa Mahakama

Soma - https://jamii.app/KongamanoTLS

#Democracy30 #30YrsOfMultipartism
👍14
MAKARAMBA (JAJI MSTAAFU): Kuna tatizo kubwa Watanzania kuchanganya mambo. Sheria mbovu huwa inatamkwa na Mahakama siyo Mwanasiasa

> Ila wanasiasa ndio ambao tunaamini wanaweza kutunga Sheria mbovu na ndio mwanzo wa kuingiliana Mamlaka katika vile vyombo vitatu

> Wale ambao hawapaswi kutunga Sheria ndio wanatunga Sheria, ambao hawapaswi kutafsiri ndio wanatafsiri Sheria. Ndio maana mnasikia mtu anasema 'Nitakuweka ndani' yaani anakuwa Sheria, Mahakama na Polisi kitu ambacho tulipiga marufuku

#30YrsOfMultipartism
#Democracy30
👍12
FRANCIS STOLLA (RAIS MSTAAFU WA TLS): Mahakama ni Mhimili unaojitegemea ukiachana na Teuzi

> Nchi yetu inapaswa ijengwe na Mifumo. Inabidi Tawala na Idara mbalimbali nchini zifanye kazi kimfumo

Soma - https://jamii.app/KongamanoTLS

#Democracy30 #30YrsOfMultipartism
👍5
ADO SHAIBU (ACT WAZALENDO): Vyama vya Siasa viwajibike kutengeneza mazingira bora ya Ushiriki wa Wanawake ktk Siasa

> Demokrasia isipoimairishwa, Siasa zikiendelea kuwa za piga ua, za baruti, za mabomu, za kukimbizana itawafanya Wanawake washindwe kushiriki Kisiasa

#Democracy30
👍2
USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU: UNAWEZAJE KUJILINDA MTANDAONI?

- Kuwa Makini na Urafiki wa Mitandaoni: Wahalifu hutumia Mitandao kujenga uaminifu

- Usiamini kila tangazo kirahisi: Wanaofanya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu hutoa ahadi nono ambazo ni rahisi kumshawishi yeyote

Fahamu zaidi > https://jamii.app/HumanTRF2022

#EndHumanTrafficking
👍6
ALPHONCE SIMBU ASHINDA MEDALI YA FEDHA

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Felix Simbu ametwaa Medali ya Fedha baada ya kuibuka mshindi wa pili wa Mbio za Riadha katika Michezo ya Jumuiya ya Madola Jijini Birmingham, Uingereza

Simbu ametumia muda wa 2:12:29 huku Mshindi wa Kwanza, Victor Kiplagat ambaye ni Raia wa Uganda akitumia 2:10:55

#JFSports
👏19👍7
SENZO KUONDOKA YANGA, WAKILI SIMON PATRICK AKABIDHIWA MIKOBA

Klabu ya Yanga imetangaza kutomuongezea Mkataba Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza anayemaliza mkataba wake kesho Julai 31, 2022

Yanga imesema Senzo ndiye ameomba kutoongezewa mkataba kutokana na sababu za kifamilia. Wakili Simon Patrick ameteuliwa kukaimu nafasi

Soma - https://jamii.app/SenzoYangaApart

#JFSports
BONDIA MANDONGA APIGWA KWA KO

Bondia Karim Mandonga amepoteza dhidi ya Shabani Kaoneka, Raundi ya 4 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea

Baada ya pambano Mandonga amesema: "Ni ajali kazini lakini nipo tayari kurudiana na mpinzani wangu."

Soma > https://jamii.app/MandongaApoteza

#JFSports
😁32👍6🔥3
KIDUNDA AMPIGA KATOMPA KWA POINTI

Bondia Mtanzania Selemani Kidunda ameshinda Mkanda wa WBF Inter Continental kwa pointi dhidi ya Eric Katompa wa DRC

Pambano lilikuwa la Super Middleweight Raundi 10 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea

Soma > https://jamii.app/NdondiSongea

#JFSports
👍17👏5👎1
UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameamuru Raia waliopo katika Mji wa Donetsk kuondoka haraka kutokana na kuendelea kwa mapigano dhidi ya Vikosi vya Urusi

> Rais huyo amesema Serikali itawasaidia kwa Fedha wote wanaohamishwa

Soma https://jamii.app/KuhamaDonetsk

#RussiaUkraineWar
👍5😁2
MISRI: Wafungwa 7 wakiwemo Mwandishi wa Habari, Hisham Fouad pamoja na Mtafiti wa Masuala ya Binadamu (Anthropology), Ahmed Samir ambao walishtakiwa kwa Makosa ya Ugaidi wameachiwa huru

> Wameachiwa kwa msamaha wa Rais

Soma https://jamii.app/WafungwaWaachiwa

#JamiiForums
👍7
KAONEKA: KAMA NITARUDIA PAMBANO NA MANDONGA, SITAFANYA MAZOEZI

Bondia Shabani Kaoneka aliyempiga kwa TKO Karim Mandonga amesema yupo tayari kwa pambano la marudio

> Amesema hatafanya mazoezi ili kupambana na Mandonga kwa kuwa udhaifu wake anaujua

Soma https://jamii.app/BondiaKaoneka
😁37👍3👏1
NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA UKRAINE ZASHAMBULIA MELI ZA URUSI

Mashambulizi hayo yametokea katika Bandari ya Crimea na kujeruhi Watu watano

> Wakazi wa eneo hilo wametakiwa kubaki ndani kwa sababu za kiusalama

Soma https://jamii.app/RussianFleetAttacked

#RussiaUkraineWar
👍13
MDAU: JITIHADA HUAMUA KUFANIKIWA AU KUFA KWA BIASHARA

Amefafanua kuwa, kila biashara au fursa ina uwezo wa kutengeneza faida kubwa ikiwa tuu nguvu, ubunifu na mtaji stahiki vitawekezwa kwa wakati sahihi

Soma - https://jamii.app/JitihadaBiashara

#JFBiashara
👍7🥰1
UTEUZI WA DKT. CHEGENI WATENGULIWA

Rais Samia ametengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni na kumteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP)

Soma - https://jamii.app/UteuziMara

#Governance
👍14😁6
RONALDO AONDOKA OLD TRAFFORD MECHI IKIENDELEA

Cristiano #Ronaldo ameichezea Manchester United mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano, alitolewa wakati wa mapumziko, akaondoka mechi ikiendelea

> Matokeo ya mchezo huo yalikuwa 1-1

Soma https://jamii.app/CR7Exit

#JFSports
😁17👍4👎3🤔2