JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTEUZI: Balozi Caroline Kitana Chipeta ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, The Hague nchini Uholanzi

Kabla hajateuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Balozi Chipeta alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje

Soma - https://jamii.app/UteuziBalozi

#Governance
πŸ‘4🀯1
KENYA: Mgombea Urais (Chama cha wa Roots), Profesa George Wajackoyah amesema hatashiriki kwenye Mdahalo unaotarajiwa kufanyika Julai 26, 2022 kwa kudai kuwa matokeo ya Mdahalo huo yameshapangwa

> Anakuwa mgombea wa 2 kujitoa baada ya Raila Odinga

Soma https://jamii.app/MdahaloUrais

#Democracy
πŸ‘5
DR-CONGO: Takriban Watu watano wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa ktk Siku ya 2 ya maandamano ya kupinga uwepo wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa ktk Mji wa Goma

> Vikosi hivyo vinadaiwa kushindwa kudhibiti Waasi katika eneo hilo

Soma https://jamii.app/DRCProtests

#JFDiplomasia
πŸ‘13πŸ‘1
KENYA: Shule ya Mosoriot imefungwa baada ya Mwalimu wa Shule hiyo, Bernard Kirui kubainika aliwaingilia Watoto 3 wa kiume wenye umri wa miaka 11-13

> Inadaiwa Mwalimu alikuwa akilala ktk Bweni la Wavulana licha ya kuwa na chumba alichotengewa

Soma https://jamii.app/WatotoUnyanyasaji

#HakiMtoto
😒10πŸ€”5πŸ‘4πŸ‘Ž2
UCHAGUZI KENYA: William Ruto amemkosoa Mpinzani wake, Raila Odinga kwa kutoshiriki Mdahalo wa Wagombea Urais akisema kitendo hicho ni kuepuka #Uwajibikaji

Asema Raila si Mgombea halisi, anakimbia Maswali magumu, na hana la kusema kwa Wakenya

Soma - https://jamii.app/RutoDebate

#Kenya2022
😁13πŸ‘6
UPDATE: Waliofariki dunia katika maandamano ya kupinga uwepo wa Walinda Amani wa UN Nchini DR Congo wamefikia 15. Miongoni mwao ni Raia 12 na Walinda Amani 3

Waandamanaji wanadai Walinda Amani wameshindwa kudhibiti waasi hivyo uwepo wao hauna faida

Soma https://jamii.app/ChaosDRC2022

#Governance
πŸ‘15
#JFDATA: Mashirika mengi bado yanachukulia masuala ya Ulinzi wa Kidigitali kama kitu ambacho si lazima kuwa nacho

Kwa mujibu wa Ripoti ya Acronis (2022), nusu ya Mashirika Duniani hutenga chini ya 10% ya Bajeti yote ya TEHAMA kwenye Usalama wa Kidigitali

86% ya Mashirika Duniani yana wasiwasi kuhusu ongezeko la mashambulizi ya Mtandaoni

Soma zaidi - https://jamii.app/UlinziDigitali7
πŸ‘7
UMOJA WA MATAIFA (UN): Mashambulizi dhidi ya Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC yanaweza kuwa Uhalifu wa Kivita

> Hadi sasa, Wafanyakazi watatu wa Umoja wa Mataifa na Raia 12 wa DRC wameuawa katika matukio hayo

Soma https://jamii.app/GhasiaDRC

#JFDiplomasia
πŸ‘6πŸ‘Ž2
ZAMBIA: Esther Lungu (Mke wa Rais wa zamani) amehojiwa na Wakala wa Kupambana na Utakatishaji Fedha wa Zambia kuhusu umiliki wake wa nyumba 15 zilizopo Lusaka

> Serikali ya Hichilema imekosolewa kuwa inafanya matukio hayo kwa sababu za kisiasa

Soma https://jamii.app/SiasaYaZambia

#Governance
πŸ‘10πŸ‘Ž3πŸ‘1
#JFUWAJIBIKAJI: Kulingana na Ripoti ya CAG ya mwaka 2020/21, Serikali za Mitaa 131 zilikusanya Mapato ya Tsh. Bilioni 615.58 sawa na 18% tu ya Matumizi yake ya kawaida

Hii inafanya Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuwa tegemezi kwa Serikali Kuu kwa 82%, hali inayohatarisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali

Utegemezi wa Fedha unazorotesha utekelezaji wa Mipango ya Halmashauri ya kutoa Huduma kwa Wananchi pale ambapo Fedha hazijatolewa kabisa, zimetolewa pungufu au zimechelewa

#JamiiForums #WAJIBU
πŸ‘7
MWANZA: HAKIMU KESI YA 'MFALME ZUMARIDI' AGOMA KUJITOA

Hakimu Monica Ndyekobora amesema hoja zilizowasilishwa na Upande wa Utetezi za kutokuwa na imani naye hazina mashiko

> Amesema kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena chini yake Agosti 10, 2022

Soma https://jamii.app/KesiZumaridi

#SocialJustice
πŸ‘15πŸ‘Ž5😁2πŸ”₯1🀩1
MOROGORO: Donati Phabian amehukumiwa jela miaka 7 kwa kumuua bila kukusudia Alfred Damas, alimchoma kisu alipomkuta amesimama na mtalaka wake huku chanzo kikitajwa ni wivu wa mapenzi

> Baada ya tukio Donati alijipeleka Polisi

Soma https://jamii.app/HukumuYaMauji

#JFMatukio
πŸ€”7πŸ‘4πŸ‘Ž1
ZIMBABWE: Mamlaka ya Kudhibiti Dawa imeruhusu uuzwaji wa bangi katika Maduka ya Dawa ambapo pia Wauzaji wa Rejereja na Jumla wanaohitaji kuuza nje ya Nchi watatakiwa kuomba kibali Serikalini

> Mkakati huo ni sehemu ya kuongeza pato Nchini humo

Soma https://jamii.app/BangiZimbabwe

#Livelihoods
πŸ‘22πŸ‘Ž3πŸ‘2❀1
'VUMBI LA KONGO' LAPIGWA MARUFUKU

Dawa hiyo imefutiwa usajili Tanzania baada ya kubainika imechanganywa na Dawa ya Nguvu za Kiume iitwayo β€˜Viagra’

> Imeeleza kuwa, hiyo ni kinyume cha Sheria/Miongozo ya usajili wa Dawa za Tiba Asili na Mbadala

Soma https://jamii.app/VumbiLaKongoMarufuku

#JFAfya
πŸ‘20😁14πŸ€”2πŸ‘1
#KEMEARUSHWA: Rushwa hukwamisha Uwajibikaji na huwaacha Watu ktk Utawala na Viongozi wasioaminika hivyo kukabiliwa na Unyonyaji na Ufisadi

> Wanaotumia Ofisi au Mamlaka fulani kwa Manufaa ya Binafsi wawajibishwe ili wawe mfano

Soma https://jamii.app/RushwaAdui

#JFUwajibikaji
πŸ”₯6πŸ‘3
Wadau ndani ya JamiiForums wametaja baadhi ikiwemo Kuongea na Simu kwa sauti kubwa ndani ya Daladala, Kupiga Mswaki hadharani na kumuonesha Mtu picha moja tu kwenye Simu yeye anaanza kuangalia na nyingine

#JamiiForums #Maisha #LifeStyle
😁7πŸ‘6
MDAU: Siku hizi mtu anaona kuliko kuhoji Kiongozi asipotimiza majukumu yake na kukosa fursa kwa kuonekana mkosoaji, ni bora akubaliane na kila jambo ili apate uteuzi fulani

> Tuwajibishane na kukosoa pale panapostahili kwa manufaa ya Jamii

Soma https://jamii.app/KuhojiUwajibikaji

#JFUwajibikaji
πŸ‘22😱1
KAFULILA, HAPI WATEMWA. CHALAMILA AREJESHWA

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Chalamila amewahi kuwa Mkuu wa Mikoa ya Mbeya na Mwanza

Mbali na Chalamila, Wakuu wa Mikoa wapya walioteuliwa ni pamoja na Peter Serukamba (Singida), Nurdin Babu (Kilimanjaro) na Fatma Mwasa (Morogoro)

Wengine ni Halima Dengego (Iringa), Dkt. Raphael Chegeni (Mara) na Dkt Yahaya Nawanda (Simiyu), Kanali Ahmed Abbas (Mtwara) na Kanali Laban Thomas (Ruvuma)

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
πŸ‘20πŸ‘Ž3πŸ‘2❀1
MABADILIKO YA VITUO: Anthony Mtaka (Dodoma) amepelekwa Njombe, Queen Sendiga (Iringa) anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Waziri Kindamba anahamishiwa Songwe (alikuwa Njombe), Martin Shigella aliyekuwa Morogoro anahamishiwa Geita

Omary Mgumba amehamishiwa Tanga (alikuwa Songwe), Adam Kigoma Malima amehamishiwa Mwanza (alikuwa Tanga) na Rosemary Senyamule wa Geita anaenda Dodoma

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
πŸ‘10πŸ‘1
WAKUU WA MIKOA 10 WABAKI KWENYE NAFASI ZAO

Amos Makalla (Dar es Salaam), John Mongella (Arusha), Mwamvua Hoza Mrindoko (Katavi), Charles Makongoro Nyerere (Manyara), Zainab Rajab Telack (Lindi) na Juma Homera (Mbeya)

Wengine ni Thobias Andengenye (Kigoma), Sophia Mjema (Shinyanga), Balozi Batilda Salha Burian (Tabora) na Abubakar Kunenge (Pwani)

Soma - https://jamii.app/UteuziRC2022

#Governance
πŸ‘14