JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky amewafuta kazi Mkuu wa Idara ya Usalama, Ivan Bakanov na Mwendesha Mashtaka Mkuu, Iryna Venediktova

Amesema hatua hiyo ni kufuatia tuhuma za maafisa wao kushirikiana na #Russia

Soma https://jamii.app/MaafisaUkaine
👍11😢1
CHELSEA YATAKA KUWASAJILI KIMPEMBE NA KOUNDE

Chelsea imetoa ofa ya Paundi Milioni 40 (Tsh. 109,600,000,000) ili kumnasa Beki wa PSG, Presnel Kimpembe (26)

Aidha, imerejea kwenye mazungumzo ya kumsajili Beki wa Sevilla, Jules Kounde (23) anayewaniwa pia na Barcelona

#JFSports
👍8🥰1
ARSENAL MBIONI KUMSAJILI ZINCHENKO

Arsenal ina tumaini la kumsajili Beki wa Manchester City, Oleksandr Zinchenko (25) wiki hii, baada ya kutoa ofa ya Paundi Milioni 35 (Tsh. 95,900,000,000)

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anathamini sana uwezo wa Beki huyo wa Kushoto

#JFSports
👍9🔥1
Kila Julai 18, Siku ya Mandela au Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela inasherehekewa duniani kote kuenzi mafanikio ya Kiongozi huyo

Kwa mwaka 2022, Maadhimisho haya yanaangazia Usalama wa Chakula na Mabadiliko ya TabiaNchi

Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 na kufariki dunia Desemba 5, 2013. Alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya 1994 - 1999

Soma zaidi - https://jamii.app/Mandela2022

#MandelaDay
👍9👏1
GHANA: Visa viwili vya Virusi vya #Marburg vimethibitishwa huku Wagonjwa wote wawili wakiripotiwa kufariki kwa Virusi hivyo vilivyo kundi moja na Virusi vya #Ebola

> Hadi sasa Watu 98 wapo karantini kwa kushukiwa kuugua Ugonjwa huo

Soma https://jamii.app/MarburgGhana

#JFAfya #PublicHealth
👍6😢3🤔1
SUDAN: Idadi ya Watu waliofariki kutokana na ghasia za Kikabila katika Jimbo la Blue Nile imefikia 65 na wengine 150 wamejeruhiwa tangu yalipozuka machafuko

> Chanzo ni mgogoro wa ardhi kati ya Watu wa Kabila la Berti na Haswa

Soma - https://jamii.app/ChaosSudan2022
👍5😢4
#MANDELADAY: Maadhimisho ya kumuenzi Nelson Mandela yalipitishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mnamo Novemba 2009, na Siku ya Mandela imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu 2010

Hatua hiyo ni ishara ya kutambua mchango wake katika nyanja mbalimbali zikiwemo Demokrasia, Amani, Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Haki za Watoto na vita dhidi ya Umasikini

Zaidi, soma > https://jamii.app/Mandela2022
👍13
DE LIGT AKUBALI KUJIUNGA NA BAYERN MUNICH

Juventus imekubali kumuuza Beki wake wa Kati, Matthijs de Ligt (22) kwenda Bayern Munich kwa Paundi Milioni 68 (Tsh. 186,320,000,000)

Atasaini mkataba wa miaka 5 baada ya kukamilisha vipimo vya afya anavyotarajia kufanya leo

#JFSports
👍2👎1🎉1
WAZIRI UMMY: UGONJWA WA MKOANI LINDI NI HOMA YA MGUNDA

Amesema Vipimo vilivyofanyika vimeonesha Ugonjwa ulioripotiwa siku chache zilizopita Mkoani Lindi ni Homa ya Mgunda (Leptospirosis)

Imeelezwa kuwa, Ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa Wanyama mbalimbali wakiwemo Panya na Swala. Mtu anaweza kuupata kwa kugusa Mkojo, Maji, Udongo au Chakula kilichochafuliwa na mkojo wa Wanyama wenye Maambukizi

Soma - https://jamii.app/HomaMgunda

#JFAfya
👍19
SUDAN YAFUNGUA MPAKA WAKE NA ETHIOPIA

Mpaka wa Gallabat ulifungwa Juni 27, 2022 baada ya Sudan kuishutumu Ethiopia kwa kuwanyonga Wanajeshi wake 7

> Hatua hiyo ni baada ya Viongozi wa nchi hizo kukubaliana kutatua mzozo maeneo ya mpakani

Soma https://jamii.app/MpakaSudanEthiopia

#JFDiplomasia
👍6
DAR: Serikali imekata rufaa kupinga Mahakama ya Kisutu kumfutia Kesi ya Uhujumu Uchumi Jitesh Jayantilal Ladwa (wa Hoteli za Golden Tulip) ikidai Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kutoa uamuzi huo

> Alikuwa anakabiliwa mashtaka 24 yakiwemo ya kujihamishia Hisa za Wanahisa wenzake

Soma https://jamii.app/SerikaliRufaa
👍3
Siku ya Mandela inalenga kuhamasisha watu wote kuchukua hatua na kuleta mabadiliko katika Jamii kwani kila mmoja ana uwezo kufanya hivyo

#MandelaDay
👍10🎉2😁1
TETESI: RONALDO ANATAKA KUICHEZEA ATLETICO

Inadaiwa Cristiano Ronaldo anamshawishi Kocha Diego Simeone ili amsajili kwa ajili ya kuichezea Atletico Madrid msimu ujao

> Anataka kuondoka Man. United ili apate nafasi ya kucheza UEFA Champions League

Soma https://jamii.app/UsajiliWaCR7

#JFSports
👍8
Idara ya Ujasusi ya DR-Congo inamshikilia Mwanahabari wa Marekani, Stavros Nicolas Niarchos (33) kwa kudaiwa kukaribia makundi yenye silaha Kusini Mashariki mwa nchi hiyo

> Anadaiwa kuwasiliana na Wanamgambo wa Bakata Katanga

Soma - https://jamii.app/USJournalistDetained

#PressFreedom
👍5
MWANZA: Maombi ya Diana Bundala 'Mfalme Zumaridi' ya kutokuwa na imani na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Monica Ndyekobora yameshindwa kupata majibu baada ya Hakimu huyo kusema alipata changamoto ya kiafya

> Maamuzi yatatolewa Julai 27, 2022

Soma https://jamii.app/KesiYaZumaridi
👍6
UINGEREZA: Hali ya Joto inatarajiwa kuwa Nyuzi Joto 43 kwa siku ya Jumanne Julai 19, 2022 ikiwa ni hali ya joto kali kuwahi kutokea katika historia ya Nchi hiyo

> Mamlaka ya Hali ya Hewa Uingereza imesema leo Julai 18, 2022 hali ya joto ni Nyuzi Joto 40

Soma https://jamii.app/JotoUK

#ClimateChange
👍4🔥3👎2
TARIME: Watu 6 waliodaiwa kuwa Majambazi Sugu wa Mifugo wamehukumiwa kwenda jela miaka 70 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha aina ya bunduki na mapanga

> Washtakiwa hao walifanya fujo Mahakamani hapo kupinga hukumu kabla ya kudhibitiwa

Soma - https://jamii.app/MaraMahakamani

#JFMatukio
👍15🥰2😁1
SOMALIA: Ndege ya Shirika la Ndege la Jubba imeanguka wakati ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden Adde Jijini Mogadishu ilipokuwa ikitokea Baidoa

> Watu 36 katika ndege hiyo wameokolewa

Soma https://jamii.app/NdegeYaanguka
👍6👎2😢2
KENYA: Serikali imepunguza bei ya Unga wa Mahindi kuwa Ksh. 100 (Tsh. 1,944) kwa Kilogram Mbili kutoka Ksh. 210 (Tsh. 4,084) iliyokuwa awali

> Hatua hii ni ili kukabiliana na mfumuko wa bei uliotokea hivi karibuni

Soma https://jamii.app/BeiYaUngaKE

#Governance
👍13😁9🔥1
HOMA YA MGUNDA NI NINI?

Ni Ugonjwa unaoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu

Homa ya Mgunda 'Leptospirosis' husababishwa na Bakteria aina ya 'Leptospira interrogans'

Baadhi ya dalili zake ni Homa, Maumivu ya Kichwa na Misuli, Uchovu na kutokwa damu puani

Fahamu zaidi - https://jamii.app/UgonjwaHomaMgunda

#JFAfya #PublicHealth
👍4