JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IMF YAIDHINISHIA TANZANIA MKOPO WA TSH. TRILIONI 2.4

Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 1.046 (Takriban Tsh. 2,422,536,000,000) kwa #Tanzania katika kipindi cha miezi 40 kusaidia kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine

Vita hiyo imetajwa kukwamisha Uchumi wa Tanzania kuimarika kufuatia mlipuko wa #COVID19

Soma - https://jamii.app/IMF-TZMkopo
😁21👍7👏1
HOMA YA MGUNDA: BINADAMU ANAPATAJE MAAMBUKIZI?

1) Kugusa mkojo/maji maji mengine ya mwili kutoka kwa wanyama walioambukizwa

2) Kugusa Maji, Udongo au Chakula kilichochafuliwa na mkojo wa Wanyama

3) Kunywa Maji yaliyochafuliwa na Bakteria wa Homa Ya Mgunda

Fahamu zaidi - https://jamii.app/UgonjwaHomaMgunda

#JFAfya #PublicHealth
👍3
Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuipa Ukraine msaada zaidi wa Kijeshi wa Dola Milioni 508 (Tsh. Trilioni 1.17)

> Pia, Nchi Wanachama zimekubalina kuongeza vikwazo ikiwemo kuzuia dhahabu ya Urusi kuzuiwa kuuzwa Ulaya

Soma https://jamii.app/EUUkraine2022

#RussiaUkraineWar
👎4👍3
SPURS YAENDELEA KUJIIMARISHA, YAMSAJILI SPENCE

Tottenham imemsajili Beki, Djed Spence (21) kutoka Middlesbrough kwa Paundi Milioni 20 (Tsh. 55,400,000,000)

Spurs tayari imewasajili Ivan Perisic, Fraser Forster, Yves Bissouma, Richarlison na Clement Lenglet (Mkopo)

#JFSports
👍5
PAKISTAN: Miili 20 imeopolewa na takriban Watu 30 hawajulikani walipo baada ya mashua iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu 100 wa ukoo mmoja kupinduka kwenye Mto Indus

> Boti hiyo iliyojaa mizigo ilikuwa ikielekea katika harusi ya kifamilia

Soma https://jamii.app/VifoPakistan
😢9🤯4👍2👎1
IVORY COAST: Wanaharakati wa Haki za Wanawake wamesema Muswada unaopendekezwa wa kuhalalisha na kurejesha tena ndoa za wake wengi kwa Wanaume ni kurudisha nyuma jitihada za Vita ya Usawa wa Kijinsia

> Ndoa hizo zilipigwa marufuku nchini humo 1964

Soma https://jamii.app/MswadaIvoryCoast

#GenderEquality
😁9
Mtazamo hasi kuhusu Wosia unatajwa kusababisha migogoro mingi katika jamii, huku Watoto na Watoto wakiathiriwa zaidi

> Nini Mtazamo wako kuhusu kuandika Wosia? Unafikiri sababu nyingine zinazopelekea watu wachache kuwa na Wosia ni zipi?

> Je, wewe upo tayari kuandika Wosia?

Soma https://jamii.app/ElimuYaWosia

#JFSheria
👍8
ARUSHA: Diwani wa Kata ya Mswakini, Nanga Mollel amethibitisha vifo vya Watoto watano wa Familia moja Wilayani Monduli, ikidaiwa walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya tumbo

Inadaiwa vifo hivyo vimetokea kwa siku tofauti (Julai 5, 16, 17 na 19, 2022)

Soma https://jamii.app/VifoWatotoArusha
😢8👎7👍1
BARIDI KUONGEZEKA IRINGA, NJOMBE NA MBEYA

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, imesema hali ya hewa inatarajiwa kufikia viwango vya 4°C katika Mikoa hiyo

Kwa sasa viwango ni Njombe 15°C, Iringa 20°C na Mbeya 21°C

Soma https://jamii.app/BaridiKuongezeka
😁20👍16🤔10😢2🔥1
SIRRO ATEULIWA KUWA BALOZI, WAMBURA AWA IGP MPYA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)

Aliyekuwa IGP, Simon Sirro ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe

Soma https://jamii.app/UteuziIGPMpya

#Governance
👍22😁8🤩5🤬3🤔2
SRI LANKA: Usalama umeonekana kuimarishwa eneo la Bunge wakati Wabunge wakijiandaa kupiga Kura itakayoamua nani atakuwa Rais

Miongoni mwa wagombea watatu wa Urais ni Rais wa Mpito, Ranil Wickremesinghe ambaye anaonekana kutoungwa mkono na Wananchi wengi

Soma - https://jamii.app/UraisKuraSL

#Democracy
👍14😁1
ANGOLA: Hatimaye Watoto wa Rais wa zamani, José Eduardo dos Santos wamekubali baba yao azikwe Mjini Luanda lakini baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 24, 2022

> Hapo awali familia hiyo ilisema Rais huyo alitaka kuzikwa Mjini Barcelona-Uhispania

Soma https://jamii.app/FamiliaDosSantos
👍8😁1
SRI LANKA: Bunge limepiga Kura na kumpitisha rasmi Ranil Wickremesinghe ambaye amehudumu kama Waziri Mkuu kwa mara 6 kuwa Rais wa Nchi hiyo, akimshinda Mpinzani wake mkuu, Dullas Alahapperuma kwa Kura 134 - 82

Wabunge wamemchagua licha ya Raia wengi kuonesha wazi hawamuungi mkono

Soma - https://jamii.app/UraisKuraSL

#Democracy
👍13🤔2😁1
RAIS SAMIA: MFUMO WA TAASISI ZA HAKI JAMII KUFANYIWA MAGEUZI

Amesema miundo ya Taasisi hizo zinazojumuisha Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Magereza na nyinginezo itatazamwa ili kuona kama inaleta ufanisi

Ameeleza, "Tutatizama wale tuliowaamini kwenye maeneo hayo, mifumo yao ya ajira, mafunzo, maadili na nidhamu zipoje"

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#Governance
👍11
RAIS SAMIA: UPANDISHWAJI VYEO JESHINI KUANGALIWA

Akizungumza baada ya uapisho wa Viongozi Rais Samia amesema, "Nimetizama kila ninapokwenda, Mtu anakaribia kustaafu lakini bega lipo tupu. Nikawa nasema upandishwaji vyeo upoje kwenye haya Majeshi?"

Aidha, amesema uhusiano kati ya Raia na Taasisi za Haki Jamii utaangaliwa kwani malalamiko yamekuwa mengi

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#Governance
👍14😢1
RAIS SAMIA: TUTACHUJANA KUJENGA MAJESHI YENYE SIFA

Amesema upatikanaji wa Watenda kazi kwa Majeshi yote utatazamwa ili kujenga majeshi yenye sifa na hadhi ya kusimamia Nchi

Amesisitiza, "Kama yalishapita, huko mbele tutachujana vizuri"

Pia, amegusia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Polisi barabarani akisema, "Hudhani kama ni Mhitimu wa Chuo"

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluLeo

#JFUwajibikaji
👏13👍5🤮1
KUONGEA MWENYEWE NI HALI YA KAWAIDA?

Kwa mujibu wa Jariba la Medical News Today, ni kuwa mara nyingi mtu kuongea peke yake ni tabia ya kawaida yenye manufaa mbalimbali ikiwemo kukusaidia kutafakari

Hata hivyo, baadhi ya Watu wanaweza kuona kuongea mwenyewe kunaathiri #AfyaYaAkili ikiwa kauli ni hasi na za kujikosoa wakati wote

Fahamu zaidi > https://jamii.app/SelfTalkJF

#JFAfya #PublicHealth
👍18
Mdau wa Jukwaa letu la Ajira ametoa ushauri kuhusu Lugha za Mwili (Body Language) ambazo ni vizuri kuzikwepa au kutozionesha wakati wa Usaili wa Kazi kwa kuwa zinaweza kutoa tafsiri hasi kwa wanaokusaili

Msome hapa - https://jamii.app/ElimuYaAjira

#JFMdau #Ajira
👍18
NIGERIA: Padri John Mark Cheitnum amekutwa amefariki ktk Jimbo la Kaduna ikiwa ni siku chache tangu iliporipotiwa kuwa ametekwa Julai 15, 2022

> Padri mwenzake ambaye walitekwa pamoja, Donatus Cleophas akifanikiwa kutoroka

Soma https://jamii.app/PadriAuawaNigeria
😢12👍8🥰1😁1😱1
UCHAGUZI KENYA: Mgombea Mwenza wa Urais wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua amesema Rais Kenyatta alijaribu kumtisha kuhusu kumuunga mkono Ruto

> Amesema Kenyatta anatumia Mfumo wa Sheria ya Jinai kukabiliana na wale ambao hawakubaliani naye

Soma https://jamii.app/GachaguaKenyattaSaga

#Democracy
😁4👍2🤔1