JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPUNGUFU WA MAJENGO YA MAHABUSU NA WAFUNGWA

Gereza la Keko lilikuwa na msongamano mkubwa zaidi ambapo lilikuwa na Wafungwa 1,075 zaidi ya uwezo wake sawa na 194%

Magereza 8 kati ya 15 yaliyokaguliwa hayakuwa na huduma ya Maji Safi na Salama kutokana na kutolipia Huduma ya Maji kwa Mamlaka husika

#JFUwajibikaji
😢7🤔3👍2
KUCHELEWA KWA RIPOTI ZA CAG

Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Japhet Hasunga amesema CAG anatumia mifumo kuandaa ripoti yake hivyo ripoti hizo zitoke mapema ili Bunge pia liweze kuzijadili mapema

Hasunga amesema hiyo itatoa fursa ya Uwajibikaji kabla fedha nyingine hazijaombwa Bungeni

#JFUwajibikaji
👍14🤔2
SOMALIA: WAANDISHI WAHIMIZA SHERIA ZA VYOMBO VYA HABARI KUREKEBISHWA

Wamesema Kanuni za Adhabu na Sheria ya Vyombo vya Habari zimekuwa tishio kwa usalama wao

Wameeleza kuwa Sheria mpya hailindi usiri wa Vyanzo vya Habari, na inaruhusu Waandishi kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kukata rufaa

Soma - https://jamii.app/SomaliaJounalists

#PressFreedom
👍7
RAIS WA MPITO AAPISHWA SRI LANKA

Ranil Wickremesinghe aliyekuwa Waziri Mkuu ameapishwa kuwa Rais wa Mpito, akimrithi Gotabaya Rajapaksa aliyejiuzulu kufuatia maandamano

Atahudumu kwa muda uliosalia katika Muhula wa Rajapaksa unaokamilika 2024

Soma - https://jamii.app/RaisMpyaSriLanka

#Governance
👍11🔥1
GEITA: Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amethibitisha vifo vya Wachimbaji 3 wa dhahabu na majeruhi wawili baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyamatagata

> Shughuli kwenye machimbo hayo zimesimamishwa kwa muda

Soma - https://jamii.app/VifoGeita

#JFMatukio
👍8😢3👎2
MANCHESTER UNITED YAMSAJILI ERIKSEN

Christian Eriksen (30) amesaini mkataba wa miaka mitatu kufuatia kufanyiwa uchunguzi mkali wa afya

Mchezaji huyo anaimarisha safu ya kiungo ya Erik ten Hag baada ya kuchagua kutosalia Brentford, alikokuwa msimu uliopita kwa mkopo

#JFSports
👍16👏1
JOTO KALI: UINGEREZA YATANGAZA HALI YA DHARURA

Mamlaka imetangaza hali ya dharura ya Kitaifa na kutoa onyo la joto kali katika baadhi ya maeneo

Wataalamu wamesema joto linaweza kufikia viwango vya juu vinavyoweza kuathiri watu na miundombinu

Soma - https://jamii.app/UKHeatRise
👍8🤔4👎21🔥1😁1
UGANDA: Zaidi ya watu 500,000 katika Mkoa wa Karamoja wanakabiliwa na njaa iliyosababishwa na ukame uliodumu kwa muda mrefu

Aidha, watu kadhaa wameripotiwa kufariki dunia maeneo ya Kaskazini Mashariki ya Nchi hiyo kutokana na njaa

Soma - https://jamii.app/UgandaNjaa
😢11👍4😱1
MISRI KUONDOA VIKOSI VYAKE VYA KULINDA AMANI NCHINI MALI

UN imesema Misri itaondoa Wanajeshi wake ifikapo Agosti 15. Kujitoa kwao ni pigo jingine baada ya doria za Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali kusitishwa kwa muda

Wanajeshi 7 wa Misri wameuawa mwaka 2022

Soma https://jamii.app/VikosiMali

#Diplomacy
👍11👏1
AFRIKA KUSINI: Mamia waandamana kushinikiza kuondolewa kwa Rais Ramaphosa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na kukatika kwa umeme mara kwa mara

> Sababu nyingine ni kukithiri kwa rushwa ktk Taasisi za Umma na ukosefu wa ajira

Soma https://jamii.app/MaandamanoAfrikaKusini

#Democracy
👍14🔥4😁2
BARCELONA YAKUBALIWA KUMSAJILI LEWANDOWSKI

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert #Lewandowski atasajiliwa kwa takriban Tsh. Bilioni 117

> Anasafiri leo kwenda Hispania kukamilisha usajili huo, anatarajiwa kusaini miaka mitatu

Soma https://jamii.app/LewandowskiBarca

#JFSports
👍21
TMA: NJOMBE KUNA SAKITU SIYO THELUJI

Mamlaka Hali ya Hewa (TMA) imefafanua kuwa kinachotokea Njombe hivi karibuni ni Sakitu inayosababishwa na umande kuganda na siyo Theluji

> Pia, Upepo wa Kusi unasababisha baridi kali maeneo mengine Nchini

Soma https://jamii.app/BaridiLaNjombe
👍11😁2🎉1
UTAFITI: KANDA YA ZIWA YAONGOZA UKATILI WA WENZA

Wataalamu wa Afya wamesema Mikoa inayoongoza ni Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita

> Mikoa ambayo ina kiwango cha chini cha ukatili kwa wenza ni Pemba, Ukanda wa Pwani na Tanga

Soma https://jamii.app/UkatiliRipoti

#JFSaikolojia
👍14🤔1
KOCHA WA BARCELONA AZUIWA MAREKANI

Kocha Xavi Hernandez amezuiwa kwenda Marekani kutokana na rekodi ya kuingia Nchini Iran zaidi ya mara tatu

Ili kuingia Marekani, yeyote mwenye rekodi kama hiyo anatakiwa kupata kibali maalum

Soma > https://jamii.app/XaviMarekani

#JFSports
😱12👍7😁7💩7🤔5🎉1
KENYA: MTENGENEZA MAUDHUI YA 'TIKTOK' ALAZWA BAADA YA KULA BUIBUI

Inadaiwa Aq9ine alianza kuumwa kifua huku joto la mwili likifika 48℃ baada ya kula buibui

Baada ya kushambuliwa Mitandaoni amesema akipona, atapika na kula chura na nyoka

Soma - https://jamii.app/TiktokerHospitalized
😁10🤔6👍1
MEXICO: Helikopta iliyokuwa ikitumika kusaka wahalifu wakiwemo wa dawa za kulevya imeanguka na kuua watu 14, huku mmoja akijeruhiwa vibaya

Chanzo cha ajali ya ndege hiyo hakijawekwa wazi

Soma - https://jamii.app/HelikoptaMexico
👍8😁4🤔4👎2🤮1
Huduma ya Intaneti imetoa usaidizi mkubwa katika kutafuta kazi, lakini bado ina safari ndefu kuwa namna ya kutegemewa katika kutafuta kazi kwenye jamii masikini kwani ufikiaji wake ni changamoto

Kwa mujibu wa Takwimu za Benki ya Dunia, ongezeko la 10% la upenyaji wa Intaneti Afrika linaweza kuongeza Pato la mtu mmoja mmoja kwa karibu 2.5%

Soma - https://jamii.app/HudumaIntaneti

#JFData #DigitalRights
👍7
WAMAREKANI 61 MARUFUKU KUINGIA IRAN

Iran imetoa orodha ya majina 61 ya Wamarekani ambao hawaruhusiwi kuingi Iran. Sababu kubwa ni kuunga mkono kikundi cha MEK ambacho wanakishutumu kwa ugaidi

Wengi wao ni Maofisa wa Serikali

Soma - https://jamii.app/IranUSA

#JFDiplomasia
👍14👎1
MDAU: JINSI YA KUTIBU/KUZUIA KISUKARI KWA KUTUMIA LISHE

Saga Karoti, Tango, Kitunguu Maji, Hoho, Nyanya na Limau likiwa na maganda na mbegu zake

> Kunywa mchanganyiko huo kila asubuhi dakika 45 au 60 kabla ya kula kitu kingine

Je, unafahamu lishe gani nyingine?

Soma https://jamii.app/TibaYaKisukari

#PublicHealth #JFAfya
👍293🤮3😁2
MANCHESTER UNITED KUMSAJILI LISANDRO

Imefikia makubaliano na Ajax kumsajili Lisandro Martinez (24) kwa £55.3m (Tsh. 151,522,000,000)

Atakuwa beki wa 2 ghali zaidi ktk klabu hiyo baada ya Harry Maguire

Atasaini mkataba wa miaka 5 na kulipwa £120,000 (Tsh. 328,800,000) kwa wiki

#JFSports
👍23😁9🔥3💩2